AZAM na Baraka Mpenja punguzeni mahaba kwa Yanga, kuweni professionals

Ameteleza tu kuandika,ana stress za pira papatupapatu
 
Unaumia ukiwa wapi kolo?
Mbona Utakunya jabali mwaka huu
 
Azam wanaonyesha mpira kwa mazoea, hata mechi ya juzi ya yanga badala ya kuonyesha mpira wanaonyesha watu jukwaani ile kurudi mpira unaingia golini hata moves hazikuonyeshwa.
Kuhusu watangazaji wengi hawana maadili ya kazi, mechi iwe ya yanga au Simba inapoonyeshwa kwanini ulinganishe matukio na upande was pili.
 
Mpenja anaanglia $$$$$$$$$$$,❤️❤️❤️❤️❤️❤️ Kwa timu baadae

Hata nyie mkimpa Hela atawarembaremba
Tukiacha lawama Kwa Mpenja,lile pira unalionaje mkuu?

Mpira ni mchezo wa wazi. Hauhitaji kelele na manjonjo ya mtangazaji utadhani anamtoa mwali ili watazamaji wajue timu fulani inapiga mpira mwingi. Kama mtangazaji pro na anayejitambua lazima utambue si kila anayetazama hiyo game ni mpenzi wa hiyo timu unayoipamba kwa hiyo lazima ubalance shobo.
 
Jibu swali,pira lile unalionaje!?
 
Hilo la kuonyesha mashabiki nalo nimeliona sana tu. Uswahili umeingia sana pale wanasahau hata jinsi ya kufanya kazi. Usiniambie hawajafundishwa au hawaoni mpira wa nje kujua ni wakati gani ni sahihi kurudia tukio la nyuma au kuonyesha mashabiki.
 
Uliposema watangazaji wapo kwemye payroll ya Yanga, ulitaka na Simba wafanye hivyo.
Ndio maana nikakuambia kesho utakuja utasema pia na waamuzi wanalipwa na Yanga
Sasa wewe kesho yangu unaijuaje? Na hilo la kusema nataka Simba wafanya hivyo hayo ni mawazo yako maana kama ningeona ni jambo sahihi nisingekuja kulikemea. Ninachotaka ni viongozi wasiifanye Simba iishi kinyonge. Nataka Simba ambayo ikifanyiwa uhuni na yenyewe iwe tayari kufanya uhuni ili heshima iwepo mjini. Uliona ishu ya Ngoma walivyonyong'onyea?
 
Unapingana na ulichokosema mwenyewe sasa.
 
Unampangia mshehereshaji kusheheresha wenye shughuli yao?, Kama Simba inacheza pira papatupapatu asiseme?. Hata hivyo mtamgazaji kuna mahali aliitaja Simba?, mashabiki wasimba mnaongoza kuwa na nyuzi za kisengelema Sana humu... Hebu punguzeni ujuha nyambafu nyie.
 
Upo kihisia zaidi na sio uhalisia. Simba haipo vizuri kiutawala japo wana structure nzuri kuliko yanga. Uzuri wa Engineer kiutendaji na uaminifu umetukuka mno ukifananisha na wahuni wa pale Simba.
Kuna mambo ya kuweka sawa kwenye uongozi na ufuatiliaji wa mambo nadhani hilo nimeligusia pia
 
Nikazi ya comentantor kufurahisha upande uliofurahi.

Hata wakati Simba anafanya vizuri uwanjani nimeshuhudia mara nyingi Mpenja akituma madongo kwa Yanga.
Naomba nikutoe rasmi kwenye list ya vijana wa Rage kwa muda ,hata Simba day mwaka huu alipiga dingo kwa Yanga na sio mechi moja anafanya hivyo.
 
Kwa sababu mpira una pande mbili.
 
Nilikuwa sehemu fulani nafuatilia kanfanda mubashara , ghafla nikamsikia Mpenja akianza kumtofautisha yule Malila na Umalila ghafla nikaona banda lote watu shangwe huku hakuna goli wala kitu cha kuwafanya wafurahi .

Kumbe bwana ndugu zake Mpenja walifurahia kusikia ndugu yao anawataja mara mwamba wa umalila , mara Fahari ya Itete basi banda likaw ni full kuongea kimalila .

Popote ulipo Baraka Mpenja napenda kukuambia kuwa ndugu zako Umalila wanakupenda sana ila jitahidi kudeal na kazi yako punguza mahaba na maelezo mengi kama watafsiri muvi za kivita kama Mkandala lufufu .

.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Simba mtaumia sana na Yanga
 
Haya mateso unayapitia ukiwa wapi ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…