Audio: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu, amezungumza na waandishi wa habari leo, Januari 7, 2022

Audio: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu, amezungumza na waandishi wa habari leo, Januari 7, 2022

Hebu twendeni taratibu...

Ina maana Mbunge/Spika wa Bunge kila anachosema kama ni cha kiserikali inatafsirika kwamba aliyeongea ni Mhimili wa Bunge, na kwahiyo kum-challenge ni kuingilia Mhimili wa Bunge?!

Anyway, wacha nami niache unafiki na niongee moja kwa moja!!!

Kusema kwamba challenge ya SSH kwa Ndugai ni kuingilia Mhimili mwingine, NI UPOTOSHAJI WA WAZI!!!

Kilicho Mhimili ni TAASISI na sio MTU au Cheo cha Mtu!! Kwa muktadha huu, Mhimili ni BUNGE na sio MBUNGE/SPIKA!!

Mbunge anapoongea au kufanya kazi ya Kibunge NDANI YA BUNGE, anakuwa amefanya au kusema kwa niaba ya Mhimili!! Na anaposema kwa niaba ya Mhimili, hapo ukimwingilia au kum-challenge ndo utakuwa unau-challenge Mhimili kwa sababu, ingawaje Mhimili ni Bunge na sio Mbunge lakini bado Bunge haliwezi kuwa Bunge bila Wabunge!!

Ni kutokana na hilo, ndo maana Ibara ya 100(2) ya Katiba yetu inasema:-

Hapo utaona wazi kwamba, Comfort Zone kwa Mbunge ni Ndani ya Bunge! Akiwa ndani ya Bunge anakuwa anafanya kazi ya kibunge kwa niaba ya Bunge ambalo ndilo Mhimili!

Na akiwa hapo, Mbunge HAKAMATIKI wala HAGUSIKI kwa sababu analindwa na Ibara ya 100(2)! Na ndo maana hata huyu Tundu Lissu mwenyewe, kaipa vitofa sana Serikali ya JPM akiwa bungeni lakini hawakuweza kumfanya chochote kwa sababu humo, at least theoretically, hakamatiki wala hagusiki!! Na kwa kujua hilo, ndo maana mara zote walikuwa wanamlia timing kwa yale atakayotamka akiwa nje ya bunge!!

Turudi kwa Ndugai vs Samia!!!

Hebu kwanza nijuzeni!

Ndugai ni Kiongozi wa Mhimili mmoja wapo and at the same time, Samia nae ni kiongozi wa Mhimili mwingine, kama ambavyo Ibara ya 33(2) ya Katiba yetu inavyosema:-

Now, WHY ionekane Samia ndie ame-challenge Mhimili wakati alichofanya Samia ndicho kile kile alichofanya Ndugai?! Mbona hatusemi kwamba Ndugai ameingilia Mhimili mwingine? Mbona hatusemi Ndugai ame-challenge mamlaka nyingine?

Najua wapo watakaosema

Lakini kama nilivyosema hapo juu... kwani Maoni ya Ndugai yalikuwa ni sehemu ya kazi zake za Kibunge ndani ya Bunge ili tuhalalishe kwamba alichofanya Samia ni kuingilia Mhimili mwingine?!

Let me again go straight to the point...

SAMIA HAKUINGILIA MHIMILI WOWOTE ULE BALI, "AMEINGILIA" UHURU WA KUTOA MAONI kama unavyotajwa kwenye Ibara ya 18(1) kwamba:-

Ndugai hakuwa anafanya kazi kama Mhimili wa Bunge kwa sababu Mhimili sio cheo bali taasisi!!! Kwa maana nyingine, maoni yake HAYALINDWI na Ibara ya 100(2) bali yanalingwa na Ibara 18(1) kama inavyotakiwa kwangu mimi na wewe hata kama sio Wabunge au Spika wa Bunge!!

Lakini hata hiyo Ibara ya 18(1), Samia ameiingilia vipi?!

Labda kama kuna kitu nime-miss lakini ninachoona Ndugai alitumia uhuru wake wa kutoa maoni ili KUTEMA NYONGO dhidi ya Samia, na Samia nae katumia uhuru wake kutema nyongo dhidi ya Ndugai... ngoma droo!!

