Athlete Crown sio gari la kubishana nalo ukiwa barabarani acha liende

Ukiwa unasafiri utajifunza mengi saana njiani kwakifupi kuna magari yako vizuri mno barabarani,haya magari yetu TOYOTA ni ya kawaida mno kwa European cars
 
Speed kasi hutegemea ukubwa wa engine na piston

Gari hata iwe na speedometer inayosoma 260 ila ni 2500 cc v6 haiwezi ifikia 3600cc v6 yenye 200
Nipe maelezo kidogo mkuu, nijuavyo mimi speed ya 100km/h ni 100km/h kote koye haijalishi.. Sasa hapo iweje 260 iwe cha mtoto kwa 200!?
 
Asante kwa darasa aisee haya mambo nilikuwa sijui kabisa
 
Gari yoyote yenye injini ya GX100 ogopa sana.likifungua hata uwe na range rover v8 na uko spidi 200 itakupita kama umesimama na huku yenyewe imeandikwa spidi 180
Ndio unavyojidanganya hivyo?Unajua horse power ya range rover v8 ukafananisha Gx 100?Sema ulikuta hilo range linatembea km 60/hour na wewe upo 80km/hour na gari yako Gx 100.
 
Mwaka jana siku moja niko na rafiki zangu tunatokea Moshi kurudi Jijini tukawa tunaweka mafuta pale Total Korogwe zikaja gari 3 kwa muda ule ule kuweka mafuta..

Moja: ilikua ni Mercedes-Benz W203 Kompressor ya zamani kidogo hii ilikua inaendeshwa na mzee flani ivi ila anaoneka bado kijana alikua na wanawake wa 3 kwenye gari..

Mbili: ilikua ni BMW 3 series hizi 6th generation hii ilikua ni gari ya ubalozi (plate ya kijani) walikua jamaa wawili weusi wamekula suti matata.. na gari ni mpyaa

Tatu ilikua Toyota Crown Athlete inaendeshwa na muhindi nayo ilikua mpya (yenye hali nzuri)

Hawa wote tuliwaona maana pale kituo cha mafuta ni kawaida mtu ashuke kwenye gari kwa sababu mbalimbali ikiwa ni kwenda kujisaidia au kununua vitu vidovidogo vya kutumia njiani..

Sasa tulivyoona vile tukajua tu hapa lazima kutakuwa na ligi moja matata tukasema ngoja tufatane nao tushuhudie..

kitu ambacho ambacho kilitokea baada ya muda kama nusu saa yule jamaa wa BMW alipotea bila kuonekana tena (disappeared without a trace) nadhani pia jamaa walikua hawajali tochi wala traffic police.. wakabaki Benzi na Crown.. jamaa wa Crown alikua anatii sana sheria za barabarini kwenye 50 anakubali jamaa wa Benz anampita ila tulivokuja kuingia porini Benz alikatwa tena kwenye kilima..

Kiukweli siku ile tulifuraia sana ile ligi ya wale jamaa.. Unaweza ukawa dereva wa hapa mjini ila ukiwa High-way unajifunza mambo mengi.. wale wa desemba nadhani wanaelewa nachosema..
 
Wengi mmeongea kwa hisia tu!Kiukweli kwa barabara zetu huwezi kukimbia zaidi ya kasi ya km 140/saa.Na hapo gari yako inatakiwa iwe katikati ya barabara na huo mwendo hauzidi umbali wa km 15.
Na ni barabara zifuatazokutoka DSM.

Barabara ya Morogoro
Ni kuanzia Chalinze kuitafuta bwawani,hapa unaweza kuona mbele kwa umbali wa km 15 na zaidi pamenyooka sana.

Barabara ya Morogoro -Iringa
Hapa ni kuanzia Sangasanga(njia panda ya kwenda Mzumbe university) kuitafuta kijiji cha doma(kabla hujaingia hifadhi ya mikumi)
na sehemu nyingine ni kuanzia Ruaha mbuyuni(Al Jazira hotel) kuelekea kijiji kimoja kinaitwa mahenge.
Iringa -Mbeya(TANZAM road)
Hapa ni igurusi

Morogoro -Dodoma
Hapa ni kuanzia Kibaigwa kuelekea Dodoma.

Dodoma - Singida
Hapa ni kuanzia manyoni,na ndio sehemu ya pekee kulikuwa na kibao kinachorohusu km100/saa miaka ya nyuma.

Dodoma - Iringa
Hapa unaanzia sehemu moja inaitwa chipogola hadi makatapora (Mpwapwa)

Babati- Arusha
Hapa ni kuanzia Babati hadi Magugu.
Same - moshi(Kilimanjaro)
Hapa ni same na pana upepo mkali sana.
 
Naongezea,hapo Dar-Moro ni eneo linaitwa Mwidu,pia usisahau Dodoma-Kondoa kuna sehemu nyingi unaweza kwenda mpaka 180 km/h..
 
Inamaana wewe unajua zaidi ya wajerumani [Bavarian]
Inamaana wewe unajua zaidi ya wajerumani [Bavarian]
hapana mkuu ...kwan ww utaacha labda boxer yenye hp 12 ila speedmeter inasoma 140 ukafate piki piki ya kichina yenye hp 9 kisa dash yake inasoma 180 ndo ujidanganye utaipita boxer wakat boxer na hp zake hizo 140 haifiki ikiwa stock labda ukorokochoe ndo yenye hp 9 itafikaje sasa
 
Mkuu nilikuwa sijui lolote kuhusu hizi crown asante kwa kunipa elimu....vipi kuhusu crown majesta? nalo ni sports car?
hapana lenyewe kidogo liko unique Crown Majesta has been a
separate model with distinct
styling differences and a
longer platform than the
Crown,
 
Dah....ajabu sana...3200rpm
kisha 140km/h....kuna tatizo
mahali....@rohombaya

ww kibovu unaona ni nini yani speed ndogo sana ukimatch ya rpm au spid kubwa sana
 
Haka kagari ni hatari sana mkuu,ni cha muingereza baadae kalinunukiwa na bmw
 
Sina budi kukaa kimya kwenye uzi wowote wa mwana Jf unao husu Magari ama Degree...[emoji12] [emoji12] [emoji12]
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
hahaha
 
Bahati nzuri nimewahi kutembea na Crown na pia magari ya mjerumani kama Benz na BMW.

Kiukweli nilivyosoma komenti yako nimecheka sana kuona unavyojaribu kufananisha BMW na Crown. This is a total joke.

Yani kwa komenti yako hii, kama ni Wanyama, ni sawa na kumfananisha Cheetah na Pundamilia.

Hivi BMW ata iwe 3 series ya zamani 1700 cc ikifunguka Toyota Crown inabidi ukae pembeni.....hapa sijazungumzia BMW "M" Power.

Kama hujui kuhusu magari ni vyema uende google ukajifunze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…