Askofu Shoo Hajasema anaunga mkono Mkataba. Kasema uwekezaji

Askofu Shoo Hajasema anaunga mkono Mkataba. Kasema uwekezaji

Ni kama ukienda kucheza miaka mitatu SAUTI. Walipoenda walienda kama TEC, BAKWATA na CCT. Hawakwenda kama taasisi moja bali tatu. Unatarajia kwa utofauti wao pia watoe maoni yao kwa njia moja, wakati mmoja, namna moja?? Huku wakiwa hawana ushawishi wa aina moja, msukumo mmoja na ujasiri wa aina moja...
Umeongea meengi, lakini hujaweka hoja yoyote. Kwani kwenye Waraka wa TEC Kuna mahali wamesema walishauri hivi na imefanyika tofauti? Na je, ukishauriwa, ni lazima ufanye kama ulivyoshauriwa? We wa wapi?

Lini iliishawahi kuwashauri basi hata hao Maaskofu? Wao wenyewe ni madikteta wa hali juu ndani ya Kanisa Katoliki, unazungumzia ushauri? Lini Kanisa Katoliki liliishawahi kuomba ushauri kutoka kwa Walei (yaani wasiojua?) Unazungumza nini wewee?

Eti unaleta hoja za eti mlisoma nini? Ujinga mtupu! Wewe uliyesoma zamani una mchango gani kwenye nchi hii? Mbona mlisoma zamani ndio mmeifikisha nchi hii kwenye umaskini na ufisadi wa hali ya juu?
 
askofu anaoa, ana mke, watoto na ndugu kibao wana mtegemea, hapo ni njaa tu. amna kanisa hapo. tuwe kwakweli. kkkt ni kikundi Cha wahuni.
 
Wew mweny ufaham nikuulize

Kama viongoz wa dini walienda ikulu kupeleaka maoni yao WHY WATOE WALAKA KABLA YA KUJUA KAMA MAONI YAO YAMEFANYIWA KAZI AMA LAA?

I DECLARE HATA KAMA INGEKUA BAKWATA AU TAASISI YOYOTE YA DINI YA KIISLAM NINGEPINGANA NA WALAKA WAO
Kimya nacho ni jibu.
 
Nimesikiliza live hotuba ya askofu mkuu wa KKKT Askofu Shoo. Hakuna mahali amesema kanisa la KKKT linaunga mkono mkataba wa bandari kama ulivyo. Alichosema ni kwamba kanisa linaunga mkono uwekezaji. Na kusema kweli wote wanaopinga mkataba wa bandari hakuna hata mmoja anayepinga uwekezaji!!. Wanapinga baadhi ya vipengele kwenye mkataba vinavyoibana Tanzania.

Hatya waraka wa waaskofu wa kanisa Katoliki hawajasema kuwa wanapinga uwekezaji, bali wanapinga baadhi ya vipengele kwenye mkataba na wameviainisha. Naomba nimnukuu Askofu Shoo alivyosema: "lipo hili la DP World Mheshimiwa…kwanza naomba ieleweke wazi Kanisa linaunga mkono uwekezaji, hatupingingi uwekezaji na tunajua wewe kwenye nia yako unataka uwekezaji, hata hivyo jambo hilo limekuwa na maoni mbalimbali ya wananchi na vyombo vya habari".

Alichosema Askofu Shoo ni kwamba wao pamoja na viongozi wengine wa dini walishawahi kuongea naye na wakatoa mapendekezo yao kuhusu mkataba huo, rais aliwaahidi kuwa atayafikisha kwa wataalam ili yazingatiwe!

Japo hakuweka wazi ni maoni gani ya viongozi wa dini walimpatia, lakini inafahamika kuwa vipengele walivyotaka virekebishwe ni vile vile vilivyoainishwa na waraka wa kanisa katoliki. Tofauti tu ni kwamba maaskofu wa katoliki wameweka waraka wao hadharani wakati ule wa viongozi wa dini haukuwekwa hadharani (sijui ni kwa nini).

