Askofu Renatus Nkwande asikitishwa na uongo wa Polisi kuhusu wana CHADEMA waliokamatwa ndani ya Kanisa

Kasi ya Polisi kumharibia Mama ni ya 5G. Sukuma Gang wamejipanga vizuri kweli kweli
 
"Wakati wanakwenda kunawa polisi wakavamia eneo hilo na kuanza kukamata kila aliyekuwa na sare za Chadema. Awali asubuhi,

walikwishakamata wanachama watano akiwemo mama yake mzazi na John Pambalu ambaye naye alikuwa anaigia kanisani hapo kwa ajili ya ibada hiyo"

Nimesoma hicho kipande Cha mama ake John Justin pambalu kukamatwa nimesikitishwa Sana yule mama namfahamu ni mkatoliki kindakindaki na sio mtu wa Virugu....

Yule mama kwa jinsi Alivyo walea watoto wake naenda mitaa ya butimba watoto wake ni mifano ya kuigwa sijawai kumsikia mtoto ake hata mmoja kitukana matusi yeyote hata Hili neno K*m* hawawezi kulitaja Wala kulitukana popote mafichoni wala hadharan.....

Profesa Lipumba mwenyewe anajutia kuingia kweny siasa za upinzani Tz.....

Gharama za kufanya siasa za upinzani ni kubwa mmo Africa.......Binafsi Kwa tafsiri yangu naona kuwa mpinzani in third world country kwa kijana ni kuhatarisha your destiny.
 
Mpaka sasa hivi tunaendelea kushughulikia sakata la kukamatwa kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA walipokuwa kwenye misa jana Kawekamo, Mwanza. Waliopo mahabusu ni katibu wa kanda ya Victoria, Mwenyekiti wa Ilemela, katibu wa Nyamagana na wanachama wengine jumla yao ni 20.

OCD asubuhi ya leo, alitueleza wanatuhumiwa kwa kufanya vurugu kanisani na kwamba alipigiwa simu na viongozi wa kanisa. Ilibidi tukauone uongozi wa kanisa Katoliki jimbo la Mwanza, tumeonana na msaidizi wa baba Askofu na akatuwezesha kuongea na askofu Mkuu Renatus Nkwande.

Askofu mkuu jimbo katoliki Mwanza, Renatus Nkwande amesikitishwa sana na uongo wa jeshi la polisi na kuthibitisha kwamba hakukuwa na vurugu yoyote kwenye misa hiyo. Na alipokea matoleo ya wanachama hao wa Chadema na kusali pamoja nao. Akawakaribisha wale chakula pamoja nae.

Wakati wanakwenda kunawa polisi wakavamia eneo hilo na kuanza kukamata kila aliyekuwa na sare za Chadema. Awali asubuhi, walikwishakamata wanachama watano akiwemo mama yake mzazi na John Pambalu ambaye naye alikuwa anaigia kanisani hapo kwa ajili ya ibada hiyo.

Baba askofu Renatus Nkwande kamuelekeza msaidizi wake tukaenda naye hadi Kirumba na ameongea na OCD, sasa OCD akageuza kwa si kanisa lilimpigia simu bali ni waumini wawili mmojawapo anaitwa Gerald Joseph na kusema kanisani kuna wana CHADEMA wanaleta vurugu, hivyo wanataka msaada.

Msaidizi wa Askofu Renatus Nkwande, kawasiliana na (OCD) sasa Askofu mkuu jimbo katoliki Mwanza, Nkwande amemtuma katibu wake, Padre Nyanda na tunaendelea kumsubiri hapa Kirumba.

Tumemueleza Baba Askofu masuala kadhaa, lakini pia jinsi ambavyo tunaona inapendeza watu kutendewa

1. Jeshi la polisi liwaachie wote bila masharti yoyote (kwa kuwa hakuna kosa kisheria ambalo wamevunja)

2. Au ikiwezekana, baba Askofu, jimbo katoliki Mwanza, Renatus Nkwande, akawadhamini waumini wake.

Tutaendelea kuwajulisha kila hatua. Ahsante.
Mamaake Pambalu si akasali Parokia ya Butimba ambako ndo jirani na nyumbani kwake
 
Mimi ni Mkatoliki ila nawaomba sana Kanisa Katoliki nchini Tanzania wasiingizwe katika Mtego huu wa Mzozo wa Kisiasa baina ya CHADEMA na Mamlaka zote zilizo chini ya Serikali ya Chama Tawala cha CCM. Kuna Hatari naanza Kuiona.
Hatari gani unayoiona?
Mbele za Mungu itasimama haki na siyo dhurma,kutetea haki ni moja yakazi waliyotumwa viongozi wa dini

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Mimi ni Mkatoliki ila nawaomba sana Kanisa Katoliki nchini Tanzania wasiingizwe katika Mtego huu wa Mzozo wa Kisiasa baina ya CHADEMA na Mamlaka zote zilizo chini ya Serikali ya Chama Tawala cha CCM. Kuna Hatari naanza Kuiona.
Wakulaumiwa ni Jeshi la Polisi. Askofu Mkuu atoe ushahidi wa uongo kisa asiwe upande wa CHADEMA?
 