Au, bila kujali ikiwa tuhuma ni za kweli au si za kweli, bado Kiongozi wa Mhimili mmoja ana haki ya kutema nyongo dhidi yaMhimili Mwingine lakini huo Mhimili mwingine ukijibu inakuwa ni kuingilia Mhimili ule uliotema nyongo hata kama nyongo hiyo ipo nje ya kazi ay Mhimili?

Ninachosema ni kwamba, kwanini iwe ni halali Ndugai kutema nyongo dhidi ay Mhimili mwingine lakini iwe haramu Mhimili mwingine kujibu?!

Hapo kwenye Samia kuingilia uhuru wa kutoka maoni nimeweka kifunga na kifungua semi kwa sababu sioni ameingilia vipi hata kama TL anadai Ndugai amelazimishwa kujiuzulu Sina taarifa za Samia kushinikiza Ndugai ajiuzulu au kuagiza Ndugai akamatwe... hiyo ndo ingekuwa kuingilia uhuru wa kutoa maoni!

Nilichokiona ni Samia kutema nyongo kwa staili ile ile ya Ndugai, lakini from nowhere, kama kawaida yao CCM ndo wakaanza kuibuka na kumtaka Ndugai ajiuzulu... yaani utadhani hapo kabla hawakufahamu Ndugai aliongea nini, lakini hakuwafanya chochote hadi SSH alipoonesha kutopendezwa na sindao za Ndugai... KUJIPENDEKEZA EFFECT!!

Kama wana-CCM waliona Ndugai alikuwa na wajibu wa kujiuzulu basi wangemshinikiza afanye hivyo hata kabla SSH hajasema chochote!!

PAMOJA NA YOTE hayo, Samia amekurupuka na Ndugai amehukumiwa largely kutokana na video editing na ujengaji mbovu wa hoja!

Ingawaje watu wamemkejeli Ndugai aliposema video imekuwa edited, ukweli ndo huo! Video inayosambazwa mitandaoni inaanza kwa kumuonesha Ndugai akianza kusema:-

Ukianzia hapo, ni rahisi sana kuamini Ndugai alim-target Samia moja kwa moja! Binafsi, nilipata mashaka kidogo na hivyo nikaamua ni-search more clips ndipo nikakutana na nyingine ambayo imeanza kama ifuatavyo:-



Sasa ukiachana na huo utangulizi ulioachwa kwa makusudi kabisa, ndo unakuta Ndugai anaendelea:-

Sasa ukiunganisha sehemu iliyokatwa na sehemu inayosambazwa, utagundua Ndugai alikuwa anawasemanga wanaopinga TOZO! Ndo hapo akasema hatupo bungeni kukomoa watu, kwa mfano hili la tozo tumelaumiwa sana! lakini wakati tunalaumiwa, ni tozo hizo hizo ndizo hivi sasa zinajenga madarasa na vituo vya afya!!

Na hapo ndipo akaingiza suala la mkopo wa mama, na ndipo anahoji ni lipi bora kwa taifa! Tuendelee kukamuana wenyewe kwa wenyewe au tugemee mikopo?! Na kwa maoni yake, anaona ni lazima tukamuane wenyewe kwa wenyewe, na kama 2025 mtatuhukumu na kuwataka Wafuasi wa Mikopo badala ya kukamuana wenyewe, let it be!!

Kwa bahati mbaya kabisa, SSH wakaona kipengele cha mikopo bila kufahamu hilo suala la mikopo limeingiaje!

Lakini kwa upande mwingine, nimeshangazwa sana na Mwananchi Communication kwa sababu kwa ukubwa wa hii media, sijui ni kwanini wakaamua ku-upload video ambayo imekatwa na matokeo yake ikaharibu kabisa hoja ya Ndugai!!

Aidha, nashangazwa na jazba za SSH kwa sababu kama angemuita Ndugai amuulize imekuaje tena mtu kama yeye anainanga serikali kuchukua mikopo, bila shaka Ndugai angefafanua, na kutoa full video!! Kinyume chake, SSH akanuna, na kwenda hewani huku akiwa na nusu tu ya kile alichoongea Ndugai unless kama alisikiliza yote lakini akaamua kupuuza!

