Gentleman,
huo ni mtazamo wako na haki yako ya kutoa maoni,
lakini kamwe haiondoi ukweli kwamba nchi yetu inaongozwa kwa misingi ya kikatiba na sheria na hakuna kitu cha kuiweka misingi hiyo pembeni, bali kuitekeleza kwa maneno na matendo, vinginevyo utawajibishwa kwa mujibu wa sheria utakazokiuka.
AZAKI kupanga, kufadhili na kutekeleza matukio ya kigaidi ni kinyume na katiba lakini pia sheria za nchi yetu.
Lazima sheria ichukue mkondo wake ipasvyo kwenye hili.
Mnawaonea Tu
Hawana hiyo ela ya kufadhiri mapinduzi ya inchi
And I think kama watu wanataka kupindua inchi Kwa kutumia kuhonga watu ela basi inchi ingekuwa imeshapinduliwa,
Maisha ni magumu, hakuna matumaini tena, na viongozi wote wanaishi maisha ya Anasa
Tena anasa za wazi wazi,
Tunakunywa nao bar tunaona, nyumba zao zinajengwa na wabeba zege maskini wanaona na wanasema
Gentleman ongea na viongozi wenzako wa huko kwenye chama na serikali, wawajali watu wa Hali ya chini, maskini, Mambo yote hayo ya kuhisi kupinduana hutayasikia trust me
Tujifunze Kwa serikali ya Zanzibar inavyojali watu wake wa chini
Nenda kaone mwendokasi ya Zanzibar,
Nenda kaone sehemu zilizotengwa za vijana kujipatia pesa,
Nenda kaone masoko yao,
Hakuna soko la tope kama haya ya kwetu
Hakuna mwendokasi mbovu kama za kwetu
Hawezi kumkuta Waziri au mkuu wa mkoa Zanzibar anafanya kufuru ya pesa, na mamlaka, njoo hapa kwetu sasa
Ndio maana Zanzibar kumetulia
Wanasikiliza hoja za watu ambayo wanamtazamo tofauti ndio maana wizara ya utalii IPO chini ya upinzani