Askofu Ruwa'ichi: Watanzania hawashabikii haki, wengi kwa ujinga au kutokujua wanajidai wadau wa amani

Uliwahi kuchukua hatua kokote kupeleka huo ushaidi hata katika mahakama za tanzania au nje ya tanzania ili kuweka rekodi sawa au huu ni uzushi tu mnaokaa bavicha na kujitungia halafu mnataka majibu?
Mahakama za maelekezo unapeleka ushahidi gani? Jaji mkuu na muuwaji wanakula meza moja
 
Laana unayo wewe
Watumishi wa Mungu matepeli mfano wa ruachi tunawapinga hadharani

Watumishi wa Mungu kupingwa na mawakala wa shetani kama wewe wala hawashtuki kwani hawategemei wanapoukemea uovu, ninyi watumishi wa shetani muwapongeze au muwaunge mkono, mnafanya wanachokitegemea. Hivyo watafurahi tu kwa kuwa ninyi mawakala wa sjetani mmejua kuwa wao siyo sehemu ya uovu wenu.
 
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Juda Thaddeus Ruwa'ichi, amesema Watanzania wengi hawashabikii haki wala siyo wadau wa haki.

Amesema wengi wao kwa ujinga, kwa kurubuniwa au vinginevyo wamekuwa wadau wa amani akiweka msisitizo kuwa pasipo na haki hakuna amani.

Askofu Ruwa'ichi ametoa kauli hiyo leo Desemba 24,2025 katika misa maalumu ya mkesha wa Krismasi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

"Sisi tunaoadhimisha Krismasi kuzaliwa kwa mwokozi tunatakiwa kuwa watu wa haki, wewe mwana Dar es Salaam, Mtanzania je, wewe ni mtu wa haki...? Wewe ni mdau wa haki....?

Naomba kuthubutu kusema kwamba Watanzania wengi hawashabikii haki siyo wadau wa haki, Watanzania wengi kwa ujinga au kutokujua wanajidai wadau wa amani," amesisitiza.

Askofu Ruwa'ichi ameeleza kuwa hana ugomvi na mtu anayeshabikia amani lakini akiwakumbusha kuwa haiwezekani kuwepo kwa amani bila haki.

Amesema haki na amani ni vitu viwili vinavyotegemeana na vyote hivyo ni zawadi inayofunganamana na Yesu mwokozi.

"Ewe Mtanzania kama utaka kujigamba kuwa mtu wa amani jitose kupigania haki, jitose kusema kweli, amani na yanayompendeza Mungu,"amesema.

Askofu huyo amehitimisha mahuburi hayo akisema Yesu Kristo aliyezaliwa kwa ajili ya wanadamu na anatambulika kwa haki, mwokozi, mwenye upendo na huruma.

Akizungumzia mafundisho hayo muumini wa kanisa hilo, Barnaba Josephat amesema hitaji la haki ni la msingi kwa binadamu kwa kuwa bila haki hakuna amani.

"Amani msingi wake mkuu ni haki, ukitenda haki amani lazima itakuwepo kwahiyo nimejifunza viongozi wetu wa kiroho wanatutaka kusimamia haki na kutoumiza watu wengine, unaweza kuishi katika utulivu lakini huna amani kwa sababu hujatendewa haki," amesema.

Kwa upande wake, Lightness Samson amesema katika kusheherekea Sikukuu za Krismasi ni muhimu Watanzania kuendelea kutenda mema pamoja na kutenda haki.

"Tuishi kwa umoja na upendo kwenye jamii tuilinde amani yetu kwa kutenda haki."
​
Huyu Askofu yeye ndio mjinga ndio maana tulimtolea nje Mwanza ikabidi Vatican wamtoe alikuwa anataka kuiua Hospitali ya Bugando kwa kuchukua mapato na kupeleka kwao Moshi ndio maana yule Sister akaamua kujiua tu baada ya auditing kwa kuwa inasemekana pesa zote alikuwa anachukua yeye. Kwahiyo atukome kabisa kutuita wajinga.
 
