Aunt Ezekiel: Tununue bongo movie, movie za mbele hazituhusu

Ongezeni basi standards kwenye bongo movie.
Hizi changamoto nyingi zinazoendelea Bongo movie wanajitakia wenyewe, achilia mbali wao wenyewe ndio chanzo cha kuporomoka kwa hizo Bongo movie.

Leo hii hata ukiwaita wakwambie ni wapi wanakwama na nini wasaidiwe hawana hata kauli moja, kila mmoja mjuaji, kila mmoja kiongozi sijui ni miujiza gani wanatarajia.

Kuna bodi ya filamu, baraza la sanaa ambazo hata sijui kazi zao ni nini zaidi ya kusubiri kutangaza 'tumefungia movie tano' wao huwa wapo tu bongo movie ife sawa, ibaki sawa...na wadau hawana hata nguvu ya kuwawajibisha coz wao wenyewe umoja hawana, wapo kila mtu na lwake.
 
Wajitaidi kama wapopo.
 
Mbn wao pia wanabandika mikucha, kope na kuanza miwigi kichwani kwa nn wasiwe kiasili km wanaona vya nje havituhusu?
 
Yaani nipoteze masaa mawili ya maisha yangu, kuangalia Bongo Movie, kweli?
 
Watu wengi wanazipotezea bongo movie kwasababu sio wabunifu wanatengeneza kazi mbovu yaani jambazi anavua viatu kuingia kufanya tukio!
Jaman waoneeni huruma hizi nyumba nyingine wanaomba waigizie sasa wanaogopa kuchafua na viatu [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
yani bongo muvi me naona kumejaa vituko tu. hakuna cha mana story zile zile kila siku.
 
WANAMWITA
-THEODORE
-TEDDY
BAG-MAN
-WOLF
BILA THEODORE PRISON BREAK SI KITU AISEE.

TUSUBIRI UJIO MPYA WA PRISON BREAK NEW SEASON MWEZI WA 6 MWAKA HUU

t- bag naye ndaniii [emoji39] [emoji39]
 
Nisiangalie American Sniper??? Haiwezekani
 
Inawezekana pia, huyo jambazi labada alivua viatu ili kunyata na kupanda madirishani kwa urahisi
 
Hivi Kweli niache kuangalia tamthilia za kifilipino niangalie ujinga wa bongo movie.
Wajipange Sana wasanii wabongo na usanii siwezi poteza faru JOHN kwa kununua CD za kibongo
 
Kama sikosei ni Siri ya mtungi
 
Kama sikosei ni Siri ya mtungi
Yeeees.. Umenikumbusha ndio yenyewe.. Ukiangalia uigizaji. Uongozaji... Sauti.. Mwanga na ubora wa picha.. Hv bongo movie wakifikia walau level hiya why nisinunue kazi zao... Tatizo wamechukulia poa hiyo tasnia.. Kila mtu akinunua kikamera chake cha harusi basi anafungua production company na kuproduce movie zake...
Anakuwa yeye mhusika mkuu.. Yeye mwandishi.. Yeye mwongizaji na yeye ndiye editor.. Na mbaya zaidi aliingia kwenye fani kijanjajanja hajui chochote.. Hapo unategemea movie inakuwaje...
 
A see ile tamthiliya ipo vizuri sana tena sana.
Japo sikufanikiwa kuiangalia mpaka mwisho
Wasipojirekebisha huko mbeleni hii tasnia itakufa kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…