Katika maisha unayoyapitia kumbana na shida zote ila sio shida ya umri umeenda ushajichokea afu eti upo mwenyewe yaani upo home alone utajuta!
Mzee wangu aliwahi nambia bora uwe na mke hata kama si mlieanza nae maisha ila usikose mke utakufa siku si zako hata kama kifo ni lazima.
Nikupe mf: alikuwepo mzee 1 pale Sirari aligoma kuoa akiwa kijana na mpaka uzee umemfika kauli yake ilikuwa ni ile ile NITAOA AMBAYE HANYI.
Katika umri kusonga akajikuta amezeeka bila kuoa shughuli kubwa ikabaki ni kuuza miwa, aamke asubuhi awahi shambani atake miwa aipakie kwenye baiskeli aikokote hadi center auze ifike jioni arudi home maisha yakawa ni hayo ikafika kipindi akaonyesha kuchoka mno, kumbe siku za mwishoni akifika home anajilaza ili apumzike kumbe ndo mpaka asubuhi kuna siku analala njaa uwezo wa kuwasha jiko ajipikie ukakosa njaa ndo ilimuua.
Hivi jiulize upo home mwenyewe uugue ghafla hata usiku itakuweje labda simu ikusaidie umpigie mshikaji lakini ujue kuna umri unafika huna washikaji.
Na niwahikikishie maisha ni magumu mno na wanawake ni pasua kichwa sana ila Mungu ana lengo lake kutaka uoe na kuolewa. Kuna vitu hata hela iwepo kama kazi bure.
Mzee Mrema kwa upande wangu yupo sahihi kabisa.
Hawa watoto wa siku hizi ni wajibu tu kuwazaa ila usiwategemee kwa lo lote labda waamue kuwa na wewe ila sio wewe ubweteke ninao watanisaidia.
Katika maisha ambayo umri umeenda ni vizuri kuwa na msaidizi hasa mwenzi wako! Asanteni ni ushauri tu