Ipo wapi Tanganyika, unawajua wale 55 akina Njeru Kasaka kwanini alitishia watu kurudisha kadi ya CCM.
Mkuu 'Rufiji dam', ninao uelewa wa kutosha kabisa kuhusu hilo sakata la G55.
Ni muhimu utambue kwa nini hakuwa anataka Tanganyika irudishwe wakati huo.
Pia, inabidi utambue sababu zilizofanya muundo uwe kama ulivyokuwa wakati muungano ulipoanzishwa. Lengo halikuwa kuwepo kwa serikali tatu, bali serikali moja baada ya kuondoa hofu ya Zanzibar "kumezwa" na Tanganyika.
Na wala hapakuwepo na lengo la kuifanya Zanzibar ndiyo ionekane kuwa inaitawala Tanganyika kama inavyojionyesha waziwazi sasa hivi.
Hali hii iliyopo sasa hivi ni matokeo ya udhaifu wa viongozi waliofuata, kuhakikisha kuwa Muungano unaendelea kuimarishwa kwa usawa wa wananchi wa nchi hii.
Badala yake, CCM kwa udhaifu wao kukabili kundi dogo la wapemba, njia waliyoona ni bora ni kuwapa kama rushwa hivi kwa kukubali masharti yaliyowasilishwa kila mara kama "kero za muungano" Badala ya kuimarisha muungano, ndio wakawa wanaudhoofisha muungano
Kiujumla, watu walishakubali kuondoka kwa Tanganyika. Hata hilo kundi la G55 unalolizungumzia hapa walielewa maelezo yaliyotolewa wakati huo. Tanganyika inadaiwa kwa nguvu zote sasa hivi (nami nikiwa mmoja wa wadai hao) kwa sababu sasa ni wazi kwamba Muungano ulionuiwa tokea mwanzo, sasa hivi umegeuzwa na kuwa wa upande mmoja kufaidi matunda ya muungano kwa hasara za upande wa pili.
Binafsi sioni maana ya Muungano wa serikali tatu, ni bora kabisa kuachana na wazo la Muungano moja kwa moja.
Kwa hiyo, bado ninakukatalia kabisa kwamba kwa haya tunayoyashuhudia sasa hivi ndani ya Muungano ni matokeo ya maamuzi yaliyofanyika enzi za Nyerere. Haya ni matokeo ya kazi za viongozi hawa waliopo sasa na wengine walioachia malengo ya mwanzo na kuishia kutoa ruhwa kwa wapiga kelele nyingi wa Pemba.