Uchaguzi 2020 Askofu Niwemugizi ataka walioenguliwa wote warejeshwe kwenye kinyang’anyiro, Uchaguzi uwe wa Haki

Uchaguzi 2020 Askofu Niwemugizi ataka walioenguliwa wote warejeshwe kwenye kinyang’anyiro, Uchaguzi uwe wa Haki

Ukweli ndio huo sasa watahaha kutafuta uraia wake
 
Anayefananisha siasa na Mpira wa miguu hajielewi. Siasa ni maisha
Hahaha haya bhana kama unajua ni maisha kwa nini uweke mtu ambae hajui hata kujaza form?
Sasa huyi ataweza kusaidia maisha yako?
 
Hahaha haya bhana kama unajua ni maisha kwa nini uweke mtu ambae hajui hata kujaza form?
Sasa huyi ataweza kusaidia maisha yako?
Haahaa kwani uchaguzi ni mtihani? Hii tume imeshindwa kazi, huwezi wapitishia wananchi viongozi wao kwa kigezo cha kujaza fomu vizuri.Hata Benki watu na elimu zao hukosea kujaza fomu za kutolea pesa na wasaidizi was Benki huwaelekeza.
 
Vipi kamanda Askofu Shoo na kamanda Mwamakula, wamesemaje hao maaskofu makamanda 😂?
Haaahaa, vipi askofu gwajima? Maana juzi kajaribu kuhonga mashekh kawe ili wampigie kura baada ya kuhaidi kugeuza misikiti kuwa Sunday school
 
Vipi kamanda Askofu Shoo na kamanda Mwamakula, wamesemaje hao maaskofu makamanda 😂?
Unatuaminisha kuwa watetea Haki wote ni CDM?CCM huwa inatetea uovu na waovu ambao wamepachikwa mjina la wasojulikana.
 
Kwamba kamanda Askofu anataka kuwapangia NEC, kama mtu hana umakini kwenye kujaza tu fomu hawezi pia kuwa na umakini kwenye mambo muhimu mengine ya uongozi.
Waacheni wananchi wawachuje hao wasiokuwa na umakini wa kughushi tunaoaminishwa na Tume na Watu wake.Wapiga kura wanafahamu wasiofaa kuwa viongozi.
 
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwetu ninyi nyote mnaosoma uzi huu ama kijiswali hicho kidogo. Asalaam alaykm!

Nataka niulize kajiswali kadogo. Je, kazi za wasimamizi wa uchaguzi ni kuwaengua wagombea kwa mitego midogo midogo au kuwasaidia ili wapate sifa za kugombea?

Ni kwanini wasimamizi wa uchaguzi anapoona mgombea amekosea kujaza form au kuna kitu amekisahau asichukue nafasi yake kama kiongozi kumwelekeza ajaze vizuri? Anashindwa nini kumpigia simu kamaameondoka arudi ili aijaze vizuri?

Kwanini refa ndio anakua adui wa mchezaji badala ya kumwelekeza kufuata utaratibu?

Kwanini refa ndio anamtegeshea penati mchezaji?

Nia ni kuwaengua au kupata wagombea watakaoshindana ili mshindi apatikane kwa njia halali?

Ni sahihi kuwachagulia wananchi mgombea badala ya wao?
Wakukujibu hayupo,Polepole yupo busy na kampeni za Baba yao,hawa waliotumwa na Bashiru ni wepesi kwenye kujibu maswali kama hayo.
 
Kwamba kamanda Askofu anataka kuwapangia NEC, kama mtu hana umakini kwenye kujaza tu fomu hawezi pia kuwa na umakini kwenye mambo muhimu mengine ya uongozi.
Mkuu unaamini kweli ktk hili?
Yaani Mh Msukuma (MB) na std 7 ajaze fomu kwa usahihi kuliko Mh Devotha Minja (MB) a University graduate !!

CCM wakati fulani iache Upimbi yaani ndo chama pekee chenye wabunge zaidi ya 6 std 7 halafu eti wako sahihi zaidi kuliko wagombea wa Upinzani wenye elimu zaidi yao tena Kwa mbali zaidi !!

Huyu Mnyampara wa Barabara aache ku-panic ajue limemfika !!
 
Kwamba kamanda Askofu anataka kuwapangia NEC, kama mtu hana umakini kwenye kujaza tu fomu hawezi pia kuwa na umakini kwenye mambo muhimu mengine ya uongozi.
Yaani akitokea mtu akasema kweli bac Ni kosa nchi hii bhana
 
ASKOFU NIWEMUGIZI ATAKA WALIOENGULIWA WARUDISHWE WOTE, UCHAGUZI UWE WA HAKI

Mimi naamini kwamba amani msingi wake ni haki. Pale ambapo kuna haki, amani itatawala." Askofu Niwemugizi aiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kutenda haki kwenye mchakato mzima wa kupata viongozi wa nchi oktoba 28,2020.

Wale wanaoenguliwa waenguliwe kwa misingi sahihi, sio kwa sababu za ovyoovyo. Lakini, kwa bahati mbaya picha tunayoiona upande fulani umeathirika sana na hii engua engua, wakati upande mwingine hamna.Hii inaweza kuleta doa katika mchakato mzima wa uchaguzi huu.

Upande flani unaonekana hakuna walioenguliwa, wameenguliwa wa upande mmoja. Tulitarajia mchakato uonekane ni wa haki kabisa tangu wakati wa w
Atuoeatu kutafuta kuteuliwa, ionekane kweli watu wameteuliwa kwa haki, na wale wanaoengeuliwa waenguliwe kwa misingi inayokubalika

Ni vizuri wadau wote wahusika wa mchakato wa uchaguzi, kila mmoja afanye wajibu wake, sasa ni bahati mbaya kidogo kwamba tunaongea wakati matayarisho ya awali ya uchaguzi yamekamilika.

Atupe mrejesho wa Corona kwanza. Tanzania nzima halikuwa na lockdown. Ila yeye alikataza watu wasiende kusali. Askofu ana ajenda gani sijui!
 
Anaamini Roma inatawala dunia hadi leo
"Askofu Ataka..."
Heil JPM
ASKOFU NIWEMUGIZI ATAKA WALIOENGULIWA WARUDISHWE WOTE, UCHAGUZI UWE WA HAKI

Mimi naamini kwamba amani msingi wake ni haki. Pale ambapo kuna haki, amani itatawala." Askofu Niwemugizi aiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kutenda haki kwenye mchakato mzima wa kupata viongozi wa nchi oktoba 28,2020.

Wale wanaoenguliwa waenguliwe kwa misingi sahihi, sio kwa sababu za ovyoovyo. Lakini, kwa bahati mbaya picha tunayoiona upande fulani umeathirika sana na hii engua engua, wakati upande mwingine hamna.Hii inaweza kuleta doa katika mchakato mzima wa uchaguzi huu.

Upande flani unaonekana hakuna walioenguliwa, wameenguliwa wa upande mmoja. Tulitarajia mchakato uonekane ni wa haki kabisa tangu wakati wa watu kutafuta kuteuliwa, ionekane kweli watu wameteuliwa kwa haki, na wale wanaoengeuliwa waenguliwe kwa misingi inayokubalika

Ni vizuri wadau wote wahusika wa mchakato wa uchaguzi, kila mmoja afanye wajibu wake, sasa ni bahati mbaya kidogo kwamba tunaongea wakati matayarisho ya awali ya uchaguzi yamekamilika.

Back
Top Bottom