Huo ndo ukweli haki kwanza mengine yanakuja baaadae
Hakuna, Amani ndio inatangulia then utapata nafasi ya kutengeneza hizo taratibu na sheria bila amani, haki haitatokea angalia Sudani na Somalia.
 
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Juda Thaddeus Ruwa'ichi, amesema Watanzania wengi hawashabikii haki wala siyo wadau wa haki.

Amesema wengi wao kwa ujinga, kwa kurubuniwa au vinginevyo wamekuwa wadau wa amani akiweka msisitizo kuwa pasipo na haki hakuna amani.

Askofu Ruwa'ichi ametoa kauli hiyo leo Desemba 24,2025 katika misa maalumu ya mkesha wa Krismasi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

"Sisi tunaoadhimisha Krismasi kuzaliwa kwa mwokozi tunatakiwa kuwa watu wa haki, wewe mwana Dar es Salaam, Mtanzania je, wewe ni mtu wa haki...? Wewe ni mdau wa haki....?

Naomba kuthubutu kusema kwamba Watanzania wengi hawashabikii haki siyo wadau wa haki, Watanzania wengi kwa ujinga au kutokujua wanajidai wadau wa amani," amesisitiza.

Askofu Ruwa'ichi ameeleza kuwa hana ugomvi na mtu anayeshabikia amani lakini akiwakumbusha kuwa haiwezekani kuwepo kwa amani bila haki.

Amesema haki na amani ni vitu viwili vinavyotegemeana na vyote hivyo ni zawadi inayofunganamana na Yesu mwokozi.

"Ewe Mtanzania kama utaka kujigamba kuwa mtu wa amani jitose kupigania haki, jitose kusema kweli, amani na yanayompendeza Mungu,"amesema.

Askofu huyo amehitimisha mahuburi hayo akisema Yesu Kristo aliyezaliwa kwa ajili ya wanadamu na anatambulika kwa haki, mwokozi, mwenye upendo na huruma.

Akizungumzia mafundisho hayo muumini wa kanisa hilo, Barnaba Josephat amesema hitaji la haki ni la msingi kwa binadamu kwa kuwa bila haki hakuna amani.

"Amani msingi wake mkuu ni haki, ukitenda haki amani lazima itakuwepo kwahiyo nimejifunza viongozi wetu wa kiroho wanatutaka kusimamia haki na kutoumiza watu wengine, unaweza kuishi katika utulivu lakini huna amani kwa sababu hujatendewa haki," amesema.

Kwa upande wake, Lightness Samson amesema katika kusheherekea Sikukuu za Krismasi ni muhimu Watanzania kuendelea kutenda mema pamoja na kutenda haki.

"Tuishi kwa umoja na upendo kwenye jamii tuilinde amani yetu kwa kutenda haki."
​
Haki ni faida au nafasi mtu anayopewa kisheria au kimaadili, mfano: haki ya kuishi, haki ya elimu, haki ya kusikilizwa.
Wajibu ni jukumu au kazi mtu anayopaswa kutimiza kwa mujibu wa sheria, maadili au makubaliano ya kijamii, mfano: kulipa kodi, kutii sheria, kuheshimu haki za wengine.

Kipi kinaanza?
Wajibu hutangulia haki. Huwezi kudai haki ikiwa hufanyi wajibu wako.

Katiba ya Tanzania 1977, ibara ya 12 hadi 29 inaeleza haki na wajibu.
Mfano, ibara ya 25(1): “Kila mtu ana wajibu wa kushiriki kazi halali ili kujenga jamii.”
Ibara ya 29(1): “Kila mtu ana wajibu wa kuheshimu haki na uhuru wa watu wengine.”

Kumzuia mtu kupiga kura ni kosa chini ya Sheria ya Uchaguzi ya Tanzania, hasa Kifungu cha 73(1) cha The National Electoral Commission Act, Cap 343 kinakataza kuzuia au kuingilia haki ya mtu kupiga kura..
 
Back
Top Bottom