Azam Media wakataa shutuma dhidi ya rushwa ya kurusha vipindi vya tamthilia kutoka kwa wazalishaji binafsi

Azam Media wakataa shutuma dhidi ya rushwa ya kurusha vipindi vya tamthilia kutoka kwa wazalishaji binafsi

Alafu kweli nipo nyuma ya muda Ila ofisi gani haina mkuu wa Idara? Hata Mkurugenzi? Hakuna kiongozi wa Idara husika ambae anawawakilisha wengine yaan Idara ikihitajika wanaenda wote?
Hivi wewe una akili kumzidi Tido Mhando ambaye amekuwa Mkurugenzi wa BBC Swahili Bush London kwa miongo kadhaa?

Hebu tuanzie hapo kwanza.
 
Hivi wewe una akili kumzidi Tido Mhando ambaye amekuwa Mkurugenzi wa BBC Swahili Bush London kwa miongo kadhaa?

Hebu tuanzie hapo kwanza.
Ninaweza nikawa nina akili mingi sana kumzidi hata yeye you never know alafu unasema as if unanijua personally, any ways ni maamuzi yao kufanya wanachojisikia tusiwapangie wao ndio wanajua wanachofanya all in all ujumbe umefika
 
Hivi wewe una akili kumzidi Tido Mhando ambaye amekuwa Mkurugenzi wa BBC Swahili Bush London kwa miongo kadhaa?

Hebu tuanzie hapo kwanza.
Jamaa ana hoja ya msingi mjibu hoja yake achana na kufananisha akili za watu
Anachosema hapo ni kwamba kuna uwezekano mkubwa hiyo barua ni feki na kama siyo feki kuna na shida mahali kwenye hilo shirika ama kampuni si sawa kuandika barua kienyeji hivyo

Alafu jua kwamba wewe kuwa tido muhando haikuhakikishii kwamba una akili sana kuliko Makonda wote wa daladala Tanzania

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Wakanushe pia kuwa wanatuibia kwa kurudia rudia movie ktupitia cha
TAARIFA KWA UMMA

Kampuni ya Azam Media Ltd, imebaini vipande vya picha jongefu vinavyosambaa kupitia mitandao ya kijamii vikimuonesha mwigizaji na mtengeneza filamu, Deogratius Shija, akiwatuhunu baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yetu kwa vitendo vya rushwa.

Kampuni yetu inamuarifu Shija na umma kwa ujumla kuwa, haivumilii vitendo vya rushwa, udanganyifu na mbinu zozote chafu katika kusaili maudhui kwa ajili ya kuonyeshwa katika chaneli zetu, kadhalika hatupendezwi na tabia ya watengeneza maudhui kutunga shutuma dhidi ya watendaji wetu kwa sababu tu kazi zao hazikupitia kwenye chujio la kupima ubora.

Kwasababu hizo, tunatoa muda wa wiki mbili kwa Deogratias Shija, kuwasilisha ushahidi au vielelezo kuhusu tuhuma alizozitoa kwa Mkurugenzi Mtendaji au kwenye mamlaka za kisheria, TAKUKURU, Film Board, au Jeshi la Polisi, ili kuwezesha hatua stahiki zichukuliwe kwa watuhumiwa wote wanaodaiwa kuihujumu kampuni kwa vitendo vyote kinyume na taratibu za kazi.

Kampuni yetu ina utaratibu maalum wa ndani, ulio wazi na shirikishi katika manunuzi ya filamu na maudhui mengine kutoka kwa wazalishaji binafsi.

Azam Media Ltd inatumia fursa hii kuwaomba wadau wa filamu nchini kufuata njia sahihi zinazokubalika kisheria ikiwemo kutoa taarifa kwa Mkurugenzi Mtendaji, Bodi ya Filamu, Polisi au TAKUKURU pale wanapokuwa na ushahidi wa madai yao badala ya kutumia njia ambazo zinaweza kuleta taharuki na taswira mbaya kwa jamii ndani na nje ya Tanzania.

