Pac the Don
JF-Expert Member
- Feb 17, 2021
- 6,170
- 7,710
Daaah mkuu ungekua angalau unaish bongo usingeandika hivi, si ajabu utakua unaishi Cambodia ww??Huyu askofu ni mnafiki balaa yani,kipindi magufuli yupo hai alikua
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Daaah mkuu ungekua angalau unaish bongo usingeandika hivi, si ajabu utakua unaishi Cambodia ww??Huyu askofu ni mnafiki balaa yani,kipindi magufuli yupo hai alikua
Askofu ungemwambia tu bila kumficha, kuna watu wengi mno wamefungwa hadi maisha, wengive vifungo virefu na wengine wanasota magelezani - mambo ya UCHAGUZI Mkuu uliopita- ameshaombwa haya mambo kwa muda mrefu sana ila sijui nini kinamkwambisha.“Nikikuombea uwe na afya njema na uwe mnyenyekevu lakini pamoja na madaraka hayo makubwa uliyonayo usikubali kamwe kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile usikubali."
Brother una akili sana hongera, Nyerere aliwahi kusema kabisa kwamba aliingizwa Chaka na wasaka fursa na hili lilimpata Magu alikuwa akizungukwa na machawa hadi kerohapa Tanzania ni vigumu ukiwa kiongozi ukatae misifa kwa sababu watu wengi wanafiki sana
hata Nyerere alisema kuna kipindi walimuingiza kingi, "Mwalimu ukistaafu nchi itabaki na nani ?"mwisho wa siku anasema aligundua walikuwa ni wachumia tumbo
Hapana. Neno Mtukufu lilitumika sana kipindi cha awamu ya pili. Nakumbuka mwaka 1995 tena ilikuwa mwezi November kama sikosei siku Rais Mkapa (RIP) anataka kutangaza Baraza lake la Mawaziri la kwanza ndiyo ametoka tu kuchaguliwa October 1995 ndipo ALIPOLIPIGA MARUFUKU neno MTUKUFU baada ya MC (yule aliyekuwa anaendesha hiyo event sijui hata anatakiwa kuitwaje) alivyomuaddress kama Mtukufu Rais. MC alikuwa anamkaribisha ili ahutubie na kutangaza Baraza la Mawaziri.Nyerere hakuitwa mtukufu.
Enzi za Nyerere viongozi na watu wote walikuwa wanaitwa Ndugu.
Mtukufu na waheshimiwa mlianza kipindi cha Mkapa.
Nani aliwahi kujifananisha na Mungu Tz?
Mheshimiwa Nyerere alikataa, ilirudi wakati wa mkapa.... kizazi cha lini wewe? Official salutation ya Nyerere ilikuwa Mwalimu or Ndugu or (rarely) Mheshimiwa na sio vingenevyo!
Huyu askofu ni mnafiki balaa yani,kipindi magufuli yupo hai alikua kimya
Askofu severine kachanganyikiwa yeye kwanza ajitambue asimuite yesu mungu. anajua yesu hataki kuitwa mungu na ndani ya biblia yesu kawaeleza wazi kuwa mungu yupo.
Lakini askofu bado anamwita binadamu mungu halafu leo anakuja kusema mbele ya mama samia usifananishwe na mungu. binadamu hawezi kuumba mbingu wala hawezi kulipeleka jua au kulizuia jua lisitoke mnaenda kumuita mungu askofu sahihisha kwanza hapo
No hiyo sidhani kama yeye alipenda. Ni kama Mama alivyokaa kimya kuacha Dkt Magufuli adhalilishwe sidhani kama anamaanisha hakumpendaMagufuri. Aliwahi kuitwa Mungu na Waziri Fulani na Wala hakukanusha. Pia amewahi kuitwa Yesu na mbunge mmoja wa CCM , tena kwa kusema jina la Magufuri libarikiwe.