Je, Ndugai alitumia vibaya Uhuru wake wa Kutoa Maoni?

Ibara ya 62(1) inasema Bunge litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge! Kwa maana nyingine, SSH nae ni sehemu ya Bunge! Na kifungu kidogo cha 3 cha ibara husika kinasema:-

Sijui mnanielewa?!

Kumbe jambo linalotakiwa kuamuliwa na pande zote mbili litahesabika limetekelezwa IPASAVYO endapo tu lina baraka za Bunge na Rais.

Sasa Je, hivi nyie mmeshawahi kusikia Samia or any former President akiingia bungeni kujadili suala la nchi kuchukua mkopo?! Kama wenzangu mmewahi kusikia, then well and good lakini binafsi sijawahi kwa sababu utaratibu haupo hivyo, bali:-

Wizara mbalimbali zinaanda bajeti zao!! Ikishafanyika consolidation, Wizara ya Fedha ndiyo itafahamu vyanzo mbalimbali vya mapato yetu! Sasa ikionekana vyanzo vyetu haviwezi kuivusha bajeti husika, ndipo hapo linaingizwa suala la MIKOPO kama moja ya vyanzo vya mapato!

Utaratibu huo ukikamilika, ndipo pale mnasikia kuna KIKAO CHA BAJETI BUNGENI!

Kazi ya Bunge ni KUIDHINISHA AU KUKATAA, chochote kitakacholetwa kwao na Wizara ya Fedha!! Wabunge mkishasema NDIYOOOOOO BAJETI YA WIZARA YA FEDHA IPITIE, hapo tafsiri yake inakuwa mmeiruhusu serikali, pamoja na mambo mengine KWENDA KUKOPA!!

Kwavile Wabunge, including Ndugai mlishamwambia Mwigulu Nchemba kwamba "BABA, BAJETI YAKO NDIYOOOO", manake Ndugai na wenzake wamemwambia Mwigulu NENDA TU KAKOPE HIYO MIHELA! Sasa wakati Mwigulu atakapokuwa anatekeleza moja ya NDIYOO ambayo ni kukopa, yeye atakachofanya sio baadae kurudi tena kwenu ili mjadili kuchukua mkopo kwa sababu mlishamruhusu!!

KItakachofuata hapo ni timu ya wachache tu, including rais, ndio watakaoshughulika na huo ukopaji, and finally, itakuwa imekamilika ile sehemu ya Ibara ya 62(1)(3) inayosema "mpaka liwe limeamuliwa au limetekelezwa na Wabunge na vile vile na Rais "! Wabunge mlishapiga makofi ya NDIYOOO ikiwa ni pamoja na NDIYOOO KOPENI TU, na Rais nae anakuja kukamilisha Mchakato akiwa na timu yake!!

Sasa kama Ndugai alishasema NDIYOOOOOO, KOPENI TU, inakuaje tena anatoka nje na kuanza kulia lia?!

Anyway, ametumia Uhuru wake wa Ibara ya 18(1)... Uhuru wa Kutoa Maoni bila kuingiliwa lakini linapokuja suala la COLLECTIVE RESPONSILIBITY, anakuwa amefanya jinai kubwa sana ya kiuongozi kwa sababu huwezi kutoka nje kupinga kitu ambacho wewe mwenyewe umeshiriki kupitisha!!!

Lau kama Ndugai angekuwa ni Mbunge wa Kawaida, well and good lakini unapokuwa KIONGOZI wa taasisi iliyofanya maamuzi halafu tena unaenda kukejeli maamuzi hayo hadharani, my friends, nashangaa akina Tundu Lissu wanaongea kirahisi rahisi tu but that's a serious violation of collective responsibility!!
Japo kwa muonekano wa kwenye makaratasi/kisheria hao watu wawili ni binafsi, Ndugai na Samia, na ni wakuu wa mihimili yao, lakini ukienda ndani zaidi utaona yupo mmoja anayeonekana ana nguvu zaidi ya mwingine, na kwasabau ni kiongozi wa mhimili mmojawapo basi mhimili anaouongoza lazima uonekane una nguvu zaidi ya mwingine.

