Atakayeweza kuniloga nitamlipa Milioni 25

Atakayeweza kuniloga nitamlipa Milioni 25

Kama kweli upo serious na Milioni 25 za kulogwa,,, basi fanya hivi??

Milioni 5 fanya tangazo likiwa na DETAILS zinazohitajika na WACHAWI,,, weka bango gazeteni, nunua ukurasa pale MWANASPOTI au MWANANCHI... au mtandaoni kama FACEBOOK, Google Adsense au zingine.

Halafu hiyo Milioni 20 inatosha kabisa ndo iwe zawadi.. Na hii unaiweka kwenye Escrow Account mapema kabisa, maana unaweza ukafanywa chizi halafu hela isipatikane tena..

Zaidi ya hapo tuendelee kunywa supu Nyama zipo chini..
Escrow account ndio ikoje hiyo?.
 
Unakuta mtu na elimu yake anaenda kwa mganga aliyeishia darasa la 7 ili apewe dawa ya utajiri,wakati huyo mganga mwenyewe ni choka mbaya,anaishia tu Kukuagiza Jogoo kisha analifanya supu na kula na wanae huku wewe ukisubiri utajiri uje kimiujiza!

😀😀
Mkuu, sheria za ulozi ni hatari sana...
Hupewa amri na mizimu yao,, hakuna kujenga wa kununua gari..


Na wengine mizimu inawakatalia hata kuoga Zaidi ya mwaka mzima.

Siyo kwamba hawapendi bata ila ndo hivyo.. Sheria ni kali sana.. Ukikaidi mizimu inakuua
 
Sasa wewe ndo tunaweza kufanya biashara.
Nasubiri kitu mkuu.
Waambie kabisa nini utanifanya.
Ila usiniue ili nije kutoa ushuhuda😂.
Na ukiweza kuniloga itabidi tukae mezani tuone namna gani tutumie ndumba kupiga hela na ikibidi tutumie uchawi wetu kunufaisha Taifa liwe first world country.
Na usafiri wetu wa ungo nitahakikisha unachuana na KLM,Ethiopian airline na Emirates kuongeza pato la taifa🤣
holy holm Half american Achraf hakim Bufa
wewe maneno mengi nunua hio dawa inaitwa makata....nawa au oga uone utakavyoiloga utatafuta tiba mwenyewe....kama uchawi ni sayansi hio ndio proof yake...
 
Sad indeed. Mwaka jana kuna survey ilisema TZ inaongoza kwa imani za kishirikina Africa meaning watu wanaoamini ushirikina upo ila sababu wabongo wengi wana comprehension disorder hawawezi kung'amua mambo wengi walielewa "wabongo wengi ni washirikina." These are two different meanings. Watu ambao hawawezi kung'amua sentence rahisi tu hivi huwezi tegemea wawe rational. Wao wanaamini tu kama nyumbu kila wanachoambiwa.
Tatizo ndo liko hapo.
Hatutaki kuchosha akili tumeamua kuamin tu.
 
Huyu mleta mada ajue tu kuwa kitanda usichokilalia huwezi kujua kunguni wake, na asifiaye mvua imemnyea. Huyu anajisemesha tu hajawahi kukutwa na huo mkasa lakini waliopitia huo mtihani hapa huwezi kuwaambia kitu. Quran na Biblia vyote vinakubaliana na uwepo wa uchawi. Fuatilia kisa Cha Musa and et al utapata majibu labda km wewe una abudu miungu.

✓Ila km wewe mleta mada ndiyo hiyo picha Yako nadriki kusema wewe ni mwanga na mchawi uliekubuhu. Mimi nakwambia ukweli. Hapo kwenye mwili wako tu una vitu vingi vya kishirikina ingawa wewe hujui au huoni km ni ushirikina. Siku ukipigwa kipapai usiste kutupa mrejesho.
nonsense
 
Mchawi akiwa Mwanaume ni afadhali aweza kuwa na huruma ikafika mahala akamfungua mtu Au kugairi kumuua au kumdhuru lakini Mchawi mwanamke hana huruma ni mazima [emoji108]
Hata jambazi Au mwizi akiwa mwanamke huwa ni katili mara millions kuliko jambazi /mwizi Mwanaume
Kwanini wanawake waovu ni makatili mno ?
 
