Azam anapita njia ngumu CAFCL, atatoka hatua ya awali

Nimecheki game ya coastal aise yani wamecheza utumbo kabisa.

Kwanza hawana stamina wanaangukaanguka hovyo uwanjani .game plan mbovu huoni wakitafuta goli japo kunamuda kipindi cha pili walitulia kidogo wakaanza kutafuta goli ila sasa wakajisahau wakapigwa cha tatu.

Kiufupi hao wameenda kuliaibisha taifa hakuna lolote wao warudi waendelee kumkamia simba tu .
 
Hata Simba na Yanga zilianza hivyo.

Wanatakiwa kujitafuta sana
 
Halafu ile timu waliocheza nayo ni timu ya hovyo tu.
Coastal hawana mbinu za kucheza ugenini kabisa yani.
 
Azam atawapiga APR na Pyramid, zote hazitishi kivile.
 
Azam atakwama Kwa APR huko pyramids ni mbali
Mkuu umekomalia sana Azam kutolewa na APR, sijui kisa Azam kufungwa na Yanga au vipi ndio uwabeze Azam. Azam anapita kwa APR labda iwe APR nyingine tofauti na ile niliyoiona ikicheza na Simba
 
Sasa ili wawe walubwa wanapaswa kuwaomdoa hao wapinzani
 
Mkuu umekomalia sana Azam kutolewa na APR, sijui kisa Azam kufungwa na Yanga au vipi ndio uwabeze Azam. Azam anapita kwa APR labda iwe APR nyingine tofauti na ile niliyoiona ikicheza na Simba
Wewe unachukulia Simba poa
Simba ni team nzuri kuliko Azam
Na Simba wakiifunga APR sio kinyinge na kumbuka Ile ilikuwa bonanza
 
Coastal Union ni kama wamelazimishwa tu kushiriki hayo mashindano.

Wamekivuruga kikosi chao baada ya msimu kumalizika! Mpaka muda huu haijulikani golikipa wao namba moja Ley Matampi alipo!! Hovyo kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…