Atakayeweza kuniloga nitamlipa Milioni 25

Atakayeweza kuniloga nitamlipa Milioni 25

View attachment 2615767

KUMVUJISHA DAMU MFULULIZO MWANAMKE​


WANAVYOFANYA UCHAWI HUU
~WANACHUKUA KOPO JIPYA KABISA
LA PLASTIKI AMBALO HALIJAWAHI
KUTUMIWA NA WANALIANDIKA MANENO

HAYA
---------------------------------------------------------------[Nayaficha

kwa sababu ni maneno mazito ya kufru na kuwaapia
mabwana zao wa kishetani kuwatukuza kuwasifu na
kuwaabudia kuwa wao ndyo wenye nguvu kuliko
muumba wala chochote, na mwisho wanamalizia
kuandika jina la binti anayetakiwa kuvujishwa damu na
jina la mamake au km hawamjui mamake hutumika
HAWAA mama wa binadamu wote na wakimaliza kopo
hilo wanalifukiza haltiti,nywele7 za sehemu za siri za
punda mweusi na damu ya hedhi wanachanganya
pamoja na kulifukiza kopo hilo.
Baada ya kumaliza hapo hilo kopo linatobolewa
kwenye kitako na sindanO au msumari mdogo sana kiasi

cha kupata kitobo tuu
Baada ya hapo wanalitundika kopo juu ya mti wowote
na wanalitia maji
ile maji yakidondoka ndo ndo ndo ndo ndo kupitia
kwenye kile kitobo huyu mwanamke ataanza kutokwa na
damu na damu hiyo haikati
Kazi anayoifanya mchawi hapa ni kuongeza maji kila
yakiisha huku mwanamke anaendelea kuteseka kwa
kuvuja damu.......
Dah Mkuu mpaka mwili umesisimka yani kuna dada alikuwa anakaa changanyikeni ndio alipata maradhi hayo alipitia kipindi kigumu yule dada japo alienda kuponea pemba huko
 
Mkuu nishaishi uswazi.
Sijazaliwa ushuani dear.
Nishaishi nyumba fulani pale magomeni karibu na kwa bibi nyau.Wapangaji wote mpaka kaka yangu alikua akiamin bibi mwenye nyumba ni mchawi ila mim peke yangu ndio nilikua siamini.
Nilikua sina story na mtu na maringo ya kisichana,na katika mabinti mim ndio nilikua na kaz,ilikua ya muda ubaloz fulani.
Nilikua naringa,sina time na mtu na nilikua navaa mtaa mzima naongoza na wamama na vibinti walikua hawanipend wanasema naringa ila mim peke yangu ndio nilikua naweza fua nguo nakuzianika kisha nikatoka nikaziacha.Mimi peke yangu ndio nilikua naacha madumu ya maji ya kuogea yanaishi korido na hakuna kilichowahi kunipata.
Wengine wote wakifua wanalinda nguo eti mtu atachukua uzi awaloge.Maji nilikua naambiwa ninavyoyaacha pale eti nitawekewa kitu nikioga nipate kitu.Nilikua naambiwa nisigaqe nguo au viatu eti watavitumia kuniloga ila nilikua nikivichoka nagawa.Na hapo nilikua mdogo elimu ni form six tu na sina hata exposure niliyonayo leo ila nilikua tu smart kutoamin upuuzi.
Nakuambia hv,Kila Mtu na asili yake,wewe waweza sema hvyo kumbe vizazi vyako vilivyopita vishafanya mambo usidhurike
Kingine km unaamini dini zeu hizi mbili huwezi sema hakuna uchawi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Aah Acha kutusumbua wachawi bwana,mtu mwenye kujenga hekalu na kuweza kitulipa mln 25 wachawi hawezi kuvaa gauni la kama Hilo....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hayo ni matumizi mabaya ya mikoba
Mfyuuuuuu [emoji16][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
wewe maneno mengi nunua hio dawa inaitwa makata....nawa au oga uone utakavyoiloga utatafuta tiba mwenyewe....kama uchawi ni sayansi hio ndio proof yake...
Siwezi kuogea mavitu sijui ni manini yaje yaharibu my expensive skin bure🤣.
Kama unaniloga niloge ila matakataka siogei
 
Hello Africans.

