Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Screenshot_2017-03-19-02-08-04.png
 
Unajua huyu jamaa anayeitwa Askofu au sijui mchungaji Gwajima nilikuwa sijawahi kumfuatilia kwa ukaribu hivyo sikuwa najua mengi juu yake.

Lakini tokea haya mambo ya ile taja taja ya wahusika wa madawa ya kulevya ndo kidogo kidogo nikaanza kumfuatilia.

Eti naye anajiita ni dokta. Yaani ana shahada ya uzamifu. Shahada yenyewe kaipatia kutoka chuo kiitwacho Omega Global University.

Vichekesho! Omega Global University ni diploma mill! Chuo hakina hata accreditation ya maana.

Tuachane na hayo ya 'PhD' yake. Tuje kwenye mwenendo na mdomo wake.

Baada ya kuiangalia hii video sasa naelewa ni kwa nini alidai anavyo vyeti vya Paul Makonda ofisini kwake [which was dumb].

Hebu sikiliza hayo maneno aliyoyaongea kuhusu Kadinali Pengo. Eti huyo ndo askofu. Askofu mwenye wafuasi tele.



Huyu mtu hana credibility yoyote ile. Ni msanii tu. Alifaa awe kwenye tasnia ya akina Omari Tego na akina Mwinyi Mkuu. Huko kwenye utumishi wa mungu anafanya utapeli tu.

Awali nilikuwa sielewi kwa nini anafanya hivo anavofanya ila sasa nishaelewa.

Ila hao wafuasi wake nao hmm....kaazi kweli kweli yaani!

Blaza ngabu hayo uliliyoyasema yote tunayafahamu,hiyo ishu ya kumtukana le kadinali linafahamika na lilijadiliwa kwa upana kipindi zinatokea,zipo tuhuma na skandali nyenginezo nyingi tu kama kutaifish mke wa mbasha,kujilimbikizia mali za sadaka,kutukana waislamu na mengineyo mengi
Hivyo tunafahamu kuwa gwajima ni msanii kama makonda na trupsi lake la akina le mutuz,mange naye inafahamika ni mental case tokea siku mingi,Kinachotuvutia sisi kufuatilia hili songombingo ni kuwa wote wanavuana nguo na kuumbuana,kila mmoja anavujisha siri na maovu ya mwenzake.
Huu mtanange ndo umeibua suala la ukakasi wa elimu ya mkuu wa mkoa,swala ambalo linatuhusu pia sisi wananchi.
 
Huyu Gwajima na Mange Kimambi hawana tofauti yoyote.
 
Ninachokiunga mkono ni ukweli na haki tu.

Kama Makonda kafoji vyeti na aende jela.

Mpaka sasa sijaona ushahidi wowote ule wa kunishawishi kwamba ni kweli kafoji.
Gwajima alushawahi fanya kazi baraza la mitihani la taifa? Au anategemea umbeya?
 
Kwani huyo Gwajima yeye ni kabila gani?
Anadharau mtu wa kwao msukuma mwenzie Biblia inasema amelaaniwa mtu asiyependa wa kwao Ni mbaya kuliko wapagani wasioamini .Hii vita ya kumpiga vita makonda haikutakiwa kutangazwa na mtu wa kabila yake au walokole Wenzie Kama gwajima nk Vita ya mtu wa kwetu hairuhusiwi hata Kama mtu wa kwetu ana sifa chini ya kiwango
 
Back
Top Bottom