Asusiwa chakula msibani kisa huwa hali kwenye misiba ya wengine

Et eeh Unakua na maana gani ya kwenda msibani sasa kama unajua hutokula
Unachekesha
msibani wewe unaenda kula au kuwapa faraja wafiwa ikiwemo kumzika marehemu?

Nyie mnaong'ang'ania kula mnakera kwanini kila mtu asile kwake ndiyo aende

Chakula ilifaa wapikiwe wale wanaotoka mbali tu nyie wengine nendeni kula kwenu
 
Unachekesha
msibani wewe unaenda kula au kuwapa faraja wafiwa ikiwemo kumzika marehemu?

Nyie mnaong'ang'ania kula mnakera kwanini kila mtu asile kwake ndiyo aende

Chakula ilifaa wapikiwe wale wanaotoka mbali tu nyie wengine nendeni kula kwenu
Ndo hao sasa waliotoka mbali wamesusa chakula
 
Hii kitu wasuse ukiwa na hela huwezi kupata lakini kama Mimi kajamba nani, haloo utaangaika sana 😭
 
Mtaani kwetu, Tatizo likitokea Nyumbani wote watu wazima muonekane kwenye matatizo, dada aingie kupika, kaka waingie kuchimba kaburi, bila hivyo ni faini ya sururu hujaudhuria miwili sururu 2, ndugu zangu natafuta hela kwa nguvu nitoke niwe na hela 😥
 
Akatafute watoto yatima huko mjini, ungekuwa Dsm hakuna kususa hao washamba wanaofuatilia nani kala nani hajala mpk wana kanzidata ni uchawi tu hakuna kingine
 
Mimi ndiyo maana katika maisha yangu ninachukia sana kuishi kijijini.
Kijijini kwa maana nje ya Dar? Ila mikoani mjini hayo mambo yapo. Kanda ya ziwa huko kila mtaa wanaita nzengo kila msiba kuna daftari la mahudhurio na michango(jambo zuri) ila usipokula na wenyewe hawali kwenye msiba wako.

Nafikiri jambo la kulazimisha kula ni jambo la hovyo. Muhimu ni mahudhurio au michango ili kufarijiana.Kwanza kwa mfiwa ukimuona mtu anafakamia misosi unaona kama amefurahia msiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…