Kwa kuwa waraka wa viongozi wa dini upo, kuna siku utawekwa hadharani na sijui wanaosema viongozi wa dini wanaunga mkono mkataba wa bandari (kama ulivyo) watajificha wapi! Kama kuna mtu anaweza kutuwekea clip ya askofu Shoo kwenye kipengere hicho tutashukuru!!
 
Uwekezaji ndio Mkataba
Siyo kweli!! Uwekezaji hauanzii kwenye mkataba wa bandari!! Hakuna punguani wa kupinga uwekezaji!! Tunachopinga ni mkataba mbovu wa uwekezaji!! Rais Samia amemwelewa vizuri sana Dr Shoo maana msimamo wake kuhusu mkataba wa bandari alishaongea naye akiwa pamoja na viongozi wengine wa dini!! Walikataa baadhi ya vipengele vya mkataba!!
 
Nimesikiliza live hotuba ya askofu mkuu wa KKKT Askofu Shoo. Hakuna mahali amesema kanisa la KKKT linaunga mkono mkataba wa bandari kama ulivyo. Alichosema ni kwamba kanisa linaunga mkono uwekezaji....
Siti ya mbele kabisa nimekaa. Tatizo la nchi hii kiongozi wa dini anayeunga mkono mkataba mbovu wa bandari husifiwa na chawa wote wa Samia lkn kiongozi wa dini anayepinga huo mkataba mbovu hulaumiwa kwamba anachanganya dini na siasa
 
Ni kawaida ya maCCM na chawa wake kupotosha mambo ya msingi.

Wote wenye akili tunajua na tulimwelewa vizuri askofu mkuu wa KKKT, hawakubaliani na mkataba wa bandari lakini kwa hekima na busara wamelinda heshima ya Rais kwa kuwa walimpa mwaliko aje na akaja, hivyo busara sio kumnanga, kumrarua na kumbeza rais mbele za watu tena akiwepo hapo hapo.
 
Ni kweli hakuna anayepinga uwekezaji, tunapinga uwekezaji hatarishi. Na vipengere hatarishi vimeainishwa.
 
Angalau Dr. Shoo kasema mapungufu yarekebishwe, sio hao warumi wanaosema wananchi wengi wamekataa mkataba ufutwe wakati huo huo wanawapa waumini wao waraka wa ushawishi kukataa mkataba!
 
Machawa walishaanza kupiga tarumbeta humu, kilichoungwa mkono na KKKT ni uwekezaji siyo mkataba wa kimangungo wa DP world.
 
Binafsi niwashauri TEC. Wawe makini sana na Baba Padre Dk. Kitima. Alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo SAUT wakati nasoma pale 2006 - 2009. Ni mtu wa kukurupuka na kuongea kabla ya kufikiri. Hata wao Mababa Askofu wanalijua Hilo na wanajua pia ndio sababu ameshindwa kuupata Ubaba Askofu kutokana na hilo. Wawe makini asiwapotoshe!
Sasa wewe Mtoto wa Shule, Unataka tukuelewe vipi hapa? Kwamba, hili si tamko la TEC bali ni la Padre Dr Kitima siyo?

Unafahamu kuwa Dr Kitima ni Katibu mkuu wa TEC na msemaji mkuu wa taasisi hiyo na kwenye hili kazi yake ilikuwa ni kusoma tu kilichopitishwa na kukubaliwa na TEC kwa ujumla?

Au mwenzetu wewe umesikia kuwa Kanisa Katoliki limetoka na kupinga kuwa huo sio waraka wao bali ni wa mtu aitwaye Padre Dr Kitima..?

Sasa mbona unamshambulia Dr Kitima badala ya kushambulia hoja za TEC za Kwanini hawaungi mkono mkataba wa bandari?

Mkurupukaji na asiyejua asemalo ni nani kati yako na Baba Padre Dr Kitima? Bila shaka ni wewe, au siyo?
 
Nimesema! Nimesema! Na wewe una haki ya kutoa maoni yako!
Yes, ni maoni yako, nayaheshimu..

