Azam FC mtoeni Dube kama mlivyomchukua Fei

Kama mkataba wa Dube ungekuwa hivyo US3000 wakala wake asingekubali Dube atie sahihi. Mkataba kama huo maana yake mchezaji angekuwa analipwa TZS 100,000,000 kila mwezi.
Bongo kwa ujuaji nimewashindwa aiseee 😂😂😂😂
Mkuu hio hapa ni sheria gani umetumia 🤔 release clause ya Vini Jr ni €1B, kwa hio Vin Jr analipwa €333M kwa mwezi ? 🤔😂😂😂😂 Acha kunywa kahawa na wazee kijana watakupotosha 😂😂😂😂
 
soko lao linaruhusu hayo kufanyika (demand and supply, purchasing power, marginal cost, equilibrium, elasticity, etc.). Sisi soko letu ni dogo na linaruhusu busara kutumika kwenye football.
 
soko lao linaruhusu hayo kufanyika (demand and supply, purchasing power, marginal cost, equilibrium, elasticity, etc.). Sisi soko letu ni dogo na linaruhusu busara kutumika kwenye football.
Mzee usitie maneno kwenye pesa,
Hakuna mahali kwenye pesa panapowekwa maneno, mkataba uheshimiwe, pesa itolewe, hizo busara zitatumika wakati wa kusolve matatizo ya michepuko, huku kwingine usilete maneno/busara sehemu ya pesa. Kama huna pesa pita hivi simple as that
 
Azam hawakuwa waungwana walifanya dhuluma kwa Yanga

Sent using Jamii Forums mobile app
Azam wanaiandama Yanga tangu iundwe. Sijui ni kwasababu ya usimba na uyanga au kwasababu wanazo hela?

Tunakumbuka matukio ya Obre Chirwa, Donald Ngoma, Ngassa, Sure boy, Yanick na Juma, Kavumbagu, Fei na pengine Dube. Mara zote wanawaza kuibomoa yanga na sio simba. hakuna mchezaji wanamchukua kutoka Simba ila kuna wachezaji wanaotoka Azam kwenda Simba. Dhambi hii kwa timu yenye wafuasi wengi sana nchini kama yanga lazima itawatafuna wapende wasipende. Kuna vitu huwezi kuvipata kwa pesa zako hata kama unazo nyingi sana. Na Iko siku Yanga itakataa udhamini wa Azam kwa lolote lile huko mbeleni huko kama Azam wakiendelea na mambo ya kitoto wa kuihujumu yanga kama vile simba walivyokataa udhamini wa GSM hata kama TFF ilikubali (presidency) . Nimekaa paleee.
 
Yanga ndio wanawahitaji Azam kuliko Azam wanavyowahitaji Yanga,hivi juzi tumeona wazee wa Yanga wakitangaza kususia bidhaa za Azam,matokeo yake mmeona hata uwanja mnatumia wa Azam
 
Yanga ndio wanawahitaji Azam kuliko Azam wanavyowahitaji Yanga,hivi juzi tumeona wazee wa Yanga wakitangaza kususia bidhaa za Azam,matokeo yake mmeona hata uwanja mnatumia wa Azam
ulikuwa msimamo ambao hakuungwa mkono na uongozi na mashabiki wa Yanga. Mashabiki wakisema bidhaa za Azam ni haram kwao utawafanya nini. akili yako ikutangulie mbele
 
Dube aende cas kamwe hauwezi kusikia msaada kwa mzimbabwe, kiwango chake kikifa hakuna athari kwa taifa letu
 
ulikuwa msimamo ambao hakuungwa mkono na uongozi na mashabiki wa Yanga. Mashabiki wakisema bidhaa za Azam ni haram kwao utawafanya nini. akili yako ikutangulie mbeleK

ulikuwa msimamo ambao hakuungwa mkono na uongozi na mashabiki wa Yanga. Mashabiki wakisema bidhaa za Azam ni haram kwao utawafanya nini. akili yako ikutangulie mbele
Kama mashabiki wa Yanga watasema kuwa bidhaa za Azam ni haramu nina uhakika kuwa JK na mzee Sunday Manara hawatakuwa miongoni mwao.
 