Kwamba Ndugai alimuuliza Samia kuhusu mikopo, ni sawa, na Ndugai sio bunge, Ndugai ni Ndugai. Samia nae akatakiwa kujibu kuhusu mikopo, sababu Samia ni Samia, Samia sio serikali, ni sawa pia, lakini kiuhalisia ukweli wa mambo hauko hivyo.

Lakini badala ya Samia kujibu hoja ya Ndugai, akaishia kumsuta, huku akiwa amezungukwa na wenyeviti wa mikoa wa CCM ambao kimsingi yeye ndie mwenyekiti wao na Ndugai akiwa miongoni mwao.

Kumbuka nguvu ya huyu mwenyekiti inaingia mpaka bungeni sababu anahusika kwa nafasi yake kuwateua wagombea ubunge wa chama chake, hapa tayari anaonekana Samia ana nguvu zaidi ya Ndugai. Hapa utaona mamlaka ya Samia yanaingia mpaka bungeni, licha ya kuwa mkuu wa serikali.

Hivyo kwa muonekano wa kawaida japo Samia sio serikali, lakini ni mwenyekiti wa chama kinachounda serikali kilichojaza wabunge bungeni ambao Ndugai alikuwa Spika wao, kuwa kinyume nae kunaweza kumgharimu yeyote ndani ya chama chao bila kujali nafasi yake hata kama wakiwa mihimili taofauti, na ndicho kilichomkuta Ndugai.

Matokeo yake, licha ya hoja ya Ndugai bado alishutumiwa toka kila upande, "chawa wa mama" wote waliingia kazini.

Kauli ya NS Tulia jana ndio ikahitimisha hili, kwamba serikali haibanwi na bunge inaweza kuamua nini ichukue na kipi aiache, ajabu Tulia kwa nafasi yake akatukumbusha Rais ndie mkuu wa mihimili ndio maana akamwambia Lukuvi hutagombea uspika!.
 
Japo kwa muonekano wa kwenye makaratasi/kisheria hao watu wawili ni binafsi, Ndugai na Samia, na ni wakuu wa mihimili yao, lakini ukienda ndani zaidi utaona yupo mmoja anayeonekana ana nguvu zaidi ya mwingine, na kwasabau ni kiongozi wa mhimili mmojawapo basi mhimili anaouongoza lazima uonekane una nguvu zaidi ya mwingine.
Wanaoamini hivyo ni wale wanaosoma Katiba Nusu Nusu huku wakichanganya madesa, na cha kushangaza wengine ni wanasheria!

Rais atakabaki kuwa Rais popote pale utakapoenda duniani unless kama nchi yenyewe sio jamhuri! Watu wanachanganya madesa linapokuja suala la MIHIMILI...

Of course, Ibara ya 4 (2) inataja MGAWANYO WA MAMLAKA ya UFANYAJI JAMBO na HAISEMI kwamba hawa watu wapo sawa!!
Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki vitakuwa ni Idara ya Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Idara ya Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni Bunge na Baraza la Wawakilishi.
Unaona hapo, watu wanachosema hii mihimili ipo sawa kumbe ni mamlaka ya utendaji!! Kwamba, Serikali ndio YENYE MAMLAKA YA UTENDAJI kwahiyo Samia hawezi kukaa na watu wake wa karibu au peke yake kisha akatunga au kuanzisha sheria mpya na kuisaini kwa sababu chombo chenye mamlaka ya kufanya hivyo ni Bunge!

Hata kama mbunge mmoja anampiga mbunge mwenzake hadi kufa wakiwa bungeni, bado "Ndugai" au bunge hawawezi kutoa hukumu hapo hata kama sheria zenyewe wanatunga wenyewe kwa sababu chombo chanye mamlaka ya utekelezaji wa haki ni Mahakama!!

Mahakama na yenyewe pamoja na kwamba timu yake inaundwa na Wataalamu wa Sheria lakini bado hawawezi kukaa wakatunga sheria mpya kwa sababu chombo chenye mamlaka ni Bunge!

