Gwajima! Ni mtu hatari sana kwa kauli zake anachanganya madawa, kama angekuwa ni mtu mwenye busara angetoa mtazamo wake na angeheshimimu mawazo ya Pengo kwa kuwa alitoa msimamo wake kama mkuu wa Kanisa Katoliki, hivi jamani busara ya huyu Gwajima iko wapi, tuipime kwa kijiko cha sukari? ni kiongozi wa kiroho au? Sielewi nisaidieni maneno aliyoyatoa ni ya kulaaniwa na kupingwa na kila mtu anayeheshimu uhuru wa mawazo bila kuvunja sheria kwa kutoa maneno ya kejeji,vitisho,au matusi dhidi ya Pengo.
Namshangaa huyu Gwajima anajitokeza hadharani na kumtusi Pengo, hivi ana usafi gani katika hiyo huduma yake,tusimwage mchele kwenye kuku wengi.Nikiwa mmoja wa waumini natangaza rasmi kujitoa kwenye Kanisa la Gwajima. simuungi mkono wala sishabikii kauli zake kwa kuwa amekengeuka.