Hakuna binadamu ninaowadharau kama wanaoamini mauchawi na mauganga.

Huwa nawaona ni watu wenye kasoro kubwa kichwani na wameoza kiasi kwamba hata uwaambie nini huwezi kuwabadili imani.

Hizi imani pumbavu zinaonesha vile Africans tuko na IQ ndogo.Na ndio maana pamoja na utajiri uliopo ktk hili bara tunateseka na shida karne kwa karne huku wenzetu wasioamini haya maujinga wakituacha mbali kwa maendeleo. (Najua kuna wazungu wachache vichaa pia wanaamin ushirikina).

Ukweli hizi imani zinanikera sana maana mbali ya kuchelewesha maendeleo ya hili bara pia ni hatari.Tushaua sana wenzetu wasio na hatia sbb ya hizi imani pumbavu.Albino,Vipara,wazee with red ayes na wengine wengi.Upumbavu mtupu.

Mimi binafsi nilishahama sehemu kwa kusingiziwa eti mimi ni freemason.Nilifanya kosa nikaporomosha hekalu wanakoishi wajinga.Mjengo wetu uko tofaut by far na nyumba zingine zote.

Wale wapuuzi walishindwa kujua kuwa kufanikiwa hakuna uchawi bali janja janja na timing kwenye fursa,basi yenyewe yakajiongoza eti hapa ni masonic na makafara tu.

Mwanzoni niliwapuuza ila badae kuna kitu ilitokea nikaona hawa wapuuzi kuna siku wanaweza wakajiunga wakanichoma mle ndani wakiamin mie natoa damu za watu kafara.Ikabidi niondoke.

Yupo mfanyakazi wangu alinichana Live kuwa "boss najua huwez kutoa siri zako ila siwez amini umefika hapa ulipofika bila ndumba kuhusika"

Mimi siamini kama kuna mtu yeyote anayeweza fanya kitu digits zangu bank zikaongezeka.Siku zote ninaamini katika kutumia akili ktk kutafuta.

Pia siamini kama kuna mjinga yeyote anayeweza kuniloga kitu kibaya kikanipata sbb havifanyi kazi.Mnadanganywa tu.

UCHAWI NA UGANGA NI UONGO havipo na havifanyi kazi.
Mpo wengi humu mnaoamini hayo matakataka sasa nawapeni ofa ya 25M kwa atakayeweza kuniloga.

Nifanyeni chochote kibaya na mhakikishe hamnisamehi mpaka nije hapa niandike uzi wa kuomba msamaha na kukiri kuwa kweli uchawi upo nimelogwa na pia nilipe hiyo 25M kwa mchawi wangu.

Mkitaka niwatukane babu na bibi zenu wanaoogopwa kwa uchawi ili hasira ziwapande mniloge vizuri semeni.Nitawavurumishia mitusi hao babu/bibi zenu hamjapata kuona.Nitawatukana na kuwakashifu ma hawatanifanya chochote wajinga hao😂

Haya kazi kwenu.

NILOGENI

UPDATE:Mnaotaka jina ili mniloge siwezi kuwapa sbb ua Privacy ila nawawekeeni picha yangu muitumie kuniloga.Kateni mikono,vidole,nifanyeni niwe na miguu 4 kama.ng'ombe vyovyote.
nikimalza kukuloga pesa nazikuta sehemu gan umeweka ???
ila mimi nakuongezea tu inayoonyesha ulishalogwa tayar
 
Nakuambia hv,Kila Mtu na asili yake,wewe waweza sema hvyo kumbe vizazi vyako vilivyopita vishafanya mambo usidhurike
Kingine km unaamini dini zeu hizi mbili huwezi sema hakuna uchawi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hamna cha asili wala nini.
Na nilivyokua nanata uchawi.ungekuwepo kweli wasingeniacha salama
 
Back
Top Bottom