Audio: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu, amezungumza na waandishi wa habari leo, Januari 7, 2022

Japo kwa muonekano wa kwenye makaratasi/kisheria hao watu wawili ni binafsi, Ndugai na Samia, na ni wakuu wa mihimili yao, lakini ukienda ndani zaidi utaona yupo mmoja anayeonekana ana nguvu zaidi ya mwingine, na kwasabau ni kiongozi wa mhimili mmojawapo basi mhimili anaouongoza lazima uonekane una nguvu zaidi ya mwingine.

Kwamba Ndugai alimuuliza Samia kuhusu mikopo, ni sawa, na Ndugai sio bunge, Ndugai ni Ndugai. Samia nae akatakiwa kujibu kuhusu mikopo, sababu Samia ni Samia, Samia sio serikali, ni sawa pia, lakini kiuhalisia ukweli wa mambo hauko hivyo.

Lakini badala ya Samia kujibu hoja ya Ndugai, akaishia kumsuta, huku akiwa amezungukwa na wenyeviti wa mikoa wa CCM ambao kimsingi yeye ndie mwenyekiti wao na Ndugai akiwa miongoni mwao.

Kumbuka nguvu ya huyu mwenyekiti inaingia mpaka bungeni sababu anahusika kwa nafasi yake kuwateua wagombea ubunge wa chama chake, hapa tayari anaonekana Samia ana nguvu zaidi ya Ndugai. Hapa utaona mamlaka ya Samia yanaingia mpaka bungeni, licha ya kuwa mkuu wa serikali.

Hivyo kwa muonekano wa kawaida japo Samia sio serikali, lakini ni mwenyekiti wa chama kinachounda serikali kilichojaza wabunge bungeni ambao Ndugai alikuwa Spika wao, kuwa kinyume nae kunaweza kumgharimu yeyote ndani ya chama chao bila kujali nafasi yake hata kama wakiwa mihimili taofauti, na ndicho kilichomkuta Ndugai.

Matokeo yake, licha ya hoja ya Ndugai bado alishutumiwa toka kila upande, "chawa wa mama" wote waliingia kazini.

Kauli ya NS Tulia jana ndio ikahitimisha hili, kwamba serikali haibanwi na bunge inaweza kuamua nini ichukue na kipi aiache, ajabu Tulia kwa nafasi yake akatukumbusha Rais ndie mkuu wa mihimili ndio maana akamwambia Lukuvi hutagombea uspika!.
 
Wanaoamini hivyo ni wale wanaosoma Katiba Nusu Nusu huku wakichanganya madesa, na cha kushangaza wengine ni wanasheria!

Rais atakabaki kuwa Rais popote pale utakapoenda duniani unless kama nchi yenyewe sio jamhuri! Watu wanachanganya madesa linapokuja suala la MIHIMILI...

Of course, Ibara ya 4 (2) inataja MGAWANYO WA MAMLAKA ya UFANYAJI JAMBO na HAISEMI kwamba hawa watu wapo sawa!!
Unaona hapo, watu wanachosema hii mihimili ipo sawa kumbe ni mamlaka ya utendaji!! Kwamba, Serikali ndio YENYE MAMLAKA YA UTENDAJI kwahiyo Samia hawezi kukaa na watu wake wa karibu au peke yake kisha akatunga au kuanzisha sheria mpya na kuisaini kwa sababu chombo chenye mamlaka ya kufanya hivyo ni Bunge!

Hata kama mbunge mmoja anampiga mbunge mwenzake hadi kufa wakiwa bungeni, bado "Ndugai" au bunge hawawezi kutoa hukumu hapo hata kama sheria zenyewe wanatunga wenyewe kwa sababu chombo chanye mamlaka ya utekelezaji wa haki ni Mahakama!!

Mahakama na yenyewe pamoja na kwamba timu yake inaundwa na Wataalamu wa Sheria lakini bado hawawezi kukaa wakatunga sheria mpya kwa sababu chombo chenye mamlaka ni Bunge!

Hapo ndipo ulipo msingi wa mihimili hii matatu ambavyo ARE JUST ORGANS, ambazo according to Ibara ya 4(1) hivyo ni vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza shughuli za nchi! Hata kwenye familia yenu, baba anaweza kusema "wewe" kazi yako wewe ni kukata kuni, mdogo wako kuchota maji, na baba kazi yake kuwasomesha...

...hiyo haitafanya wewe na mdogo wako muwe sawa na baba yenu, na ndo maana Ibara ya 33 (1&2) inasema:-
Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano. Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
Kumbe, pamoja na hivyo vyombo kupewa mamlaka ya kutekeleza shughuli za nchi, Rais ndie MKUU WA NCHI YENYEWE!!

Muhimu ni kwamba, pamoja na yeye kuwa ndie MKUU WA NCHI, lakini linapokuja suala la utekelezaji wa shughuli za nchi kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 4(2) basi anatakiwa kuviachia vyombo husika kutekeleza wajibu wake bila kuwaangilia!!
Kwamba Ndugai alimuuliza Samia kuhusu mikopo, ni sawa, na Ndugai sio bunge, Ndugai ni Ndugai. Samia nae akatakiwa kujibu kuhusu mikopo, sababu Samia ni Samia, Samia sio serikali, ni sawa pia, lakini kiuhalisia ukweli wa mambo hauko hivyo.
Ibara ya 84(1) inasema:-
Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na Wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au wenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge
Kumbe Ndugai alikuwa Kiongozi wa Bunge... nothing less nothing more!!! Hapo kabla nimeshaeleza comfort zone ya WaBunge kama ilivyoelezwa na Ibara ya 100(1) kwamba:
Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.
Kumbe, akishakuwa nje ya bunge, huku akifanya shughuli ambazo sio za bunge basi atabaki tu kuwa Spika au Mbunge lakini mamlaka yake anakuwa ameacha bungeni!!

Kinyume chake, hapo juu umeshaona katiba inasema : " Rais atakuwa MKUU WA NCHI" na sio MKUU WA IKULU au Mkuu wa Serikali peke yake! Kwa maana nyingine, popote Rais anapokuwapo, atabaki kuwa rais kwa cheo na mamlaka!! Popote alipo anaweza kutekeleza kazi zake kwa kutumia mamlaka yake!!

That said, huwezi kusema "Samia alitakiwa kujibu kama Samia"! Lakini that's not an issue! Nimeshasema Ndugai ni Kiongozi wa Chombo ambacho kiliidhinisha serikali ichukue mikopo! Sasa kama kweli alikuwa serious, alitakiwa kwanza kujiuzuru ndipo akaosoe! Tena alitakiwa kujiuzuru soon baada ya bajeti kupitishwa!!

Haya mengine, baadae!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…