Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 12,599
- 26,263
Kumbe mkuu ningejua nisingefanya marudio.
Ngojea niupitie uzi wako.
Kuna wakati nilikua Handeni huko ndani ndani.
Nikatokea kupendana na bibi fulani,akatukribisha kwake.Wenzangu wakagoma eti wenyeji wanasema tukilala.pale.kesho hatuamki.
Mimi nikalala.Bibi akanipikia ubwabwa mzuri na samaki.Tukapiga sana story.Bibi was so cool ila alikua anaogopwa na ametengwa eti ni mchawi na anahusishwa na vifo kadhaa pale kijijini.
Tukalala mimi na bibi na pakakucha salama
Wale wenzangu asubuhi wanalalamika eti huko walikolala hawakulala eti mauzauza Handeni hapafai.
Nikashangaa mim nilolala na mchawi mbona sijaona mauza uza
Wengi wenye imani za kishirikina sio timamu. Their whole thought process is illogical. Wanaamini tu kama nyumbu. Story zote za ushirikina ni hearsay na kuaminishana upuuzi tu. Huyo bibi wanaweza hata kumdhuru maskini kwa imani zao za kipuuuzi.
Haidhuru wewe kuanzisha uzi mwingine labda utapata majibu tofauti ila I can assure you utapewa excuses lukuki badala ya kuokoa nguvu na muda kwa kukuroga tu mwenyewe uje kutoa ushuhuda.