ATCL, Reli ya Kati, TAZARA na SGR tuwape wanaoweza kuendesha kwa ufanisi mapema kabla ya kuumizwa

ATCL, Reli ya Kati, TAZARA na SGR tuwape wanaoweza kuendesha kwa ufanisi mapema kabla ya kuumizwa

Naunga mkono Hoja.. serikali isifanye biashara ikusanye kodi na gawio
 
Tulianza kujitegemea kuanzia wakati wa Nyerere mpaka leo tunashindwa. Kila tunachokianzisha au tulichokikuta tukikifanya kwa "kujitegemea" kinashindwa.

Misingi na dhana ya kujitegemea iliwekwa mibovu.

Tumuombe Mwenyezi Mungu, mama Samia aibomowe yote aijenge upya (Rebuild).
Kama ushatambua misingi iliyowekwa ni mibovu, kwanini usiishauri serikali iboreshe mfumo.

Keki ya taifa ni kubwa, badala ya kuwakatia keki yetu wageni ni bora tuile wenyewe.

Tatizo kubwa naloona hapa sio CCM ila ni wanaoongoza hicho chama.

Kama ATCL ilikufa na ikaja ikafufuliwa na mtanzania sasa kunahaja gani ya kumpa mzungu.

Yani unaanzisha biashara afu wewe mwenyewe hutaki kuifanya unawaachia wengine wakufanyie alafu hapo hapo unataka ufanikiwe kuliko wao.

Tujitafakari jamani
 
Kuwawachia Watanzania waendeshe nashirika hayo makubwa ni ujinga uliokithiri.

Hivi hatuelewi mashirika hayo yaliuliwa na kina nani mpaka kuwa chali?

Tumeona mwendokasi imetushinda kuendesha na sio kwa mara ya kwanza.

ATC tuliiuwa na sasa ipo njiani kuuliwa tena.

Reli ya kati na TAZARA hatujajifunza tu? Sasa tunarudia makosa yaleyale, tunawakabidhi SGR wauwaji.

Hivi lini tutapata akili?
Yaani tuhangaike kulipa Kodi, miundo mbinu imekamilika, tumenunua treni halafu wajanja wajanja waibuke waanze kukusanya hela tuu. Yaani kutengeneza application ya ticket ambapo Kila msafiri ataomba ticket mwenyewe bila kujirundika maofisini mnashindwa?
 
Mama samahani ila hufai kuwa kiongozi. Maana kiongozi bora ni yule anaelinda maslahi ya umma.

What if hayo mashirika yakiwa yanamilikiwa na Umma wa Watanzania si mapato yanaongezeka na ajira zinaongezea?

Kunaulazima gani wa kuchukua makaburu yaje kuendesha shughuli zetu. Yani ndege tununue kwa kodi zetu, SRG tutengeneze kwa kodi zetu, afu tumwachie mtu mwingine atuendeshee!!

Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Hapo msomi hatuna.
Maslaji ya umma ni kuuwa mali za umma au kuzifanya ziendeshwe zichangie pato la taifa?

Nambie kipi cha umma amacho hakijabifsishwa kuanzia wakati wa Nyerere mpaka leo hii ambacho kimechangia pato la Taifa?
 
Apewe kaka Yako Rosta
Ndio akili yake huyu bi kidude,
Kaskia majina ya kina mudy na azam na wengine wasilamu wenzie baas kabadili gia anasema wapewe.
Sasa hawa si wa hapahapa tu na mwanzo kasema watz wasikabidhiwe hayo mashirika.
 
Maslaji ya umma ni kuuwa mali za umma au kuzifanya ziendeshwe zichangie pato la taifa?

Nambie kipi cha umma amacho hakijabifsishwa kuanzia wakati wa Nyerere mpaka leo hii ambacho kimechangia pato la Taifa?
Kwahiyo kwako wewe kubinafsisha ni sahihi?
 
Back
Top Bottom