Asusiwa chakula msibani kisa huwa hali kwenye misiba ya wengine

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,455
Reaction score
5,134
Tulikuwa kwenye msiba mmoja huku Buhigwe Kigoma, tulikuja kumsindikiza jamaa yetu aliyefiwa na dada yake, kufika msibani watu walikuwa wengi tu kama kawaida ya msiba huku watu wakiendelea kumsadia mfiwa shughuli za pale kama kuandaa chakula.

Cha kushangaza baada ya kumaliza kupka kila mtu akatoka jikoni, walipoulizwa wapishi mbona hampakui kugawa kwa waombolezaji wakajibu yeye akija kwenye misiba yetu akimaliza kupika anakaa pembeni hali sisi tunawezaje kula kwake?

Baada ya jibu hilo waa ndugu wakajitokeza kupakua na kuanza kugawa sahani ila kila aliyepewa alikataa chakula hicho hadi sisi tukaona isiwe kesi nasi pia hatukukigusa ila kwa kuwa tulikua na njaa tukatoka kwenda kula mgahawani.

Kile chakula kilibaki kama kilivyo watu wakazika tukatawanyika kulekule makaburini hatukurudi nyumbani tukaondoka zetu.
 
mm kwa apa nilipofikia ata mkikataa kula sijali aisee yaan ata tushiriki msiba wanafamilia tu na kuzika sijali kabisaaaa.
 
Mbwembwe za mwafrika,can you imagine mtu kafa kwa kukisa sh 10,000 ya vipimo ila akifa ananunuliwa ng'ombe Mmoja kwa ajili ya kuwalisha waombolezaji.

Nimekuwa nikipinga sana utaratibu wa watu kula msibani hasa wenyeji,chakula kipikwe kwa wale to wametoka mbali ila wakaazi wakale kwao.
 
ya moto hii, akili yetu, malezi na makuzi yetu yatakupinga kwa sasa ila sababu kubwa ni tunaishi miaka 20-50 ya mataifa mengine na kwakua tunaendela kuwa kama wao ipo siku itakua hivyo kwenye misiba yetu pia
 
Wamatumbi hua wanashindana kwenye vitu vya kipuuzi sana,

Kitendo cha nyie wote kutokula msibani kina maanisha kua,kumbe shughuli za misiba zinawezekana kufanyika bila mfiwa kuingia gharama za kuwalisha waombolezaji.
 
Back
Top Bottom