AZAM na Baraka Mpenja punguzeni mahaba kwa Yanga, kuweni professionals

Ameongea UKWELI [emoji1787]
 
Mechi ipi Yanga amecheza halafu dstv wamefanya production.?
Mkuu ulikuwa unafatilia kweli mechi za kimataifa za yanga au ulikuwa unaulizia matokeo, mbona mechi nyingi sana dstv kafanya production, au hata fainal hukuangalia kutokana na wivu wako juu ya yanga?. Muda mwingine tuwe tunabishana kwa hoja mkuu siyo kelele za vijiweni
 
Kuna utofauti kati ya kufanya production na kuonyesha, dstv kuonyesha haina maana kwamba yeye ndie kafanya production. Mechi zote za yanga, simba na wengineo walizocheza hapa nchini production imefanywa na azam hadi hy fainali, mechi za yanga, simba na wengineo nje ya nchi zimefanywa na kampuni tofauti kabisa ila sio dstv. Kinachofanyika ni dstv anapewa clear feed tuu ndipo anaonyesha. Tafuta mtu anayefanya kazi kwenye tv atakupa hy elimu.
 
Nimekupata mkuu
 
Hivi TFF wanakamati ya kuhakiki ubora wa matangazo ya Azam kweli?

Kama hawana nawashauri waiunde haraka sana na kila wiki wawe wanatoa ripot iwekwe wazi ili tujue wanashauri nini.

Ubora wa matangazo ya Azam ni hovyo sana. Miaka inaenda lkn hawataki kujirekebisha.

Azam wakiweza hilo watauza sana visimbuzi vyao.
 
Wazo zuri. Kuna maboresho mengi yanaweza kufanyika mbali na haya. Mfano, huwa nashangaa kwa nini mechi ikiisha hawafanyi marudio ya magoli yote ya mechi hiyo kabla ya kurudi studio au kuanza mahojiano pale uwanjani. Nadhani hii ni standard inayotumika na media zingine za nje zinazotangaza mpira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…