Hivi panahitajika akili gani hadi sasa kujua makòsa ya Mbowe ni ya kutengenezwa? Hata uvae miwani ya mbao kila kitu kipo wazi.. kwa sababu;
1.Hivi ukijiuliza kauli ya Samia BBC eti Mbowe alikimbia nchi unaelewa nini? Kwamba alifahamu Mbowe ni gaidi akamfungulia akaunti ili aendeleze ugaidi? Akampa na pole ya kufiwa gaidi?
2.Mimi sio mwanasheria ila hati za mashtaka zinaleta ukakasi kwamba mtu anapaswa kuitwa gaidi kwa kupanga mauaji ya mtu mmoja? Kwamba laki 6 ilitumika pia kufadhili ugaidi? Kituo kipi cha mafuta kimechomwa?
3.Mbowe alikamatwa kwa sababu ya katiba mpya huo ugaidi ni kumkomesha tu ili akae kimya.. Nadhani kuna watu wanamwambia mama mbona enzi za mwenzako walikua kimya? Vaa roho ngumu wanyooshe bila ivyo watakusumbua..
4.. Askofu hajaongea jipya ila kavaa tu ujasiri wa kusema lililo wazi.. Mbatia, Lipumba, Zito, mabalozi na wengineo wamekua na maoni haya haya..
Kiufupi kwenye hii case kivyovyote watakavyoamua maana mahakama ni zao inawashusha sana credibility ya kutenda na kusimamia haki, Hapa ndio unaona umuhmu wa katiba mpya.
Sent from my SM-A107F using
JamiiForums mobile app