#COVID19 Askofu Niwemugizi, asitisha Misa na Ibada zote Jimbo la Rulenge, awataka waumini Wasali Majumbani pia Wajikinge na Corona

#COVID19 Askofu Niwemugizi, asitisha Misa na Ibada zote Jimbo la Rulenge, awataka waumini Wasali Majumbani pia Wajikinge na Corona

Huyo Askofu ndio amefanya tulilokuwa tunataka waumini. Viongozi wa dini hawakupaswa kukaa bila kujiongezea kwa kutegemea hisani ya wanasiasa wanaosaka huruma ya viongozi wa dini. Hongera baba askofu kwa kung'amua mtego wa wanasiasa wachovu.
Wanasiasa ni ndumila kuwili, kuna siku watawageuka,watawambia kwanini hawakufunga ibada za jumapili na Pasaka kama alichofanya huyu Baba Askofu.
 
Safi sana,huu ndio utumishi wa Mungu tunaouhitaji.

Better late than never.

Waumini katika maeneo mengine, mjiongeza,msisubiri taarifa kama hii kwani si kila kiongozi wa dini atafanya hivi katika maeneo yenu.

Viongozi wa madhehebu mbalimbali(RC,KKKT.n.k) wanaokutana kutoa matamko ya pamoja(waraka) kama ya kukemea maovu,kukemea wanasiasa,n.k,walipaswa kuwa wamekutana na kuja na tamko kama hili; hivyo, tunatumai tangazo hili litatumika kama mfano kwa viongozi wengine wa dini waliobaki.

Baba Askofu,katika hili,umevaa viatu vilivyowapwaya wengi wakiwemo viongozi wa dini na wasio viongozi wa dini.

Hongera sana Baba Askofu!
Haya ni maamuzi ya Balaza la Maaskofu yametokewa juzi, na majimbo yote yametangaziwa na waumini wote nchini wanafahamu.
 
Sema kupindi hiki Dini zetu zipo kwenye majaribu sana esp yale makanisa yakina gwajima full utapeli
 
Askofu angekaimisha ibada kwa shemasi haya ni maamuzi ya kidikteta

Waumini hawajashirikishwa

Papa aingilie kati

Sent using Jamii Forums mobile app
Target ni kuondoa msongamano wa watu,kwani amekwambia yeye anaikimbia Corona mpaka umshauri akaimishe ibada kwa Shemasi?

Huyo ni mteuliwa wa Jimbo husika kanuni za Kanisa zinamruhusu kuchukua na kuidhinisha jambo lolote atakaloona lina manufaa kwa waamini na Kiimani hata Pope hawezi kumuingilia japokuwa amemteuwa ataingilia pale atakapokuwa ameenda tofauti na wakati uliopo,let's say hakuna kitisho chochote then Askofu afute ibada Kanisani hapo itabidi aonywe but siyo kwa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninaumizwa na viongozi wa dini wanafiki wanaowaaminisha watu eti kufanya ibada ni lazima iwe katika jengo la kanisa.

Biblia iko wazi kabisa,kuwa mwili wa mtu ni hekalu la Mungu. Imefika wakati viongozi muache kuwadanganya watu wenu kuwa baraka ama ibada zipo kwenye jengo mliloliita kanisa.

Viongozi wa serikali wamekuwa na hekma na kumcha Mungu,wamewaachia uhuru tumie busara zenu,ila ninachokiona ni kama mnawadhihaki kwa kuruhusu msongamano na kushindwa kabisa kufuata maelekezo.

Tafadhali nawaomba muwe na hekma kama ya askofu Niwemugizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom