Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Nina hakika hata haujui nini unahitaji bado! Soma vizuri hapo juu kwenye comment yangu kisha njoo tena nikufungue akili iliyologwa.

Na kama huna Audio clip ya pengo nifate inbox nikutumie usikie anavyojitetea utumbo, issue hii ni zaidi ya mahakama ya kadhi ila ni namna alivyowasaliti wenzake na kwa historia mambo haya Pengo hajaanza leo kuwasaliti wenzake yaani Baraza la Maaskofu Tanzania na kuibukia upande wa serikali.
Umesema mahakama ya kadhi, usianze kutoroka, kaa hapo hapo. Usisingizie ni zaidi ya mahakama ya kadhi, baki na msimamo ule ule uliosema kwamba Pengo ametetea mahakama ya kadhi. Clip ninayo na ina urefu wa dakika 4 na sekunde 35. Hakuna mahali ambapo Kardinali amezungumzia mahakama ya kadhi!
 
Sasa huyo gwajima ana hekima gani kama ndio anashindwa kuhimili aliosema Mwadhama Kardinal Pengo?
Kiongozi lazima awe Mtumishi kwa hio pengo kacheza nafasi yake ilivyo, gwajima amechanganya huko na hisia zake binafsi

Huwezi kumtukana kuongozi mwenzio hivi Pengo ni kiongozi wa Katoliki huwezi kumtukana kiasi hiki wakatoliki wakakaa kimyaa..... umemdharirishaaaaa......
 
Bwana mdogo ushabwia ugoro nini!!?
Pengo alichopinga ni waumini kulazimishwa kupiga kura ya hapana na sio kukubali mahakama ya kadhi uwe unachangia kitu unachoelewa acha kukurupuka.

Siasa hizi zinaelekea kutugawa mda si mrefu kwanza ameambiwa ahamishe kanisa lipo mahala pa NHC......
 
Mama yangu weeeeeee! Ukweli Gwajima katumia lugha isiyokuwa ya kistaarabu. Hata kama anapingana na kiongozi mwenzake wa roho ingekuwa vema akatumia lugha ya kiutu uzima na ya staha kuliko kumchana live kama mtu wa bongo flava. Nimesikilza mpaka nikaona nafsi yangu inaniambia tuna viongozi wachache sana wa dini, wengi ni wajasiliamali wa dini.

Upumbavu hauna jina jingine zaidi ya kuitwa ni upumbavu, alichokifanya pengo ni upumbavu hivyo lazima tuukate kwa lugha zote bila kulemba.

Asante sana Nabii wa kweli na mpaka mafuta Gwajma.
 
a jamaa alituumiza sana, yaani jamaa aliuza kila siri ya chama kwa CCM.

Siri gani kavujisha uitaje ili uitaje hamwezi kuhendekeza siasa za uzushi eti ndiyo wanakuja kutukomboa kwa kutaka kutugawa watz.....
 
We mbona umewasaliti wazee wako wa Kamachumu na kujiunga na Chadema?
Au unataka tukudadavue hapa?

Maneno ya kulishwa ooo msaliti kwa kutumia haki kikatiba ya kutoa maoni binafisi....
 
Upumbavu hauna jina jingine zaidi ya kuitwa ni upumbavu, alichokifanya pengo ni upumbavu hivyo lazima tuukate kwa lugha zote bila kulemba.

Asante sana Nabii wa kweli na mpaka mafuta Gwajma.
Kwani Pengo hana haki ya kuwa na maoni au mtizamo binafsi kwasababu tu ni askofu au kardinali. Mbona alishaweka wazi kuwa hayo ni maoni yake binafsi?
 
