Azam Media Kutopeleka Vifaa vya matangazo tarehe 15.06.2025

Azam Media Kutopeleka Vifaa vya matangazo tarehe 15.06.2025

Inasemekana wameandaa barua kuidai fidia bodi ya ligi kwa hasara waliyopata tarehe 8 na endapo bodi itashindwa kulipa fidia ndani ya siku 7 basi mechi namba 184 kati ya Yanga na Simba haitarushwa.
Hatuchezi ng'oo!
 
Kwani lazima ionyeshe? Kwani mechi haiwezi chezwa..na matokeo yakapatikana?...
Halafu hao bodi nini kinawapa uzito kutoa taarifa za uchunguzi? Kuwa mashabiki wa uto walifanya vurugu na video si zipo?? Maana na hata Simba wanazo hizo video walisema watazimwaga kama itabidi...
Then hao Bodi walisema kuna viashiria vya rushwa kama ni rushwa kwanini wasiseme wazi hizo rushwa zilitoka kwa nani kwenda kwa nani..kama alipewa meneja wa uwanja asifungue waseme pia...
Yani natamani hyo ripori waitoe wanashikwa na kigugumizi kipi? Kwny hili na mm nataka watoe ripoti yao watu wabakie uchii....
 
Inawezekana hilo linalosemwa juu lakini nahisi pia yanga watakua wametuma official communication kwa Azam Media kuwa hawatoshiriki mechi na ndio maana Azam media wamerudi nyuma kwenye kuitangaza hii mechi.
Wanapeleka official comm kwa Azam wakati hawajatoa barua yoyote ya kupinga mechi TFF na bodi ya ligi...kuna mtu wa Yanga anasema mechi itachezwa....labda kama watapeleka official letter TFF na Bodi ya ligi then bodi iseme wamepokea na wakatolea maamuzi....
 
Mkataba amepata kwa kupitia tff alafu alete ujinga tena,na kumbuka kuwa Azam anategemea Africa mashariki TU ususani ligi yetu ya kibongo .je dstv wakichukua hii ligi atakula mkaa na masizi.
 
TFF/Bodi ya ligi ni yule mzazi ambae watoto wanampelekesha, kama alishindwa kuchukua hatua Simba alipotangaza kutokupeleka timu uwanjani, Yanga anafanya maksudi aone TFF atafanya nini kwenye jambo lilelile alilofanya mwenzake.
 
Back
Top Bottom