Astral projection mnaona inawezekana, ila mtu kwenda mbinguni na karudi haiwezekani. Rethink

Mbona wakristo kwa Waislam mlimtolea povu Zumaridi mkamuona muongo!?
Zumaridi ni muongo, alisema Mtakatifu Peter alitaka kumuoa. Biblia takatifu imesema wazi, mbinguni hamna kuoa wala kuolewa. Nabii wa uongo hupimwa kwa neno la Mungu.

Lk 20:34-36 SUV
Yesu akawaambia, Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa; lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi; wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo
 
Kufuru inatokea wapi sialienda mbinguni unatakiwa uamini
Kukufuru ni kwenda kinyume na neno.

Lk 20:34-36 SUV​

Yesu akawaambia, Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa; lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi; wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo
 
Asante kwa andiko bora dadaake! Kwanza mimi nasema sio JF pekee, tena walau hapa kuna watu wanaweza kuhoji kwa hoja kama hivi, huko kwingine ni majanga kabisa!
With all people, sikutegemea Mwakasege na mafundisho yake ya kutoa pesa siku zote angeingia kwenye mkumbo wa akina zumaridi
Hapa ndio lile andiko la mtawatambua kwa matendo yao ndio linapotimia
 
Astral projection? Kwangu ni mental masturbation or niseme ni fantasy. Ni akili yako inakua inakucheza shere na kukupa unachotamani kukiona
 
Kabisa zumaridi alienda pia
 
Mimi sikubali kuwepo wa roho, kuwepo kwa Mungu, kuwepo kwa shetani, kuwepo kwa uchawi, astral projection na ujinga mwingine woote unaofanana na huo.

In fact, I dare say, so far in the annals of humanity, it can be shown that, any claim of a supernatural event, is either an outright lie, or something that cannot be ruled out as a poorly understood natural event.

Hapo vipi?
 
Zumaridi na Yesu wanavyeo sawa alilonena Yesu Zu anaweza tengua inatakiwa uelewe naukumbuke walati wote
 
Astral projection , ni kwà ajili ya viumbe kwà viumbe.....hao uliowataja sijui mashetani...sijui miji kama kwenda washington...vyote hivyo vimeumbwa na Mungu.

Suala la kwenda Mbinguni via Astral projection sio rahisi kama unavyodhani....ni mpaka ue umeitwa na kuchaguliwa...ndio unaweza kuvuka zile barriers + borders na tena sio zote, na wala huwezi kuonana na Muumba.

Ni Sawa na ukitaka kwenda IKULU, huwezi kwenda tu kiboyaboya bila taratibu na ukaweza kumuona Rais.


Au upo na ndege au meli, hauwezi tu kupita kwenye maji au kwenye anga za watu pasipo kuulizwa maswali.

Na ndio maana nikasema, mtu akiwa na uhai, anakua chini ya SHERIA, ...lazima afuate taratibu na kanuni. Lakini akiwa juu ya SHERIA , maana yake amekufa tayari huyo mtu...., na anaweza kumuingia Mtu anytime na kufanyisha chochote.

Sisi tuliohai , Ulinzi na Usalama wetu upo kwenye Nuru ya Mungu na kwenye Mwanga wa Neno lake.
 
Hapo sasa leo hii kisa kasema mwakasege na hutosikia wakizuia kusema mambo ya kusadikika. Tanzania kitu kile kile kinaweza kuwa kizuri au kibaya kutegemea kakisema au kukifanya nani. Tuna double standards
Hii tabia yawanadini kumuinua huyu na kumgandamiza yule nitabia mbaya na yakishetani wajirekebishe waanze kuyachukulia mambo kwa usawa na adabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…