Nadhani kwa mazingira ya ibada haina tatizo kuwa-address hivyo kwa ujumla wao (the people) ila sio mmoja mmoja.Mheshimiwa Nyerere alikataa, ilirudi wakati wa mkapa.
Ila Kuna hii wakati wa mawaidha... "Watukufu waislam"! Hii ni sawa?
Wakati wa Nyerere ilikuwa ni NDUGUNyerere alitwa mtukufu rais mpk anang'atuka na hakuna lolote lililompata.
Ni unafiki wetu tu wanadamu tunaweza kutukuza kitu kwa mdomo lakini moyoni hakuna kitu.
Uzuri hilo neno liliisha ondolewa tangu awamu ya tatu.
[emoji38][emoji38][emoji38] we jamaa kichwani mwako hamna kituHakuna binadamu asiyependa kutukuzwa awe mbunge au mchungaji,padre ,askofu ,mbunge,shehe nk au mtu wa kawaida ndio maana hata maaskofu husujudiwa watu wanapobusu Pete yake hupiga magoti kuibusu Pete
Hivi sahihi mwanadamu kumpigia magoti mwanadamu mwenzie ville?
Na hupenda kuitwa Baba Askofu,baba padre au Baba mchungaji wakati hawakuwazaa
Mkuu Achana naye huyo, ukute Anataka kupima watu watasemaje.Kwanini usiendelee kufuatilia singeli mkuu. Yani hujui Jiwe alivyokuwa anamchukia Askofu Niwemugizi mpaka akaitwa sio raia uhamiaji wakamchunguza. Tanzania hii kuna maaskofu wawili walikuwa strong ni Askofu Niwemugizi na Askofu Bagonza, wote majirani ila makanisa tofauti
Huyu ni baadhi ya Maaskofu wachache sana Wakatoliki ninao wakubali wanajitambua.Ameyasema hayo leo katika Jubilee inayofanyika Mkoani Kagera, ambayo pia imehudhuriwa na Mh Rais
===
skofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kutokubali kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile.
Amesema hayo leo Jumanne Februari 22, 2022 katika sherehe za Jubilee ya miaka yake 25 inayofanyika wilayani Ngara mkoani Kagera.
“Nikikuombea uwe na afya njema na uwe mnyenyekevu lakini pamoja na madaraka hayo makubwa uliyonayo usikubali kamwe kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile usikubali."
"Ninakumbuka sana Hayati Benjamini Mkapa najua huko mlikuwa mmezoea mtukufu rais, mtukufu rais alifika mahali akawa mkali kabisa mtukufu ni Mungu tu naomba hilo liwe neno kwako, " amesema Askofu Niwemuguzi.
Huku akiwa makini amesisitiza,"basi nakuombea Mungu akusaidie kukuza upendo kati ya Watanzania unaotuongoza, ukuze haki nayo haki izae amani na utulivu na kukuza demokrasia katika nchi yetu."
“Ukuze upendo na mshikamo wa Watanzania ili hatimaye utumishi wako utukuke na kuacha alama itakayoonwa kwa vizazi vingi.
Mungu akujalie hekima na uvumilivu wa kusikiliza hata yale yanayokela masikio yako, unajua sisi watoto wako tuko wakorofi, Mungu akujalie tu hekima na uvumulivu hasa pale unapokuwa ni ushauri wenye nia njema ya kulijenga Taifa letu liendelee kuheshimika ndani na nje.”
PIA SOMA
- Rais Samia akataa kutukuzwa, asema yeye hawezi kujilinganisha na Mungu
View attachment 2127421
Lakini mkuu, Nyerere aliikataa ile kauli mbiu ya 'Zidumu fikra za mwenyekiti'.Nyerere alitwa mtukufu rais mpk anang'atuka na hakuna lolote lililompata.
Ni unafiki wetu tu wanadamu tunaweza kutukuza kitu kwa mdomo lakini moyoni hakuna kitu.
Uzuri hilo neno liliisha ondolewa tangu awamu ya tatu.