Nimesikiliza kwa makini clip ya Pengo na ile ya Gwajima na haya ni maoni yangu. Lakni kabla naomba kudeclare kuwa mimi sio mkatoliki na sio mfuasi wa Gwajima na pia binafsi sikubaliani na kuingiza masuala ya kidini kwenye katiba:
Askofu Pengo
Pengo was very composed, bila papara wala mihemuko
Pamoja na kwamba Pengo hakukubaliana na kile kilichomo katika matamko hayo bado alionyesha heshima kubwa na unyenyekevu kwa maaskofu wenzake walioyaandaa.
Hayo yalikuwa ni maoni yakebinafsi – kila Mtanzania ana haki ya kutoa maoni yake
Maaskofu hawana mamlaka ya kuwalazimisha waamini watende kitu kinyume cha dhamira zao, kwa sababu hata Mungu hamlazimishi mtu kutenda mema. Mungu anatuacha kama wanadamu tutende sawasawa na dhamiri zetu, kama anavyoamini kuwa Mungu anamwelekeza – Ni kweli, hakuna mwanadamu mwenye haki ya kumwamulia mwanadamu mwingine nini cha kufanya, mwanadamu anaweza tu kumshauri mwingine na sio kumlazimisha
Maaskofu hawana mamlaka ya kuwalazimisha watu kupiga kura ya hapana, waumini sio watoto wadogo wa kuambiwa kila kitu. Jambo hili linadharirisha uhuru wa waumini wa Kikristo – Ni sawa na hapo juu
Matamko haya (lile la Baraza la Maaskofu na lile la Jukwaa la Wakristo) yanawagawa Watanzania kati ya Wakristo na wale wasio Wakristo – Sina hakika na hili
Matamko haya yanawagawa Wakristo dhidi ya serikali yao – Sina hakika sana na hili
Askofu Gwajima
Gwajima alikuwa amejaa mihemuko na hakuwa ametulia kabisa
Gwajima katika hotuba yake alipungukiwa na hekima kwa kiasi kikubwa sana. Kwa mtu mwenye hekima hata kama anapinga au kukataa jambo atatumia lugha ya hekima na isiyo ya kuudhi. Binafsi siamini mameno kama mpuuzi, hafai, amezeeka, mtoto mdogo amevaa pampers, ukome, amempa vipande vyake, hana akili, n.k yanafaa kutumiwa na mtumishi wa Mungu, tena akimshambulia mtu anayemzidi umri. Hayo ni maneno ua mtaani zaidi na hayategemewi kabisa kutolewa na mtumishi wa Mungu. Hivi kweli kulikuwa hakuna maneno mengine ambayo Gwajima angeyatumia kufikisha ujumbe wake badala ya hayo yanayoudhi namna hiyo
Gwajima anadai Pengo alisaini matamko hayo – sio kweli, ni askofu Ngalelemkutwa ndiye aliyesaini kwa niaba ya TEC
Gwajima anawaambia watu wasimuheshimu Pengo – hakuna mwanadamu mwenye haki ya kumwamulia mwingine cha kufanya, kila mtu ana uhuru wa kufanya sawasawa na anavyoongozwa na dhamiri yake mwenyewe. Mwanadamu anaweza akashauri tu.
Ameliaibisha kanisa katoliki na kuwaaibisha maaskofu wakatoliki na wengineo na wakristo – sioni mantiki hapa, Pengo alikuwa anatoa maoni yake binafsi na sio msimamo wa maaskofu wala Wakristo. Pia Pengo alitoa angalizo la kuwafanya watu wachague au wasichague kitu kwa sababu tu wao ni Wakristo
Gwajima anamtakia Pengo apate matatizo, tena apigwe na malaika – hii ni kinyume kabisa na mafundisho ya Bwana Yesu aliyesema "Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi" – Mathayo 5:44