ASKOFU MKUU wa KKKT, Dk. Fredrick Shoo hajasema kuwa Kanisa la KKKT linaunga mkono Mkataba wa Bandari bali amesema wao kama viongozi wa Dini kupitia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania(TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) walionana na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu kasoro zilizoko kwenye mkataba.
Hivyo Askofu Shoo akasisitiza kuwa ushauri na maoni waliyotoa viongozi wa Dini Rais Samia alisema amewakabidhi watalaamu wa Serikali ili kufanyia kazi maoni hayo ya viongozi wa Dini.
Hivyo akatumia fursa hiyo kumkumbusha Mh Rais kufanyia kazi ushauri wa viongozi wa dini ili kuhakikisha uwekezaji unakuwa na tija na maslahi ya Taifa.