Hao wanatafuta ugomvi na kutaka kulifitinisha kanisa na serikali, na wala hawasali kutoka rohoni na ni njia tuu mojawapo ya maandamano Kwa mgongo wa kanisa
IVI MAOMBI YAO KWANI HAYAWEZI KUPOKELEWA BILA SARE ZA CHAMA?
Hivi kwa akili yako kuvaa sare za chama ni kosa?
Mbona ccm wanavaa safe zao za chama hadi kwenye misiba?
 
Kwa mtu mwenye akili, ataelewa kabisa kama ni kweli walienda kanisani na SARE basi hawakwenda Kwa ajiri ya kusali but to protest
Tofautisha kati ya msiba na kanisani mheshimiwa
 
Rekebisha hapo boss... Ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza.
 
C
Mpaka sasa hivi tunaendelea kushughulikia sakata la kukamatwa kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA walipokuwa kwenye misa jana Kawekamo, Mwanza. Waliopo mahabusu ni katibu wa kanda ya Victoria, Mwenyekiti wa Ilemela, katibu wa Nyamagana na wanachama wengine jumla yao ni 20.

OCD asubuhi ya leo, alitueleza wanatuhumiwa kwa kufanya vurugu kanisani na kwamba alipigiwa simu na viongozi wa kanisa. Ilibidi tukauone uongozi wa kanisa Katoliki jimbo la Mwanza, tumeonana na msaidizi wa baba Askofu na akatuwezesha kuongea na askofu Mkuu Renatus Nkwande.

Askofu mkuu jimbo katoliki Mwanza, Renatus Nkwande amesikitishwa sana na uongo wa jeshi la polisi na kuthibitisha kwamba hakukuwa na vurugu yoyote kwenye misa hiyo. Na alipokea matoleo ya wanachama hao wa Chadema na kusali pamoja nao. Akawakaribisha wale chakula pamoja nae.

Wakati wanakwenda kunawa polisi wakavamia eneo hilo na kuanza kukamata kila aliyekuwa na sare za Chadema. Awali asubuhi, walikwishakamata wanachama watano akiwemo mama yake mzazi na John Pambalu ambaye naye alikuwa anaigia kanisani hapo kwa ajili ya ibada hiyo.

Baba askofu Renatus Nkwande kamuelekeza msaidizi wake tukaenda naye hadi Kirumba na ameongea na OCD, sasa OCD akageuza kwa si kanisa lilimpigia simu bali ni waumini wawili mmojawapo anaitwa Gerald Joseph na kusema kanisani kuna wana CHADEMA wanaleta vurugu, hivyo wanataka msaada.

Msaidizi wa Askofu Renatus Nkwande, kawasiliana na (OCD) sasa Askofu mkuu jimbo katoliki Mwanza, Nkwande amemtuma katibu wake, Padre Nyanda na tunaendelea kumsubiri hapa Kirumba.

Tumemueleza Baba Askofu masuala kadhaa, lakini pia jinsi ambavyo tunaona inapendeza watu kutendewa

1. Jeshi la polisi liwaachie wote bila masharti yoyote (kwa kuwa hakuna kosa kisheria ambalo wamevunja)

2. Au ikiwezekana, baba Askofu, jimbo katoliki Mwanza, Renatus Nkwande, akawadhamini waumini wake.

Tutaendelea kuwajulisha kila hatua. Ahsante.
CHADEMA amekuwa adui wa Tanzania mahali popote anapoonekana na sare anasababisha vurugu ,hii ni ajabu,tuliwaambia kuwa serikali inakanyaga sheria tukaonekana vibaraka wa wazungu na mabeberu,leo wakitoka makanisani wataingia nyumba kwa nyumba kubaini wafuasi wa chadema na kuwashughulikia ipasavyo.
 
Kuwaamini police ni ngumu Sana wakafanyeje vurugu kanisani
 
C

CHADEMA amekuwa adui wa Tanzania mahali popote anapoonekana na sare anasababisha vurugu ,hii ni ajabu,tuliwaambia kuwa serikali inakanyaga sheria tukaonekana vibaraka wa wazungu na mabeberu,leo wakitoka makanisani wataingia nyumba kwa nyumba kubaini wafuasi wa chadema na kuwashughulikia ipasavyo.
Tozo ni madhara ya ukosefu wa chadema bungeni
 
Kwanini Chadema wamejitoa kuwadhamini watu wao? hata kama wamekamatwa kwa kuonewa kama Mbowe lakini bado jukumu la kwanza lilikuwa ni Chadema wenyewe kuwadhamini watu wao, sio kuelekeza hiyo kazi kwa Kanisa Katoliki, au polisi wawaachie bila masharti, vipi kama wasipoachiwa?
Sidhani kama umesoma sakata lenyewe badala yake umeanza kukurupuka kama uharo kama ilivyo adha yako.
 
Wiki hii polisi wametoa nafasi za ajira.
Qualification. Div 4 kwa 2021 ambapo Kuna div one na two zakumwaga.
Inamaana miaka ya nyuma walikua wanachukua div gani?
 
Back
Top Bottom