Upotezaji wa damu mfululizo kama bomba la maji hauhitaji hata nusu ya siku 7 ili ufe.
Menorrhagia kwa yenyewe sio fatal, ni shida inatatulika na na kutibika vizuri tuu. Lakini mdada anawezakufa kwa sinario kama hii, mdada akishapata shida hiyo ya hedhi mfululizo bila kikomo ataamini moja kwa moja kwamba kalogwa au kafanyiwa uchawi na mambo ya kishirikina, matokeo yake badala ya kwenda mahali husika (kwenye kituo cha afya) atakimbilia kwa waganga wa kienyeji, huko hatapata utatuzi wa shida yake ya uvujaji wa damu, matokeo yake ataendelea kuvuja damu mpaka anakufa, au kupata shida zingine kama upungufu wa damu nk.
Labda akutane na mganga mjanja mjanja au mganga tapeli, ajue shida yake ni nini kisha ampatie dawa ya kukata izo damu zikatike na kupona kabisa.
Dawa za kustop uvujaji damu ya hedhi zipo na zinauzwa wazi kabisa, wala hazihitaji uchawi, uganga wa kienyeji au ushirikina ili kuzijua au kuzipata.