Tatizo litakuwa kwa hao watendaji wachache wasio na maadili na si Azam nzima kama taasisi, anyway, akathibitishe kwanza hizo tuhuma zake lasivyo ajiandae kupambana na mkono wa sheria.Ikiwa proved basi AZAM TV ina tatizo kubwa sana sana
Hivi wewe una akili kumzidi Tido Mhando ambaye amekuwa Mkurugenzi wa BBC Swahili Bush London kwa miongo kadhaa?Alafu kweli nipo nyuma ya muda Ila ofisi gani haina mkuu wa Idara? Hata Mkurugenzi? Hakuna kiongozi wa Idara husika ambae anawawakilisha wengine yaan Idara ikihitajika wanaenda wote?
Azam haikuwa sehemu ya taarifa zangu, ngoja tuone watafikia wapi.
Ninaweza nikawa nina akili mingi sana kumzidi hata yeye you never know alafu unasema as if unanijua personally, any ways ni maamuzi yao kufanya wanachojisikia tusiwapangie wao ndio wanajua wanachofanya all in all ujumbe umefikaHivi wewe una akili kumzidi Tido Mhando ambaye amekuwa Mkurugenzi wa BBC Swahili Bush London kwa miongo kadhaa?
Hebu tuanzie hapo kwanza.
Jamaa ana hoja ya msingi mjibu hoja yake achana na kufananisha akili za watuHivi wewe una akili kumzidi Tido Mhando ambaye amekuwa Mkurugenzi wa BBC Swahili Bush London kwa miongo kadhaa?
Hebu tuanzie hapo kwanza.
TAARIFA KWA UMMA
Kampuni ya Azam Media Ltd, imebaini vipande vya picha jongefu vinavyosambaa kupitia mitandao ya kijamii vikimuonesha mwigizaji na mtengeneza filamu, Deogratius Shija, akiwatuhunu baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yetu kwa vitendo vya rushwa.
Kampuni yetu inamuarifu Shija na umma kwa ujumla kuwa, haivumilii vitendo vya rushwa, udanganyifu na mbinu zozote chafu katika kusaili maudhui kwa ajili ya kuonyeshwa katika chaneli zetu, kadhalika hatupendezwi na tabia ya watengeneza maudhui kutunga shutuma dhidi ya watendaji wetu kwa sababu tu kazi zao hazikupitia kwenye chujio la kupima ubora.
Kwasababu hizo, tunatoa muda wa wiki mbili kwa Deogratias Shija, kuwasilisha ushahidi au vielelezo kuhusu tuhuma alizozitoa kwa Mkurugenzi Mtendaji au kwenye mamlaka za kisheria, TAKUKURU, Film Board, au Jeshi la Polisi, ili kuwezesha hatua stahiki zichukuliwe kwa watuhumiwa wote wanaodaiwa kuihujumu kampuni kwa vitendo vyote kinyume na taratibu za kazi.
Kampuni yetu ina utaratibu maalum wa ndani, ulio wazi na shirikishi katika manunuzi ya filamu na maudhui mengine kutoka kwa wazalishaji binafsi.
Azam Media Ltd inatumia fursa hii kuwaomba wadau wa filamu nchini kufuata njia sahihi zinazokubalika kisheria ikiwemo kutoa taarifa kwa Mkurugenzi Mtendaji, Bodi ya Filamu, Polisi au TAKUKURU pale wanapokuwa na ushahidi wa madai yao badala ya kutumia njia ambazo zinaweza kuleta taharuki na taswira mbaya kwa jamii ndani na nje ya Tanzania.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano kwa Umma
1.12.2023.
Wakanushe pia kwamba hawatuibii kwa kurudia rudia movie kupita Chanel zao za MBC pamoja na kwamba wametupandishia gharama!Habari wana jamvi, kumekuwa na taarifa za chini kwa chini baada ya kuibuka sakata la wasimamizi wa televisheni kule Dstv sasa imehamia Azam nao wamejibu mapigo.
Note; ukimshtumu mtu au kampuni hakikisha hiyo kesi una ushahidi nayo la sivyo inakugeukia, kesi kama hizi ikikugeukia utalipwa faini moja mbaya ambayo itakugharimu.
Pia soma:
Video iliyosambaa mitandao ya kijamii Deogratius Shija akimtuhumu Wasiwasi Mwabulambo kwa kupokea rushwa
Ni Tido na siyo tido.Jamaa ana hoja ya msingi mjibu hoja yake achana na kufananisha akili za watu
Anachosema hapo ni kwamba kuna uwezekano mkubwa hiyo barua ni feki na kama siyo feki kuna na shida mahali kwenye hilo shirika ama kampuni si sawa kuandika barua kienyeji hivyo
Alafu jua kwamba wewe kuwa tido muhando haikuhakikishii kwamba una akili sana kuliko Makonda wote wa daladala Tanzania
Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Wamekataa soma vizuri ..ila wanataka ushahidi ila wamekataa na kuwatetea wafanyakazi wao na chombo! Shija apeleke ushahidi kinyume na hapo cas ya kuchafua watu au taasisi ina muhusuUnasoma halafu unatafsiri kivyako, mbona hawajakataa ila wanahitaji ushahidi.
Sina hakika kama nimejipambanua kuwa nina IQ kiasi gani lakini inawezekana wewe ni mtaalamu wa kuandikaNi Tido na siyo tido.
Ni Mhando na siyo Muhando.
IQ test huwa inaanza na vitu vidogo tu.
Asante.
Ingia Kwenye website Yao na kurasa zao za mitandao ya kijamiiBarua gani haina saini haina muhuri hata wa kielectronic tutaamini vipi km ni kweli barua ya Azam sio kwamba kuna mjuba kakaa tu kaiandaa huko uchochoroni yaan Idara haina hata Mkuu wa Idara husika ambae anaiwakilisha Idara husika akatia saini akagonga muhuri au Mimi ndio nipo nyuma ya muda?
Tunaamini ni official letter kwasababu imepostia na social account za Azam media sijaitoa popote tu mkuuBarua gani haina saini haina muhuri hata wa kielectronic tutaamini vipi km ni kweli barua ya Azam sio kwamba kuna mjuba kakaa tu kaiandaa huko uchochoroni yaan Idara haina hata Mkuu wa Idara husika ambae anaiwakilisha Idara husika akatia saini akagonga muhuri au Mimi ndio nipo nyuma ya muda?