Muhimu kumbukeni hata wachawi huloga mtu potential siyo Kila mtu. Mfano, nani amewahi kuskia kichaa, mlemavu au mtu wa utindio wa ubongov(tahira) nk wamelogwa. Ebu tuwape heshima wachai wote popote walipo Duniani kwani ni watu makini sana. Hufanya upembuzi yakinifu kabla ya kufikia maamuzi, huwa hawakurupuki, wanachukua kilicho Bora. Sawa na Simba mnyama mwitu huwa hali mizogo yeye mizoga huachia fisi.

Kwa Hiyo hakuna sababu ya kujitapa kuwa eti mtu huwezi kulogeka sema tu huna sifa. It means you don't meet their needs.
Sio kweli mkuu
 
Kwa wanaodai majina ya muhusika ningeomba kujua ni ipi mantiki yao ?, yaani hayo majina ya muhusika yatawasaidia vipi, kazi ya hayo majina ni ipi hasa ?

Kama ni kwa lengo la kumtofautisha muhusika anaetaka kulogwa na watu wengine wote duniani ili ulozi umfikie yeye kama yeye naomba kujua.
Nadhani lengo ni kutaka missile watakayoirusha isiende kuua wasio na hatia.
Inajua kuangamiza ila haijui kutofautisha🤣
 
Hamna anayependa .
Mi nimeuliwa baba zangu ukoo wote, wa mwisho nilikua naye
Mzima tunaagana
Asubuhi namuona huyu hapa anahema.
kumbe kashapigwa huko
mkewe ndo shughuli zake.
ajabu
Wiki 2 nimeondoka huku nyuma nae kafa.
Mkewe kakimbilia kwenye ardhi kubwa.
Kuna makaburi saba pale.
Kilichompata na yeye na wanae.
Kakimbilia kanisani na kukiri uchawi wote aliofanya
Kuua baba zangu.
Ambao wote ni wakwe zake.
Mumewe kammaliza mwisho.
Alafu mtu aseme hamna uchawi
Aseeh...pole Sana kaka
Jeep rubicon nashauri nenda kaseme hayo maneno kijijini kwenu humu jf honestly hakuna mwenye ubaya na wewe

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Aah Acha kutusumbua wachawi bwana,mtu mwenye kujenga hekalu na kuweza kitulipa mln 25 wachawi hawezi kuvaa gauni la kama Hilo....🤣🤣🤣🤣🤣
Hayo ni matumizi mabaya ya mikoba
I just like you.😂
 
View attachment 2615767

KUMVUJISHA DAMU MFULULIZO MWANAMKE​


WANAVYOFANYA UCHAWI HUU
~WANACHUKUA KOPO JIPYA KABISA
LA PLASTIKI AMBALO HALIJAWAHI
KUTUMIWA NA WANALIANDIKA MANENO

HAYA
---------------------------------------------------------------[Nayaficha

kwa sababu ni maneno mazito ya kufru na kuwaapia
mabwana zao wa kishetani kuwatukuza kuwasifu na
kuwaabudia kuwa wao ndyo wenye nguvu kuliko
muumba wala chochote, na mwisho wanamalizia
kuandika jina la binti anayetakiwa kuvujishwa damu na
jina la mamake au km hawamjui mamake hutumika
HAWAA mama wa binadamu wote na wakimaliza kopo
hilo wanalifukiza haltiti,nywele7 za sehemu za siri za
punda mweusi na damu ya hedhi wanachanganya
pamoja na kulifukiza kopo hilo.
Baada ya kumaliza hapo hilo kopo linatobolewa
kwenye kitako na sindanO au msumari mdogo sana kiasi

cha kupata kitobo tuu
Baada ya hapo wanalitundika kopo juu ya mti wowote
na wanalitia maji
ile maji yakidondoka ndo ndo ndo ndo ndo kupitia
kwenye kile kitobo huyu mwanamke ataanza kutokwa na
damu na damu hiyo haikati
Kazi anayoifanya mchawi hapa ni kuongeza maji kila
yakiisha huku mwanamke anaendelea kuteseka kwa
kuvuja damu.......
Menorrhagia sio uchawi wala ushirikina au kulogwa

Upande wa hedhi Haya mambo yapo mengi tu kwa wadada ila sio uchawi wala kulogwa. Ni mambo yanachangiwa na vitu kama stress, hormonr imbalance, mambo ya thyroid hormone nk.
 
Back
Top Bottom