Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,047
- 63,206
Umebaki muda mfupi kabla ya mahalama haijatoa hukumu kwa ndugu Lissu. Ndugu Lissu anashitakiwa kwa makosa ya uhaini. Si lengo langu kuingilia mahakama na sitofanya hivyo lakini najaribu kuiangalia possibility ya hukumu inayoweza kutokea katika worst case scenario na athari zake kwa Legacy ya kisiasa ya rais Samia. Na hivi ndivyo nionavyo
1. Kama Lissu akihukumiwa kunyongwa atapata huruma kubwa kwa umma na chuki itakuwa kubwa kwa Samia.
Pengine rais Samia kama mwanasiasa anapata taarifa ya.kinachoendelea mtaani, kiufupi wananchi walio wengi wanaamini Lissu anaonewa, anadhabitiwa ili asiichachafye serikali yake kisiasa na kwamba amepewa kesi ya mchongo ili kumtoa katika reli ya kisiasa kwa ajili ya ahueni ya kisiasa ya Samia. Iwapo atahukumiwa kunyongwa umma utamuangalia Samia kwa jicho baya sana, na haijalishi kama Samia atatia saini ya hukumu hiyo au la, itadamage legacy ya rais Samia kwa kiwango kikubwano.
2. Kama Lissu akihukumiwa kunyongwa itaharibu uwezekano wa maridhiano chini ya uongozi wa rais Samia au serikali yake.
Kiukweli Taifa lina madonda mengi, linahitaji kupona. Huwezi kuliponya Taifa kama wale ambao wanapaswa kukaa na kuzungumza na kupata muafaka wana kongwa la kitanzi shingoni mwao. Hata wale watakaobaki, watakuwa TRAUMATISED kwa kiwango cha kutisha kuweza kukaa mezani kutafuta hayo maridhiano. Kiufupi kama Lissu akihukumiwa kunyongwa, itaondoa legitimacy kwa rais Samia kuongoza mjadala mpana wa kitaifa wa maridhiano. Na hili litaathiri kwa kiwango kikubwa mno Legacy yake.
3. Lissu akihukumiwa kunyongwa kelele nyingi sana kutoka pande zote za dunia zitamuandama rais Samia.
Kwa sasa Lissi ni International figure, pengine ni mtu wa tatu ktk historia ya nchi hii kwa umaarufu nje ya nchi, wa kwanza akiwa ni.mwalimu Nyerere, wa pili ni Salim Ahmed Salim na wa Tatu ni Tundu Lissu. Kelele za kulaani uwezekano wa kunyongwa zitakuwa nyingi kama alizopambana nazo Sani Abacha wa Nigeria kwenye ishu ya mwanafasihi Ken Saro Wiwa. Image ya rais Samia itaharibika sana. Kila atakapoenda nje ya nchi ataambiwa free Lissu.
4. Kama Lissu atahukumiwa kunyongwa itamnyang'anya rais Samia fursa ya legacy ya kuandika katiba mpya
Wananchi wanahamu sana ya katiba mpya, lakini legitimacy ya anayoileta ni kigezo kimojawapo cha kuwafanya wananchi washiriki kikamilifu. Ni dhahiri, Katiba mpya ni kete ya turufu ya angalau kulinda legacy ya mama Samia kama akiukunjua moyo wake kuisapoti. Kwa sasa baada ya tukio la Nchimbi wananchi wameanza kupata mashaka kama kweli anamaanisha, maana wananchi wanaamini yaliyomkuta Nchimbi sababu mojawapo ni kauli yake ya kupigia chapuo katiba mpya kwa msisitozo mkubwa. Bila kujali ukweli au la kuhusu hili, hivyo ndo wananchi wengi wanaamini. Sasa kama Lissu atahukumiwa kunyongwa, itaongeza dhana ya wananchi kuwa rais Samia jana upako wa kuleta katiba hii. Kama nilivyoeleza hapo juu, wananchi wengi hawaamini kama kesi hii ni genuine wanaiona ni ya mchongo.
MWISHO.
Legacy ya Rais Samia imepata dhoruba kali sana kwa mambo mengi hasa hali ya usalama wa wananchi katika mambo ya utekaji na watu kupotea, faulo katika kupata nafasi ya kugombea kupitia CCM, uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2024 wenye makandokando, uchaguzi mkuu wa mawenge, October 29, Ishu ya Nchimbi Sasa kama ikitokea Lissu naye akahukumiwa kunyongwa kwa kesi ambayo umma unaiona ni ya mchongo, kwa kweli haitoacha Legacy nzuri ya kisiasa kwa rais Samia hata kidogo.