Pendo ndo kajidharirisha, Pengo ni mpumbavu hata mimi namuunga mkono Gwajima, kwa hali ya sasa ya Tanzania hakuna mtu mwenye akili timamu ataunga mkono MAHAKAMA YA KADHI.
Wewe na gwajima na wenzako mnaonyesha jinsi gani vikanisa vyenu havina Yesu. Pengo alichosema kakosea wapi? Ni vibaya kutaka waumini wapige kura kwa free will yao? Busara tupu Kardinali katoa. Na barua ya maaskofu wa TEC imetoa pendekezo tu. Siyo kuwachagulia waumini kura ya ndio au hapana. Na busara kama hii huwezi kuipata kwenye makanisa yasiyo na apostolic succession, yani ambayo si katoliki. Maana Katoliki ndiyo kanisa lenye mamlaka kamili kutoka kwa Yesu ,kwenda kwa Petro ,nk.Nyie mnawapa ujumbe gani waislamu? wao kumbuka siku zote wanapinga tu ukristo, wanaona kila kitu ni njama ata kama kina wafavor wao. Kanisa halitoshurutisha wala kusema kura ya kupiga. Jukumu la kanisa ni kuelimisha muumini alafu yeye mwenyewe ndiyo atakayeamua kwa utashi wake aliopewa na mwenyezi Mungu. Angalia hako kashetani kapotoshaji sijui gwajima, hiyo ni busara gani? hapo ndio Roho Mtakatifu kweli anafanya kazi? Nawahurumia waumini wake kama ndiyo kiongozi wenu na ibada zenu ndio zilivyo duh!!
 
Tatizo watu wametekwa na siasa, hawataki kuambiwa ukweli hata kidogo. Mahaba ya siasa ndio yanayowafanya wamtukane Pengo na kuona kakosea alichokisema. Pengo kama mkuu wa kanisa katoliki Tanzania hawezi kuona mambo yanaenda kinyume halafu akakaa kimya, haiwezekani.

Kanisa halijafikia hatua ya kufanya maamuzi kwa niaba ya waumini wake, kanisa halijafikia hatua ya kulamisha watu katika suala linalohitaji haki na uhuru wa mtu. Kumwambia mtu lazima akapige kura ya hapana hiyo si sawa hata kidogo, na hata kumwambia mtu lazima akapige kura ya ndiyo nayo si sawa hata kidogo.

Mtu anapaswa kupiga kura kwa mujibu wa maamuzi na matakwa yake binafsi na si kulazimishwa. Ni sahaihi kuwaelimisha watu manzuri na mabaya ya katiba pendekezwa lakini si sahihi kuwapangia watu kura ya kupiga.
kwanini ccm wanawafundisha wananchi wapige kura ya ndio mkukiiiiiiii.......kwa....nguruwe

umeona askofu pengo alivyopewa vidonge vyake YUDA ESKARIOTE MSALITIIIIIII
 
Safi sana MCh Gwajima,watanzania hatujazoea kukaa na vitu kama wakenya,ni lazima mambo ya kipuuzi yakemewe hazarani pasipo uoga,haiwezekani eti kiongozi wa dini unaanza kujiingiza kwenye masuala ya siasa,badala yakumtetea yesu unatetea watawala wa dunia kama yuda eskariot...hakika mwaka hautaisha pigo la mungu litakupata.yuda alijinyonga wewe badala yakutetea watawala wa dunia mbele za yesu,wewe itakuwa zaidi ya hilo.
 
Naunga mkono hoja zote gwajima alizoongea.

Nadhani pengo asipotubu na kutengua kauli, atakufa ghafla.
Hata mimi sikupendezwa na kauli ya Pengo..

Ila naomba nioneshe tusi alilotoa Pengo mpaka akubali kutukanwa matusi yote hayo..

Huyo Gwajima hakuweza kutumia lugha ya busara kufikisha ujumbe wake..??
 
pengo sijuu nimpe laana gani mbayaaaaa.anafaa kufungiwa jiwe azanishwee kwenye karooo la maji machafuu
 
Kwani Pengo alisemaje wadau naona na mimi ilinipita. Tatizo mb 8
 
Hiyo madhabahu aliyotumia ngwajima kumkashifu Pengo ndio hiyo hiyo hutumia kuita Roho Mtakatifu na Damu ya Yesu ama kuna madhabahu nyingine? Kama ndio hiyo hiyo Je? ni mungu yupi anayemtumikia? Kusali kwenye madhehebu yasiyoeleweka ni kujitafutia laana tu.
 
hata mimi sikupendezwa na kauli ya pengo..

Ila naomba nioneshe tusi alilotoa pengo mpaka akubali kutukanwa matusi yote hayo..

Huyo gwajima hakuweza kutumia lugha ya busara kufikisha ujumbe wake..??

hakuna matusi hapo ila ni maneno ya uchungu aliyoyatoa gwajima,mpuuzi ni mtu asiyetenda mambo inavyotakiwa
 
Back
Top Bottom