Attitude ya Harmonize yafikisha views Million 3 ndani ya masaa 27

Attitude ya Harmonize yafikisha views Million 3 ndani ya masaa 27

Naona video imeganda nimeitizama asubuhi masaa matatu yaliyopita bado views 3.2m,ukiona hivyo wanaivalidate kwa hiyo kuna mawili views ziongezeke au zipungue.
 
Safi sana kijana. Pamoja na mambo yote ya Wapinzani wako ila bado anawahenyesha. Nimechungulia muda huu bado ni No 1 trending na viewers 3.2m. WCB na Rayvanny watazimia. Maana pia katika trending nyimbo za Harmonize ndiyo ziko kwa wingi. Jeshi a.k.a Tembo anawakanyaga kwelikweli.
 
Naona video imeganda nimeitizama asubuhi masaa matatu yaliyopita bado views 3.2m,ukiona hivyo wanaivalidate kwa hiyo kuna mawili views ziongezeke au zipungue.
Zitaongezeka. Jana usiku niliona laki 9 plus hivi ila kukawa na malalamiko sana you tube. Hivyo update ya baadaye ni lazima ipande. WCB na Vanny boy watatulia sasa. Jeshi siyo saizi yao.
 
Wimbo wa attitude wa Harmonize yafikisha views million 3 ndani ya masaa 27 you tube. Hii ni record ya aina yake inawekwa na Harmonize. Kama anatania vile lakini ndo anachukua kijiti Cha king of bongofleva kwasasa. Tumsuport jeshi ili tupate kuongeza international artist from Tanzania.
Iyo mistari yako miwili ya mwisho ni migumu sana kwa nchi iliyojaa masikini...
 
Mnachekesha sana sana. Mimi sio mpenzi wa nyimbo za kigogo. Lakini leo nimetazama mwenendo wa YouTube. Nimekuta winbo unao seems umeshuka baada ya watendaji wa YouTube kupunguza watazamaji waliohurudia mara nyingi. Na kuwabakisha kwa wale walio tazama maramoja tu.
Sijaelewa samahani lakini
 
Unashngaa nini aise na wakati hio ni kazi ya genge la uhalifu la wcb kuna kitu walienda kufanya au kuna watu wanawatumia kwenye hizi selfish jobs zao, kwanini wasikubali tu kua harmonze ni genious na anajtegemea kwa sasa na hana shobo na mtu, wao waendelee na kununua private jets wao si wana hela bwana
Haya mambo huwa yananishangaza sana unatumia gharama kumuharibia mwenzio ilihali wewe hujawahi fanyiwa huo mchezo hata siku moja........izi roho zetu ni ngumu sana


Hii nyimbo ni another kwangwaru huko mtaani
 
Huu mchezo hauhitaji hasira. Japo wimbo sijaupenda, ila harmonize nampa hongera nahisi VanyBoy anataman kufuta post yake.
Acha ushamba wasafi wanamiliki YouTube? Mbona huwa mnajitoa ufahamu nyie au wewe ni H Baba
 
Kweli mziki wetu unakoenda hatutapata tena vijana wapya wazuri maana kuna watu wazuri sana lakini hawana fan base ndio wanataka kutoka sijui watatokea wapi maana ushindani ni views siku hizi sio mziki bora na wengi watakatishwa tamaa mziki utabaki kama mpira uwe Yanga, Simba au Azam basi na ndio tuna team 3 sasa hivi super league wengine chezeni Voda league. Hatuendi kuzuri hatujadili tena mziki mtamu au hapana ila views so sad lakini ndio hali halisi, ambao hamjatoka kimziki fanyeni kazi zingine mtapata stress na hii industry.
Mariooo namuonea huruma sana
 
Acha ushamba wasafi wanamiliki YouTube? Mbona huwa mnajitoa ufahamu nyie au wewe ni H Baba
Kuna sehemu nimesema wasafi kumiliko youtube? Unasoma lakini hata huelewi unachokisoma.
 
Hayo makelele mnayoyasema ndio vibe lenyewe hilo ukisikiliza nyimbo za Awilo Longomba anapenda makelele yaani namkubali sana na nimefurahi Konde kushirikiana na Awilo,

#Attitude#
Kweli kabisa awilo alitufanya vichaa kweli kweli miaka ile kwa makelele yake...[emoji3][emoji3][emoji3]umenikumbusha mbali
 
Back
Top Bottom