Athlete Crown sio gari la kubishana nalo ukiwa barabarani acha liende

Brevis anapigwa upepo na Fuga au Crown mkuu!.. Ila kibonde wake Progress!..
Kwa macho na mikono yangu nilizidiwa na Fugga lakini nikasikia hata Crown ni mbabe wa Brevis, ila hivyo vingine nitavisoma kwenye side mirrors tu!..
Boss amini usiamini hizi gari ndogo (toyota) karibia zote hakuna wa kufanya batle na Brevis ikashinda labda ujuzi wa dereva lakini sio acceleration yake, ile gari ione vilevile lakini moto wake ni balaa.

Wenyewe tunaiita King of the road, unafikiri tumekurupuka na jina bila ushahidi?
 
Kaka gari kama crown unapishana na hata semitrailer kwa mwendo huo haliyumbi.
Mimi ni dereva nimeendesha kuanzia trucks na magari ya mashindano(safari rally)najua nilisemalo!Huwezi kukimbia na gari ukawa katika lane yako bila kukaa katikati na mwendo huo(km140/saa) na hesabu za haraka iwe kusimama au kupishana ni kuanzia mita 500 mbele.
Kuna kipindi nilikuwa natumia range rover sport ya boss wangu ina balance nzuri sana hata kwenye kona.Huwezi kulinganisha na hicho kigari.
Kwa hiyo nina uzoefu na magari tena kwa safari ndefu.
 
Msamaha kama nachafua uzi ila tusaidiane kupata mteja wa Nissan Cube 2007, 1490cc, mileage 100k, ndio imetoka port, imesajiliwa, yauzwa kwa 9.5m, 5% itatolewa, wasiliana na huyu jamaa 0753680847
 
Mkuu Brevis tunaiita Presidential Car na nilishawahi fanya ligi na Nissan Fuga dom-arusha. Huwa napenda safiri asubuhi sana hakuna trafiki, nikakutana nayo, iliniacha ikabidi nilipofika nimsimulie jamaa yangu akaniambia hata Crown nayo ni mbabe wetu!.
Lakini hivi vingine vi saloon Car havijawahi nipita kizembe!. Nasikia na Subaru Legacy nayo ni mziki mwingine, sijawahi kutana nayo njiani so siwezi ielezea kama kweli!.
 
Eminentia anaongelea technically issue za hizi gari na wengine mnaongelea experience ya uendeshaji.

Sio kila speed itayo onekana kwenye dashboard kufikiwa, kuna vitu kama hp ya gari ni moja ya vitu vinavyo sababisha kuweza kufikiwa au kutofikiwa.
Sasa mkuu wewe na Eminentia mnataka kusema kuwa waloweka speed kwa mfano 300 kwa vw golf gti ni waongo? labda mseme tu kuwa ili kufuta sahani au kukamua full kunategemea na hali ya gari, umahiri na ujasiri wa dreva na ubora wa barabara but ni siamini kabsaaa kusema eti top speed za magari huwa zimewekwa tu na haiwezekani kuzifikia. Kwa sababu ikiwa hivyo ndo kusema ati waunda magari ni waongo na wamecalibrate poorly hizo dash board.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] we nawe unachekesha!! Carina Ti ni cc 1480 (isomeke 1500) ulitaka ulale sambamba na Crown Athlete ya cc 2500 hadi 3500 kulingana na model na mwaka iliongenezwa! Utapasua engine bro!
 
Waendesha vi baby walker naona comment zao ni kutaja kaburi,sasa walio weka odometer za speed hizo hawajui kuwa kuna kifo au ndo zile za "wivu wa kike" [emoji12]
Wamezoea kuendesha baby walker (ist, spacio, vitz na starlet) mijini na foleni, akikimbia sana ni 60 kph. Kwa hio hizi stori za 170 kph ni ngeni kwao. Wahurumie tu
 
Mi najua tu kuendesha siyajui sana magari ila ni ile iliyofanana umbo kama Niss

Mi najua tu kuendesha suyajui sana magari, kakini ni ile inayofanana na Nissan Murano kwa mbali
Ni VW Touareg hio. Ina 220 kph ile.
 
Nilikua namiliki vw touran cc 1900 speedometer inasoma 260 na ilikua inamaliza kisahani nikiamua.Japo sio mtaalam wa physics lakini naamini kuna sababu nyingi tu za kupinga theory

Gari za wajerumani zina tabia ya kuchanganya haraka sana may be kwa sababu hawatumii automatic gearbox za kawaida (vw group ambao wanamiliki Audi,Porsche, seat,Skoda gari zao zote wanatumi DSG transmission ). BMW,Benz pia in DSG au Zf transmission ambazo zipo mpaka za via 10.Toyota nyingi auto gia 5 mpaka 6 labda kama ni CVT.
 

Hahaha hupendi dharau Mkuu!!
 
Kuna jamaa alikua na crown deluxe alinipita milima ya udzungwa natoka Moro to Iringa, Niko kibati 130 na jamaa sikumuona tenaaaa... Yani ni shida hizi Gari..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…