Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

"not guilty until innocent proven" sasa gwajima kaprove guiltiness ya pengo kwa kuwasaliti maaskofu wenzake na mabaraza mengine yakikristo.Tusi gani gwajima alilotukana ndugu fazili?

Kwani ni wapi Pengo amesema Wakapige Kura ya NDIYO??????

Mpaka Ifikie Gwajima kusema Amewasaliti?
 
Baada ya kusikiliza clip ya Gwamija, nimeshangaa sana, hivi kweli mtu mwenye akili timamu anaweza kusali kwa Gwamija!? Huyu ni mpuuzi, mpumbavu na mshenzi, kweli dini imeingiliwa au ndiyo zama za mwisho..
 
Kama serikali ya CCM imeweza kuwashawishi na kuwaambia watu kabla hata haijawapa hiyo katiba elekezi na kuwaelimisha watu "imetoa wapi haki ya kuwaambia wananchi wapigie katiba kura ya NDIYO?"

Ambayo vingozi wa dini wananyimwa kuwashawishi waumini wao kupiga kura ya HAPANA..

CCM imetoa wapi hiyo haki? Kwann viongoz wa madhehebu wasiwe na hiyo haki pia? NAKUSHAWISHI UNAYESOMA HAPA PIGA KURA YA HAPANA KWA KATIBA MPYA INAYOWEKA MASLAHI YA KUNDI DOGO LA WATAWALA MBELE NA KUDIDIMIZA HAKI ZA WANYONGE TULIO WENGI..
 
Umechanganya madesa kazi ya kiongozi wa dini ni kuonyesha njia mpasayo mtu kuifuata si option ya kuchagua ila mmlaka ya kuchagua njia gani aifuate ipo katika mtu mwenyewe.

Tulia mi nimequote maneno ya Pengo... Na ulichokisema ndo alimaanisha. maaskofu wamesema wakapige kura Ya Hapana ... Ila pengo amekataa kuwashurutisha wakristo wote kama Watoto wasiojua kitu. Kwahiyo Waumini ndo wanauamuzi wote wa kupiga kura ya Ndio au hapana

Huwezi niambia kuwa Mkristo amabye Chama ni Diehard wa CCM ataenda kupiga kura ya Hapana
 
Wote mnaoshabikia alichosema Gwamija ni wapuuzi na washenzi.. inaonyesha namna gani mlivyokuwa na uelewa mdogo
 
kama viongozi wa dini hawana haki yakuwaambia watu waseme no basi na wanasiasa,TBC na wewe pia ni wakosaji.hamna haki ya kuwaambia watu waseme no.msiwatukane.tusiwe na double standard hapa.ama kanya kuku kwa hio bata kaharisha?tusitumike hivyo
 
bomouwa;

Kwa maoni yangu Mtumishi wa Mungu anatakiwa atumie lugha ya staha kwa waumini wake na hata kwa wengine wasiowaumini wake. Ukisikiliza hiyo Clip ya Mchungaji Gwajima kweli inatia kinyaa kwa wapenda ustaarabu. Kwani lazima utukane fulani ni mpumbavu, mjinga, hovyo ili kujenga hoja? Askofu Pengo alitoa maoni yake binafsi na pengine si kwa cheo chake kama Askofu Mkuu. Maoni yaweza kukubaliwa au kukataliwa lakini kutukana mtu kwasababu hukubali maoni yake hapo naona si sawa.

Mimi ni Mkatoliki lakini sikubaliani na mapendekezo ya maaskofu kwamba tusome katiba halafu tuipigie kura ya hapana. Hivi kuna mantiki gani ya kusoma kitu ambacho viongozi wa kiroho wameshachukua maamuzi ya kupiga kura ya hapana? Yaani ni kama vile waamini hawajui kusoma hivyo viongozi wa kiroho wamesoma kwa niaba ya waamini wao na kuwafanyia maamuzi.

Ni jambo lililo bayani kwamba waumini wa madhehebu mbalimbali wana uelewa tofauti tofauti, kwa mantiki hiyo maaskofu wangeshauri kuwa waumini wasome katiba vizuri na kuelewa na mwishowe wafanye maamuzi yaliyosahihi kwa kuzingatia walivyoielewa katiba. Utaniambiaje fanya uamuzi fulani wakti na mimi naina uwezo wa kuchambua mambo?

Kama kweli maaskofu walitaka waumini wao wapige kura ya hapana, basi wangewaambia waumini wao kuwa mchakato mzima wa katiba haukufuata taratibu zinazokubalika kiimaadili (kama ambayo walijaribu kuonyesha) na hivyo basi hakuna haja ya kuisoma hiyo katiba iliyopitishwa kwa mizengwe, ikataliwe. Lakini kwa kuwa wamesema waumini waisome vizuri hiyo katiba pendekezwa, basi wawaachie waumini wenyewe wafanye maamuzi.
 
Last edited by a moderator:
MABAGHEE;

Ni kweli ngwajima alitumia maneno makali sana lakini contents ya alichokizungumza kina mashiko na Pengo amevuna alichopanda.
 