Dube aende cas kamwe hauwezi kusikia msaada kwa mzimbabwe, kiwango chake kikifa hakuna athari kwa taifa letu
Ana miaka 4 Azam bila kupata hata kikombe cha kunywea mbege, hakuna mchezaji mwenye malengo anaependa hivyo, na bahata mbaya viongozi wa Azam wanashabikia Simba na Yanga kwa vitendo na kwa kumaanisha. Wachezaji walioipa Simba mafanikio wengi wamepewa na Azam. Yaani Azam inaipa Simba wachezaji muhimu halafu wao wanabakia na kengele tu. Dube anavuja jasho uwanjani kwa miaka 4 bila kunyanya makwapa, pesa hainunui furaha. Wachezaji wa Azam ni kama vile wamefungiwa kabatini. Wachezaji kama Kipre jr, Akamiko, Yanick au Fei kucheza Azam ni kama wanacheza ndondo, hawaonekani nje ya mipaka (mshikemshike ndege tunduni).
 
Kwani nyie yanga mlisema ni kiasi gani kilipwe ili mkataba uvunjwe?
Fei aliwalipa pesa mliyoisema kwenye mkataba lakini mkazidi kuwa ving'ang'a
 
Kwani nyie yanga mlisema ni kiasi gani kilipwe ili mkataba uvunjwe?
Fei aliwalipa pesa mliyoisema kwenye mkataba lakini mkazidi kuwa ving'ang'a
Mbona Morrison Yanga ilikataa lakini TFF na CAS walimruhusu kuondoka, ilikuwaje washindwe kwa Fei hadi Rais aingilie kati? ina maana kuwa Fei alikiuka mambo kama vile Dube alivyofanya. Shida ya Dube alisaababishwa na Fei toto kuhamishwa kinyume na taratibu na kumfanya Dube nae atembelee mulemule. Kama Dube atashindwa kusaidiwa sawa na alivyosaidiwa TOTO mpira wetu utakumbwa na balaa kubwa. Azam wasisubiri mpaka Rais Samia awapigie simu au awaite Ikulu kuwaambia wanusuru kipaji cha kijana no matter what. Rais kashasema taasisi kubwa kama yanga, Azam na Simba haiwezi kugombana na kitoto kinachotafuta maandazi ya kunyea chai kwa kutumia nguvu na miguu yake. Isitoshe, Rais kasema kuna kodi haikusanyi kutoka kwao kwaajili ya kuendeleza vipaji vya vijana kwenye michezo. Wasisubiri hasira ya Rais, maana ni kama wanataka kumwambia kuwa Rais alikosea kwa Fei.
 
Narudia kipaji cha dube kama taifa kikifa hakuna athari kwetu Rais hawezi kufanya ujinga kuita azam kumsaidia foreigner player wapo wengi ila wa ndani wenye ubora ni wacheche hilo sahau
 
Hizi hazifanani mkuu Yanga waliludisha Azam wao wanataka pesa dube awe huru aondoke Yanga wao walikuwa wanataka mchezaji ila syo pesa huoni ni vitu viwili tofauti ?? Mkuu
 
Narudia kipaji cha dube kama taifa kikifa hakuna athari kwetu Rais hawezi kufanya ujinga kuita azam kumsaidia foreigner player wapo wengi ila wa ndani wenye ubora ni wacheche hilo sahau
Unadhani Rais ni mjinga kama wewe? Unadhani Rais hajui nini maana ya double standard? Unadhani Rais haijui sera yake ya mambo ya nje? Unadhani Rais hajui Zimbabwe ni nchi gani? Unadhani Rais hajui kama kuna ubalozi wa Zimbabwe hapa? Usiwe mjinga Rais wa nchi ni zaidi ya raia wa kawaida. Ndo maana SS hatuupenda Rais aingilie swala la Fei wakati ule kwakuwa tulijua nn kitakwenda kutokea huko mbeleni.
 
Sasa tukubaliane Rais asipoingilia kati wewe ndio mjinga ,na Rais akiingilia kati mimi ndio mjinga,wanaume atuongei sana.
 
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]hakuna kitu kibaya kama kuwa mpumbavu na mjinga,sijui huu upumbavu umerithi kutoka kwa mzazi gani?

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…