Imetolewa na Idara ya Mawasiliano kwa Umma

1.12.2023.

Habari wana jamvi, kumekuwa na taarifa za chini kwa chini baada ya kuibuka sakata la wasimamizi wa televisheni kule Dstv sasa imehamia Azam nao wamejibu mapigo.

Note; ukimshtumu mtu au kampuni hakikisha hiyo kesi una ushahidi nayo la sivyo inakugeukia, kesi kama hizi ikikugeukia utalipwa faini moja mbaya ambayo itakugharimu.

Pia soma:

Video iliyosambaa mitandao ya kijamii Deogratius Shija akimtuhumu Wasiwasi Mwabulambo kwa kupokea rushwa

Wakanushe pia kwamba hawatuibii kwa kurudia rudia movie kupita Chanel zao za MBC pamoja na kwamba wametupandishia gharama!
 
Jamaa ana hoja ya msingi mjibu hoja yake achana na kufananisha akili za watu
Anachosema hapo ni kwamba kuna uwezekano mkubwa hiyo barua ni feki na kama siyo feki kuna na shida mahali kwenye hilo shirika ama kampuni si sawa kuandika barua kienyeji hivyo

Alafu jua kwamba wewe kuwa tido muhando haikuhakikishii kwamba una akili sana kuliko Makonda wote wa daladala Tanzania

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Ni Tido na siyo tido.

Ni Mhando na siyo Muhando.

IQ test huwa inaanza na vitu vidogo tu.

Asante.
 
Jamaa mwenyewe ndo huyu kila movie lazima asafiri aende ulaya masomoni, alafu anarudi anaendesha corolla anakuta demu wake anamimba na anakataa kumsamehe
Deogratius_Shija.jpg
 
Maana yake baada ya siku 14 shija kama hatowasilisha ushahidi basi Azam media watamshitaki na kufungua case ya madai!
Shija kazi anayo….
 
Ni Tido na siyo tido.

Ni Mhando na siyo Muhando.

IQ test huwa inaanza na vitu vidogo tu.

Asante.
Sina hakika kama nimejipambanua kuwa nina IQ kiasi gani lakini inawezekana wewe ni mtaalamu wa kuandika

Kila mtu anaweza akaimba
kila mtu anaweza akacheza mpira
Lakini kuna watu wenye hizo fani
Ukilifahamu hilo basi huwezi kuwa mwalimu wa masahihisho humu ndani

Wenye akili hujibu hoja na siyo kutafuta vimakosa vya ajabu visivyo na msingi

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Wakanushe pia kuwa wanatuibia kwa kurudia rudia movie ktupitia cha

Wakanushe pia kwamba hawatuibii kwa kurudia rudia movie kupita Chanel zao za MBC pamoja na kwamba wametupandishia gharama!
Hapo sio wizi mkuu
 
Barua gani haina saini haina muhuri hata wa kielectronic tutaamini vipi km ni kweli barua ya Azam sio kwamba kuna mjuba kakaa tu kaiandaa huko uchochoroni yaan Idara haina hata Mkuu wa Idara husika ambae anaiwakilisha Idara husika akatia saini akagonga muhuri au Mimi ndio nipo nyuma ya muda?
Ingia Kwenye website Yao na kurasa zao za mitandao ya kijamii
 
Hiyo barua umekaa kimchongo.. haijakidhi matakwa ya kisheria,. Barua gani haina saini...
 
Aloo sema kama nimemuelewa jamaa ivi, laki nane zimepigwa na bado kapigwa chini 😀 kuna watu wakaksii
 
Barua gani haina saini haina muhuri hata wa kielectronic tutaamini vipi km ni kweli barua ya Azam sio kwamba kuna mjuba kakaa tu kaiandaa huko uchochoroni yaan Idara haina hata Mkuu wa Idara husika ambae anaiwakilisha Idara husika akatia saini akagonga muhuri au Mimi ndio nipo nyuma ya muda?
Tunaamini ni official letter kwasababu imepostia na social account za Azam media sijaitoa popote tu mkuu
 
Back
Top Bottom