Hapo ndipo ulipo msingi wa mihimili hii matatu ambavyo ARE JUST ORGANS, ambazo according to Ibara ya 4(1) hivyo ni vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza shughuli za nchi! Hata kwenye familia yenu, baba anaweza kusema "wewe" kazi yako wewe ni kukata kuni, mdogo wako kuchota maji, na baba kazi yake kuwasomesha...

...hiyo haitafanya wewe na mdogo wako muwe sawa na baba yenu, na ndo maana Ibara ya 33 (1&2) inasema:-
Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano. Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
Kumbe, pamoja na hivyo vyombo kupewa mamlaka ya kutekeleza shughuli za nchi, Rais ndie MKUU WA NCHI YENYEWE!!

Muhimu ni kwamba, pamoja na yeye kuwa ndie MKUU WA NCHI, lakini linapokuja suala la utekelezaji wa shughuli za nchi kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 4(2) basi anatakiwa kuviachia vyombo husika kutekeleza wajibu wake bila kuwaangilia!!
Kwamba Ndugai alimuuliza Samia kuhusu mikopo, ni sawa, na Ndugai sio bunge, Ndugai ni Ndugai. Samia nae akatakiwa kujibu kuhusu mikopo, sababu Samia ni Samia, Samia sio serikali, ni sawa pia, lakini kiuhalisia ukweli wa mambo hauko hivyo.
Ibara ya 84(1) inasema:-
Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na Wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au wenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge
Kumbe Ndugai alikuwa Kiongozi wa Bunge... nothing less nothing more!!! Hapo kabla nimeshaeleza comfort zone ya WaBunge kama ilivyoelezwa na Ibara ya 100(1) kwamba:
Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.
Kumbe, akishakuwa nje ya bunge, huku akifanya shughuli ambazo sio za bunge basi atabaki tu kuwa Spika au Mbunge lakini mamlaka yake anakuwa ameacha bungeni!!

Kinyume chake, hapo juu umeshaona katiba inasema : " Rais atakuwa MKUU WA NCHI" na sio MKUU WA IKULU au Mkuu wa Serikali peke yake! Kwa maana nyingine, popote Rais anapokuwapo, atabaki kuwa rais kwa cheo na mamlaka!! Popote alipo anaweza kutekeleza kazi zake kwa kutumia mamlaka yake!!

That said, huwezi kusema "Samia alitakiwa kujibu kama Samia"! Lakini that's not an issue! Nimeshasema Ndugai ni Kiongozi wa Chombo ambacho kiliidhinisha serikali ichukue mikopo! Sasa kama kweli alikuwa serious, alitakiwa kwanza kujiuzuru ndipo akaosoe! Tena alitakiwa kujiuzuru soon baada ya bajeti kupitishwa!!

Lakini badala ya Samia kujibu hoja ya Ndugai, akaishia kumsuta, huku akiwa amezungukwa na wenyeviti wa mikoa wa CCM ambao kimsingi yeye ndie mwenyekiti wao na Ndugai akiwa miongoni mwao.

Kumbuka nguvu ya huyu mwenyekiti inaingia mpaka bungeni sababu anahusika kwa nafasi yake kuwateua wagombea ubunge wa chama chake, hapa tayari anaonekana Samia ana nguvu zaidi ya Ndugai. Hapa utaona mamlaka ya Samia yanaingia mpaka bungeni, licha ya kuwa mkuu wa serikali.

Hivyo kwa muonekano wa kawaida japo Samia sio serikali, lakini ni mwenyekiti wa chama kinachounda serikali kilichojaza wabunge bungeni ambao Ndugai alikuwa Spika wao, kuwa kinyume nae kunaweza kumgharimu yeyote ndani ya chama chao bila kujali nafasi yake hata kama wakiwa mihimili taofauti, na ndicho kilichomkuta Ndugai.

Matokeo yake, licha ya hoja ya Ndugai bado alishutumiwa toka kila upande, "chawa wa mama" wote waliingia kazini.

Kauli ya NS Tulia jana ndio ikahitimisha hili, kwamba serikali haibanwi na bunge inaweza kuamua nini ichukue na kipi aiache, ajabu Tulia kwa nafasi yake akatukumbusha Rais ndie mkuu wa mihimili ndio maana akamwambia Lukuvi hutagombea uspika!.
Haya mengine, baadae!
 
Back
Top Bottom