Lakini unayajenga ktk msingi wa kukosa uelewa na ufahamu ktk jambo ambalo ni FACT na sio hadithi fulani ya kufikirika...

Je, kuna ubaya mtu mwingine kukuambia haiko hivyo, bali iko hivi?
 
Binafsi niwashauri TEC. Wawe makini sana na Baba Padre Dk. Kitima. Alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo SAUT wakati nasoma pale 2006 - 2009. Ni mtu wa kukurupuka na kuongea kabla ya kufikiri. Hata wao Mababa Askofu wanalijua Hilo na wanajua pia ndio sababu ameshindwa kuupata Ubaba Askofu kutokana na hilo.
Kama humjui mtu jaribu kutulia Kijana, Mpaka uwe VC wa Chuo unafikiri hakuna Vetting inafanyika?

Kastaafu uVC kwa heshima kubwa baada ya kuipaisha SAUT kimataifa.

Baada ya KM Padre Raymond Saba kupatwa na Masaibu unafikiri TEC hawakuwa na vetting imara mpaka imteue huyo Kitima kushika wadhifa wa Juu katika Baraza?.

Weka chuki na roho mbaya Pembeni Kijana. We all know pale TEC Dr. Kitima ni Mwiba Mkali sana.. btw TEC haiwezi kumchukua mtu dhaifu kuwa KM, Refer Dr. Slaa, Raymond Saba na sasa Kitima.
 
Yes, ni maoni yako, nayaheshimu..

Lakini unayajenga ktk msingi wa kukosa uelewa na ufahamu ktk jambo ambalo ni FACT na sio hadithi fulani ya kufikirika...

Je, kuna ubaya mtu mwingine kukuambia haiko hivyo, bali iko hivi?
Hakuna ubaya. Na, je! lazima niamini na kukubali?
 
Kama humjui mtu jaribu kutulia Kijana, Mpaka uwe VC wa Chuo unafikiri hakuna Vetting inafanyika?

Kastaafu uVC kwa heshima kubwa baada ya kuipaisha SAUT kimataifa.

Baada ya KM Padre Raymond Saba kupatwa na Masaibu unafikiri TEC hawakuwa na vetting imara mpaka imteue huyo Kitima kushika wadhifa wa Juu katika Baraza?.

Weka chuki na roho mbaya Pembeni Kijana. We all know pale TEC Dr. Kitima ni Mwiba Mkali sana.. btw TEC haiwezi kumchukua mtu dhaifu kuwa KM, Refer Dr. Slaa, Raymond Saba na sasa Kitima.
Ahahahahaha! TEC is just a "Tea Party Meeting". Haina Clerical justification yoyote na ndio maana Tamko lake sio Tamko la Kanisa Katoliki. Kanisa Katoliki Tanzania na Ulimwenguni yanongozwa na Tamko la Jimbo Katoliki na Msemaji wake ni Askofu wa Jimbo Katoliki husika. TEC is just a Tea Party Meeting! Ahahahahaha!!!!
 
Naangalia maoni ya wasomaji, na maneno ya rais, ufahamu ni tatizo. Kuna dalili za kushabikia maoni ya Askofu Shoo kama ahueni kufuatia Waraka wa Katoliki kumbe ni uzi ule ule! Katoliki hawakupinga Uwekezaji.

Tatizo ni Mkataba. Askofu Shoo anasema anaunga mkono Uwekezaji. Hajasema anaunga mkono Mkataba! Rais naye anaongeza hakuna wa kutugawa! Nani kawagawa? Sema juu ya MKataba! Kuna kundi linaonekana kujawa furaha ya matumaini ya kuungwa mkonoi na KKKT! Hawajiulizi uwekezaji nani kaukataa?

Nionavyo KKKT na Katoliki wako pamoja. Katoliki wameenda mbali zaidi na kuukosoa mkataba kwa maandishi. Ninayo hisia kwamba siku chache zijazo baada ya rais kuwapisha jukwaa lao, KKT watakuja na msimamo halisi unaohusu Mkataba.
Mwambie aongee tena. Haiwezekani watu wote wakosee namna walivyomsikia
 
Back
Top Bottom