NEC walitakiwa wawasaidie kujaza form wagombea na si kuwazuia kugombea. Mbona tukienda kupata huduma sehemu zinazotuhitaji kujaza form kama huelewi jambo kwenye form unarudi kwa wahusika kuwauliza namna sahihi ya kujaza form na unapewa maelekezo ili form yako ikamilike vizuri, Mfano umeacha tarehe, hujaandika labda mwaka wa kuzaliwa, hujaweka picha nk. Vyote utaambiwa kuvikamilisha ili swala lako likamilishwe. LAKINI NEC wamefanya kugombea kama mashindano ya kufanya mtihani kumbe ni swala la kikatiba na mtu hawezi kuenguliwa kwa sababu ya kukosea kujaza form labda asiwe na sifa ya kugombea.