Askofu Ruwa'ichi: Watanzania hawashabikii haki, wengi kwa ujinga au kutokujua wanajidai wadau wa amani

Askofu Ruwa'ichi: Watanzania hawashabikii haki, wengi kwa ujinga au kutokujua wanajidai wadau wa amani

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Juda Thaddeus Ruwa'ichi, amesema Watanzania wengi hawashabikii haki wala siyo wadau wa haki.

Amesema wengi wao kwa ujinga, kwa kurubuniwa au vinginevyo wamekuwa wadau wa amani akiweka msisitizo kuwa pasipo na haki hakuna amani.

Askofu Ruwa'ichi ametoa kauli hiyo leo Desemba 24,2025 katika misa maalumu ya mkesha wa Krismasi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

"Sisi tunaoadhimisha Krismasi kuzaliwa kwa mwokozi tunatakiwa kuwa watu wa haki, wewe mwana Dar es Salaam, Mtanzania je, wewe ni mtu wa haki...? Wewe ni mdau wa haki....?

Naomba kuthubutu kusema kwamba Watanzania wengi hawashabikii haki siyo wadau wa haki, Watanzania wengi kwa ujinga au kutokujua wanajidai wadau wa amani," amesisitiza.

1766623353826.png

Askofu Ruwa'ichi ameeleza kuwa hana ugomvi na mtu anayeshabikia amani lakini akiwakumbusha kuwa haiwezekani kuwepo kwa amani bila haki.

Amesema haki na amani ni vitu viwili vinavyotegemeana na vyote hivyo ni zawadi inayofunganamana na Yesu mwokozi.

"Ewe Mtanzania kama utaka kujigamba kuwa mtu wa amani jitose kupigania haki, jitose kusema kweli, amani na yanayompendeza Mungu,"amesema.

Askofu huyo amehitimisha mahuburi hayo akisema Yesu Kristo aliyezaliwa kwa ajili ya wanadamu na anatambulika kwa haki, mwokozi, mwenye upendo na huruma.

Akizungumzia mafundisho hayo muumini wa kanisa hilo, Barnaba Josephat amesema hitaji la haki ni la msingi kwa binadamu kwa kuwa bila haki hakuna amani.

"Amani msingi wake mkuu ni haki, ukitenda haki amani lazima itakuwepo kwahiyo nimejifunza viongozi wetu wa kiroho wanatutaka kusimamia haki na kutoumiza watu wengine, unaweza kuishi katika utulivu lakini huna amani kwa sababu hujatendewa haki," amesema.

Kwa upande wake, Lightness Samson amesema katika kusheherekea Sikukuu za Krismasi ni muhimu Watanzania kuendelea kutenda mema pamoja na kutenda haki.

"Tuishi kwa umoja na upendo kwenye jamii tuilinde amani yetu kwa kutenda haki."
​
 
Naomba kuthubutu kusema kwamba Watanzania wengi hawashabikii haki siyo wadau wa haki, Watanzania wengi kwa ujinga au kutokujua wanajidai wadau wa amani," amesisitiza.
Neno "wanajidai" ndilo sahihi. Hawa wanaoimba "AMANI", siyo "wajinga", na wala siyoujuwa; ni watu wanaojidai tu kuwa AMANI inaweza kuwepo bila ya haki.

Tumeshuhudia ulaghai na hadaa nyingi toka kwa Samia Suluhu Hassan, ambaye kama wao hao wanaoimba amani wanajuwa maana halisi ya wao kukazia AMANI isiyoambatana na HAKI.
Nawweza kusema, pengine chimbuko la tabia hii ya kulaghai na kudanganya inatokana na utamaduni wa kigeni; ambao nia yake ni kulazimisha matakwa ya watawala kwa watawaliwa

Tumemsikia hata Spika wa Bunge, 'Zungu' akilalamikia yaliyosemwa na Jaji Warioba; akihimiza hayo yangesemewa faraghani ili yasizue "taharuki". huo ni utamaduni wa kuvunga watu ili watawaliwe bila kuhoji.

