Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 51,453
- 41,274
Asasi za Kiraia hususani zile zilizotajwa na tume ya jaji chande ndie mpangaji, mratibu na mfadhili mkuu wa magaidi na wa matukio yote ya vurugu za Okt 29.2030.
Ndizo zilizotoa mafunzo ya nadharia na vitendo kwa magaidi waliosababisha uharibifu na maafa mabaya sana yaliyotokea nchini kuanzia Oct.29.2025.
AZAKI pia, ndiyo iliyotoa vifaa vilivyotumiwa na magaidi kukata wapiga kura vidole, kupiga picha matukio ya kihalifu waliyokua wakiyafanya, kulipua vituo vya mafuta, makazi ya watu, ofisi za umma na baadhi ya nyumba za ibada maeneo mbalimbali nchini. AZAKI pia ndie mfadhili na msambazaji mkuu wa vyakula na maji kwaajili ya magaidi na majambazi waliokua wakifanya fujo na vurugu maeneo mbalimbali nchini.
Kwa kifupi,
AZAKI haina tofauti na Iran iliyokua ikiwafadhili magaidi wa HAMAS kuleta fujo na maafa ya watu wasio na hatia mashariki ya kati. Kupanic kwao baada ya kuumbuliwa na tume ya jaji chande kunadhihirisha ufedhuli wao waziwazi kabisa kwa dunia nzima.
Napendekeza hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi ya AZAKI zilizoshiriki kikamilifu katika kupanga, kuratibu, kutoa mafunzo, kutekeleza matukio ya kigaidi na hatimae kusababisha uharibifu na vifo vya watoto na wananchi wasio na hatia. Ikithibitika, AZAKI hizo zifutwe mara moja kwa mujibu wa sheria na wahusika kufungwa jela maisha.
Mungu Ibariki Tanzania.