Last edited by a moderator:
Naona huyo gwajima amechoka kuwatoamba wake za watu kaamua kuhamia kwenye siasa
 
.....Pengo ni mnafki sana, kama analijua hili kwanini asingegoma kusign ktk huo mkataba baada yake akasign kisha akaja kusema pembeni mambo ambayo no tofauti na mkataba.
.....Viongozi wa kiroho (Maaskofu) siku zotr huwa wanatutakia mema, mimi binafsi kwa taifa letu lilipofikia naona ni vema kwa wao kuungana na kupiga kura ya HAPANA.
.....Na ifahamike kwamba, Wakristo wengi au Watanzania wengi hawajaisoma Katiba Ipasavyo, kama wao wameiosoma na wameona haitafaa kwa Maslahi ya Watanzania ila ni kwa maslahi ya CCM ni vema wakatuambia ukweli na tuikatae.
.....Pengo najua ameona madhaifu ya KATIBA na yeye kama kiongozi alipaswa kusimama wima na kupinga vikali juu ya hiyo katiba, sio kuanza kuwa na maamuzi mepesi mepesi wakati ikipita Maisha ya Watanzania yatakuwa mabaya zaidi.
.....Asilimia kubwa ya maoni ya Watanzania yametupwa nje, sasa hiyo ndo Katiba ambayo tunaitaka? Mimi nasema kwamba Hakuna Mtanzania mwenye uchungu na nchi yake ambae ataikubali hii Katiba, hata mimi ninhekuwa na uwezo wa kupita kila mahali na kusema watu waikatae katiba mpya basi ningefanya hivyo.
.....Pia tutambue kuwa waliomuona Pengo ni mpuuzi sio Gwajima tuu, Chama cha Maaskofu Tanzania kipo na watu wengi, nadhank wote wamemshangaa Pengo na wakaamua kuwa na maneno ya pembeni, heri Gwajima katoa yake ya Moyoni.
.....Naungana na Gwajima kuwa Pengo ni mbweha tuu.
 
Pengo ni mpuuzi coz alipuuzia makubaliano ambayo maaskofu wote kwa umoja wao walikubaliana kuhusu jambo husika.
Pia Pengo ni mnafiki coz alijitenga akaongea kinyume na makubaliano ya maaskofu wenzake kwa lengo la kujipendekeza serikalini.
Ingelikuwa enzi za Agano la Kale angepigwa mawe.

Naloli uli gwa mahala nkamu!
 
Mgombea urais mmoja kaenda kuombea na Gwajima Fuska mkubwa mvunja ndoa za watu na dealer mkubwa wa dawa za kulevya aibu
 
Kama serikali ya CCM imeweza kuwashawishi na kuwaambia watu kabla hata haijawapa hiyo katiba elekezi na kuwaelimisha watu "imetoa wapi haki ya kuwaambia wananchi wapigie katiba kura ya NDIYO?"

Ambayo vingozi wa dini wananyimwa kuwashawishi waumini wao kupiga kura ya HAPANA..

CCM imetoa wapi hiyo haki? Kwann viongoz wa madhehebu wasiwe na hiyo haki pia? NAKUSHAWISHI UNAYESOMA HAPA PIGA KURA YA HAPANA KWA KATIBA MPYA INAYOWEKA MASLAHI YA KUNDI DOGO LA WATAWALA MBELE NA KUDIDIMIZA HAKI ZA WANYONGE TULIO WENGI..

......Jana kuna watu nilikuwa nakaa nao nikaanza kuwaambia alichosema Pengo na walichosema Jumuiya ya Wakristo.
.......Nikawashawishi wapige kura ya hapana na wote wamesema kuwa kuikubali katiba hii pendekezwa ni sawasawa na kujichimbia kaburi.
 
Mi hata sipati jibu,hivi kuna watu wanaojielewa kweli wanaohudhuria hizo ibada za wachungaji wa sampuli hii?

Sampuli ya Wasaliti na wanafiki kama Pengo? Wapo wengi na yawezekana wewe pia ni mmoja wapo.
 
Kardinali Pengo amekuwa siku zote mwiba kwa serikali na hana haja hata kidogo ya kujipendekeza kwa watu waliopo chini yake.

Kwa hiyo wewe unakubaliana na kulazimishwa upige kura ya hapana na unafurahi tu kwa jinsi ulivofilisika kiuelewa wa mambo

Acha uongo kijana! Kama huna taarifa kaa kimya kabisa.

Pengo amekua mwiba upi wa Serikali labda zamani akiwa kijana ila si sasa tena.

Kipindi cha Bunge la Katiba Pengo aliingilia mchakato wakati watu wanadai Tanganyika yeye alikurupuka kwa mahaba yake na CCM akawa anasema serikali ziko mbili hadi akaja kuumbuliwa na Askofu Paul Ruzoka.

Kama hujui jambo hili kwa kina utaishia ushabiki wa ukatoliki wako tu hapa, Ukweli ni kwamba PENGO NI MSALITI
 
Baada ya kusikiliza clip ya Gwamija, nimeshangaa sana, hivi kweli mtu mwenye akili timamu anaweza kusali kwa Gwamija!? Huyu ni mpuuzi, mpumbavu na mshenzi, kweli dini imeingiliwa au ndiyo zama za mwisho..

Mkuu, gwajima ni mwenda wazimu, ana mihemko ya kijinga sana.
Kila mtu anauhuru wa kutoa maoniyake,
hatakama anadhani kwamba Pengo amekosea, jinsi alivyo mkosoa angetumia maneno ambayo yange onyesha kwamba kweli yeye ana akili na maoni mazuri kuliko Pengo na sio kulopoka lopoka kama muhuni.

Otherwise labda atataka sifa aonekane ana bishana na Pengo.

Mtumishi gani wa Mungu huyu ana ongea maneno kama chizi!!!.
 
Back
Top Bottom