Kwa hiyo, kwa maoni yangu, hili swala la AMANI isiyoshirikisha HAKI, ni njama zilezile za watawala kutaka watawale bila kuhojiwa na yeyote. Wao ndio wawe watu wa kugawa HAKI, pale inapowapendeza wao kufanya hivyo

Ni utamaduni wa kigeni ndio umeingia kututikisa sana safari hii.
, unaweza kuishi katika utulivu lakini huna amani kwa sababu hujatendewa haki," amesema.
Nimeona niyashirikishe haya maneno muhimu sana aliyoyasema Barnaba josephat. Haya maneno ndiyo tafsiri halisi wanayoitafuta hawa wanaoimba AMANI bila ya kuwepo HAKI. Watawala wanataka waTanzania waishi hivyo hivyo kwa uvumilivu mradi AMANI FEKI iwepo; huku mioyo yao ikiwa na maumivu kwa kukosa HAKI.
Tawala za kifalme, hasa huko Arabuni ndiyo hayo wanayoyataka wao.. Sasa samia na yeye anadhani atayaleta hapa waTanzania wayakubali hivyo hivyo hata kama wanaumia kwa kukosa HAKI.

Kuua waTanzania, lengo lake kuu lilikuwa kuwatia woga waTanzania wanyamaze; pawepo na AMANI FEKI, wakati hakuna HAKI.
 
Uislamu unajinasibisha kama dini ya haki Sasa kwakuwa Leo kiongozi ni mwislamu mwenzao wanaikana misingi ya dini yao kwamba haki sio muhimu kesho kiongozi akija kiongozi mkristo watageukia haki na kuikana amani.

Miaka ya tisini wakati chama cha cuf kikiwa na nguvu chini ya maalim self na lipumba walikuwa na kauli mbiu ya HAKIIIIII HAKI SAWA KWA WOTEEE na cuf kilipendwa sana na waislamu kwasababu ya hiyo kaulimbiu inayoambatana na misingi ya dini yao.

Sasa Leo mashehe ubwabwa kwakuwa Samia ni mwislamu mwenzao hawaihubiri amani.

Hakika ELIMU Kwa waislamu inatakiwa ihubiriwe sana hawajitambui hawa watu. Yani ni bendera fwata upepo.
 
Uislamu unajinasibisha kama dini ya haki Sasa kwakuwa Leo kiongozi ni mwislamu mwenzao wanaikana misingi ya dini yao kwamba haki sio muhimu kesho kiongozi akija kiongozi mkristo watageukia haki na kuikana amani. Miaka ya tisini wakati chama cha cuf kikiwa na nguvu chini ya maalim self na lipumba walikuwa na kauli mbiu ya HAKIIIIII HAKI SAWA KWA WOTEEE na cuf kilipendwa sana na waislamu kwasababu ya hiyo kaulimbiu inayoambatana na misingi ya dini yao. Sasa Leo mashehe ubwabwa kwakuwa Samia ni mwislamu mwenzao hawaihubiri amani. Hakika ELIMU Kwa waislamu inatakiwa ihubiriwe sana hawajitambui hawa watu. Yani ni bendera fwata upepo.
Hawa kobazi elimu ndiyo changamoto, umenikumhusha mbali na kauli mbiu ya Cuf ya " Hakii haki sawa kwa wote" leo wanaikataa.
 
Lenyewe limejifungia ndani linakula divai kazi upotoshaji tu, Stupid ruachi

Shetani ujitambulishaye kwa jina la Kimbesa11, umelaaniwa wewe na uzai wako, Mungu wa mbinguni aliye asili ya haki na amani, tunaomba akulipe wewe na uzao wako, sawa na uovu wako wa kuwashambulia wajumbe wa Mungu waihubiriyo haki na amani.
 
Fuatilia comments zake zote huyo Kimbesa11, utagunua kuwa kama siyo mgonjwa qa akili basi shetani ameweka makao katika moyo wake, wakati anawaza uovu dhidi ya watu wema, hakuna jema litokalo katika kinywa chake, ni dalili ya laana.
Laana unayo wewe
Watumishi wa Mungu matepeli mfano wa ruachi tunawapinga hadharani
 
Back
Top Bottom