Daah!! kumbe ushabiki umekujaa, hebu jiondoe kwenye ushabiki kwanza mwanangu narudia " unapomsaini mchezaji unakuwepo mkataba wenye kuonesha mambo mengi tu, mshahara, nyumba, bima, kama ni mchezaji wa kigeni ndio basi tena mtaenda mpaka dakika za kucheza uwanjani nk nk lkn kuna kuwepo kipengere cha kuvunja mkataba, hakuna mkataba usiovunjwa, katika mkataba lazima mweke thamani ya mchezaji na mchezaji mwenyewe aijue mfano mdogo pacome kwa sasa ana bei gani kama timu ikitaka kumchukua unaweza kukuta ni dola laki moja, sasa kama ni hivyo inategemea na msimu mfano sasa hivi dirisha limefungwa hakuna timu inaruhusiwa kuongea na mchezaji ili kuhama kinachofanyika ni timu x inampa mchezaji hiyo hela ya thamani yake + mishahara ya miezi 3 mbele mchezaji analipa club yake anasepa na hutasikia ameenda timu fulani mpaka dirisha la usajili kwa sababu kukwepa rungu la FIFA hiki ndicho kilichotokea kwa fei yaan fei alikuwa na thamani ndogo yaan m 100 sasa azam thamani ya dube ni dola laki 3 kama anayo alipe asepe hapo ndio mtiti 😅 na kama kuna timu nyuma ya pazia inamuhitaji imsaidie dola laki 3 kimya kimya asubiri dirisha ajiunge nao.