Azam Pesa: Huduma mpya ya kifedha

Huduma nzuri Ila ilitakiwa ifanyiwe mabiresho ya kutosha ikiwezekana inauzwa dukani kwa kuskitratch kama vocha

Bakhresa yuko serious sana na kazi sio kama akina fulani kazi kumfuatila zeruzeru wa kariakoo
 
Du ila Bakhresa anajua kukaba,anakaba kila kona, ukija kwenye ubuyu yupo ,kwenye lambalamba ndio usiseme na sasa hadi kwenye pesa kiganjani.
 
Pia unaweza kutuma pesa kwenda mtandao washindani????......mfano kutuma pesa kutoka azampesa kwenda Tigo pesa au airtel money

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Kwa sasa ambapo huduma ndiyo imeanza, uwezo wa kutuma pesa kwenda mitandao washindani bado.

Ila kwa siku chache zijazo, uwezekano wa kutuma utakuwepo.
 
SSB kabutua hapa ,wamemuingiza chaka watu wa commercial..Azampesa ishafeli kabla ya kuanza....Bakresha kashanunua license TCRA ya mawasiliano kwanini asianzishe kampuni yake ya simu?
 
Ifike pahala serikali iwabane hawa matajiri wafanye biashara kubwa zina tija zaidi kuliko kuwaachia waue vibiashara vidogo vya wananchi wa hali ya chini.

Unataka kutuambia Airtel money, Zpesa, Tigo pesa, Halopesa na M-pesa ni watu wa hali ya chini?

Mcmpangie hela zake, hela anazo za kutosha, hata akianzisha biashara ya kuuza dagaa ni yeye mzee.
 
Isije ikawa kama wale wananunua toyota corrola halafu anaweka chata ya benz. Azam pesa ndani ya Tigopesa.

Tigo, Voda, Artel, Halotel ni washindani wenu au washirika? Anyways, wamiliki wa Azam wana akili ya biashara ngoja tuone.
 
Ninavyoijua mitandao ya simu wakiona anafanya biashara sana tena kupitia laini zao, watalemaza hiyo menu iwe ngumu ku-access. Utakuta katika attemt 5 inafanikiwa moja.

Kama amedhamiria aanzishe mtandao wa simu kabisa tuwe tunanunua na vifurushi kabisa na kujiunga intaneti na kuwapigia wake zetu kwa azam.
 
Unataka kutuambia Airtel money, Zpesa, Tigo pesa, Halopesa na M-pesa ni watu wa hali ya chini?

Mcmpangie hela zake, hela anazo za kutosha, hata akianzisha biashara ya kuuza dagaa ni yeye mzee.
Usipanick fikiria kwa taratibu utaelewa nilichomaanisha.
 
Elimu bado inahitajika tuijue kwanza hiyo azam pesa.
Na sijaona matangazo yake mkuu, imekaaje hiyo mnaitangaza vipi huenda ikaeleweka zaidi kupitia matangazo.
 

wakati huo huo wajue kabisa dstv ni 59000tsh complete set na kuna kifurushi cha 9000tsh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…