Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
ASKOFU NIWEMUGIZI ATAKA WALIOENGULIWA WARUDISHWE WOTE, UCHAGUZI UWE WA HAKI
Mimi naamini kwamba amani msingi wake ni haki. Pale ambapo kuna haki, amani itatawala." Askofu Niwemugizi aiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kutenda haki kwenye mchakato mzima wa kupata viongozi wa nchi oktoba 28,2020.
Wale wanaoenguliwa waenguliwe kwa misingi sahihi, sio kwa sababu za ovyoovyo. Lakini, kwa bahati mbaya picha tunayoiona upande fulani umeathirika sana na hii engua engua, wakati upande mwingine hamna.Hii inaweza kuleta doa katika mchakato mzima wa uchaguzi huu.
Upande flani unaonekana hakuna walioenguliwa, wameenguliwa wa upande mmoja. Tulitarajia mchakato uonekane ni wa haki kabisa tangu wakati wa watu kutafuta kuteuliwa, ionekane kweli watu wameteuliwa kwa haki, na wale wanaoengeuliwa waenguliwe kwa misingi inayokubalika
Ni vizuri wadau wote wahusika wa mchakato wa uchaguzi, kila mmoja afanye wajibu wake, sasa ni bahati mbaya kidogo kwamba tunaongea wakati matayarisho ya awali ya uchaguzi yamekamilika.