Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Jamii forum,msiwe wa kukimbilia kutukana watu kwa msilojua.hii ni hatari kwa mtandao huu ambao umekuwepo,na kupitia misukosuko.wewe mchangiaji hujifichi.kuna siku utalipa matusi yako
 
Pengo ameongea maoni yake, lakini ameheshimu maamuzi ya Maaskofu wenzake kwa kusaini tamko ili liweze kusomwa kwenye makanisa yaliyo chini ya Jimbo lake la Dar es Salaam, na tayari yameshasomwa. Sasa tatizo liko wapi, mbona amesharuhusu lisomwe?
 
Wakristu wakatoliki,wanaelimishwa na kuachwa kuchukua hatua wenyewe.Sio mbumbumbu.
 
Na ipo Siku,wewe uliyetukana,na Gwajima mtaomba kumeza kauli zenu
 

Nimekuuliza hebu toa kipande cha nukuu ambacho Pengo amekubaliana na Mahakama ya Kadhi, usikwepe swali
 
Laana ya wakulima aliowatukana lazima itamkuta
Amen.......pamoja na waumini wake waliokuwa wakishangilia bila kujua kuwa wametukaniwa wazazi au hata ndugu zao waliowaacha vijijini wakihangaika na kilimo....ambacho taifa limekiri kuwa ni uti wa mgongo wa uchumi huu......
 
Gwajima hajui asemalo.hajui siasa,wala Dini.Bora angedili na mbasha
 
Na kingine matusi ya humu ni udini tu.tumekuwa vipofu kabisa kwa hilo
 
Gwajima anasema kanisa katoliki limewalea halafu anatukana walezi kiasi hiki? Hii inawezekanaje jamani kumtukana mlezi hata kama kakosea
 

Akili zako ni fupi kama za gwajima
 
Gwajima ni mpuuzi sana....ana kiburi kiasi kujiona yeye ni Mungu mtu.Awatishe hao hao kina Mbasha maana anajua hawezi kumfanya lolote pamoja yakuwa anamto.mbea mkewe.

Nimemdharau sana Gwajima kwa hili, na wote waliomsapoti.
 
Lawama nyingi ambazo anatupiwa bwana Gwajima si kwa kupingana mitazamo yake na kiongozi mwenzie wa kiroho....bali kwa lugha aliyoitumia kufikisha ujumbe wake...yeye kama kiongozi wa kiroho ambaye waumini wake ndio kimbilio lao kwa ushauri na huduma za kiroho hakupaswa kutumia lugha kali namna hata kama angekuwa ameudhika kiasi gani na kauli ya kiongozi mwenzie.....angepaswa kuwa mvumilivu na angetafuta njia nyingine ya busara na hekima katika kumfikishia ujumbe bwana Pengo na nina hakika ujumbe wake ungefika na ungefanyiwa kazi........labda kitu ambacho bwana Gwajima hakijui ni kuwa pamoja na kuwa bwana PENGO ni kiongozi mkubwa wa kiroho lakini pia ni mwanadamu ,na inafahamika kuwa miongoni mwa wanadamu hakuna mkamilifu.......kuna kipindi wanadamu ndimi zetu huteleza kujikuta tunaongea kauli zinazoleta utata miongoni mwa jamii zetu........vile vile angepaswa kufahamu kuwa Pengo kama akiwa kama mtu kama watu wengine naye anayo haki ya kutoa maoni au kueleza jambo kulingana na anavyoona yeye......kama viongozi wetu wa kiriho wanakosa busara na kushindwa kuwa wastahilimilivu kwa kutofautina kauli na viongozi wenzao na kumwaga mitusi mazabahuni tena mbele ya hadhira kana kwamba yupo sokono na sio maeneo anayoyaita matakatifu.....je hali ikoje kwa waumini wao..........???
 
Nimekuuliza hebu toa kipande cha nukuu ambacho Pengo amekubaliana na Mahakama ya Kadhi, usikwepe swali

Nina hakika hata haujui nini unahitaji bado! Soma vizuri hapo juu kwenye comment yangu kisha njoo tena nikufungue akili iliyologwa.

Na kama huna Audio clip ya pengo nifate inbox nikutumie usikie anavyojitetea utumbo, issue hii ni zaidi ya mahakama ya kadhi ila ni namna alivyowasaliti wenzake na kwa historia mambo haya Pengo hajaanza leo kuwasaliti wenzake yaani Baraza la Maaskofu Tanzania na kuibukia upande wa serikali.
 
MIMI NI MKRISTO NA SIO MUUMINI WAKE ILA NI MKRISTO WA FPCT, Namuunga Mkono Gwajima... Hakuna lugha nyingine ya kuwaambia wanafiki na wasaliti...

Hayo maneno ni saizi yake kabisa... Pengo ametuaibisha na kudharirisha wakristo kwa kujitenga na kujiamulia mambo yake mwenyewe huku akijwa mjumbe/mwanachama wa Baraza la Maaskofu.

Lawama hii haimkwepi hata kidogo...
 
Nimemdharau sana Gwajima kwa hili, na wote waliomsapoti.

Siku nyingi nilishamdharau huyu jamaa.....toka alipoanza sarakasi zake zakumvuta Amina Chifupa nakusema yupo maeneo ya kibaha anakuja.Nikamuweka katika kundi la wachumia tumbo tu.
 
kardinari pengo hakusema watu wapige kura ya ndio au hapana. ila alitaka watu wasome hiyo kstiba pendekezwa na wakishaielewa wafanye maamuzi wakati wa upigaji kura utskapofika. sasa gwajima kama hilo lilimkwaza naona haikuwa busura kutoa hayo matusi hasa akiwa madhabahuni. angepaswa kutafuta utaratibu wa kuwasilisha hoja zake kwa njia ya kistaarabu kwani si kila wakati watu wote tutafikili sawa. na ikumbukwe wote pengo na gwajima si malaika na hawana mamlaka ya kutuamlia mambo yetu. pengo kama alikubaliana na wenzake kabla ya kutoa tamko na baadae akaja kupinga basi hakufanya vema lakini ka hakuhusika katika maamuzi atakuwa na uhuru wa kutuo mawazo yake hayo.lakini gwajima haijarishi pengo kakosea kiasi gani hakupaswa kupolomsha matusi kiasi hicho hasa kama mtumishi. anapaswa kuonya, kushauri na kurekebisha kwa namna ambayo ni nzuri kwani nionacho hapo ni kama alikuwa anajitafutia tu ujiko kwa wafuasi wake. lugha ya ustaarabu ingempa heshima zaidi kuliko matusi na dharau. ni hayo tu
 
Kwa akili yako Pengo alipowasaliti Maaskofu wenzake alifanya haki?????

Msimamo wa maaskofu kwa umoja wao ndio msimamo wa kanisa.....lakini Pengo nje ya umoja ule ni mtanzania na ana uhuru wakutoa maoni yake.Jaribu kutofautisha hizo kofia ndipo uje kubishana hapa.
 
nimemdharau sana gwajima kwa hili, na wote waliomsapoti.

aisee.... Na mimi nimekudharau sana kwa hili kwa sababu hujui nini kinaendelea na hufikirii kuwa alichokifanya kardinali pengo ni kulitukanisha na kuligawanya kanisa mbele ya jamii ya watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…