Atakayenionesha andiko linalosema mke na mume walifungishwa ndoa na kiongozi wao wa dini nampa laki 1 akale sikukuu

Atakayenionesha andiko linalosema mke na mume walifungishwa ndoa na kiongozi wao wa dini nampa laki 1 akale sikukuu

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Wakuu kwema,

Kuna laki moja hapa nataka nimpe mtu akale na wana wake. Ili uipate nahitaji uniwekee aya, mstari au sura ndani ya Quran au Biblia inayoonesha mke na mume walifungishwa ndoa na kiongozi wao wa dini au walifungishwa ndoa na Mtume, nabii au Kuhani?

Sihitaji Hadithi au andiko lisiloonyesha ninachokizungumza moja kwa moja.

Nimesema nukuu itoke kwenye Biblia au Quran si kwamba siheshimu dini zingine hapana, hivi vitabu ndivyo navifahamu.

Asante.
 
Andiko kama halipo watu wanatumia dini kuwa control watu kama kulikuwa na ulazima mungu angesema
Yesu alikuwa anapenda sana kwenda katika harusi kuna harusi moja alikwenda kama ingekuwa lazima viongozi wa dini kuwafungisha watu ndoa ndio mungu akubali basi siku ile Yesu angefungisha lakini alifanya jambo alilopenda mwenyewe walimuuliza mama ake aliwaambia atakalofanya msikilizeni basi akageuza maji kuwa pombe hapa inaonyesha jamaa kwenye mambo ya pombe yupo poa na itakuwa alikunywa tu

Muhamad alimuoa Khadija mwanamke tajiri kama Leo tunasema zali la mental kwa maana muhamad alikuwa kapuku hana hata hela unaambiwa iyo hela ya mahari katoa khadija je huyo aliefungisha ndoa yake alikuwa sheikh gani?

Ukija kuangalia hayo matukio utakuja kugundua hakuna ya haja ya mchungaji au sheikh au padri au kiongozi yoyote wa dini kuwafungisha watu ndio maana Yesu mwenyewe kaenda katika harusi hakufungisha watu ndoa sana sana kageuza maji kuwa pombe na Muhamad kama mwenyewe kiongozi hajafungishwa na sheikh hakuna ulazima wa sheikh kutaka kufungisha watu ndo nyie wakristo na waislam mumepata wapi huo utaratibu ?
 
Masare,yesu alihudhuria sherehe ya harusi,Kama ulivyonukuu,wapi Kuna andiko kwamba inatakiwa watu wafunge ndoa kwa kiongozi wa dini?
Jibu hapo
nikuulize swali.....Dini iliyokuwepo kipindi cha Yesu ni ipi
Ili uielewe Biblia ni lazima ujifunze mazingira+utamaduni wa Wayahudi kipindi cha Yesu
 
Injili ya Yohana sura ya 2 anzia mstari wa 2.
Yesu alihudhuria sherehe ya harusi kana sasa sijui hoja yako ni ipi.....hiyo harusi aliifungisha nani sasa wewe au😅😅😅
Harusi ni sherehe.

Hebu nenda kwenye kamusi ya kiswahili andika harusi.
Tena neno fasaha zaidi ni harusi.

Sherehe hata wewe na mpenzi wako mnaweza kujifanya bila hata uwepo wa sheikh au padri
 
Screenshot_20230101-185747.jpg

Wapi hapo wamefungishwa ndoa na kiongozi wao?
Au hilo neno agano hujalielewa?
 
Back
Top Bottom