rich1
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 3,020
- 3,309
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Du ila Bakhresa anajua kukaba,anakaba kila kona, ukija kwenye ubuyu yupo ,kwenye lambalamba ndio usiseme na sasa hadi kwenye pesa kiganjani.Kampuni kubwa na iliyoenea katika nchi ya Tanzania pamoja na nchi jirani 'Bakhresa Group' imeleta sokoni huduma mpya ya kifedha ijulikanayo kama 'Azam Pesa'.
Huduma hii ni kama zilivyo huduma nyinginezo za M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa and the like.
Ili kuielewa zaidi huduma hii, nitaenda katika mtindo wa Maswali na kisha majibu.
Je, Azam wameanzisha mtandao wao wa simu?
Hapana. Azam bado hawajaanzisha mtandao wao kama zilivyo kampuni kadhaa za mawasiliano hapa nchini.
Bali AzamPesa wameingia makubaliano na baadhi ya mitandao kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa huduma kupitia line za mitandao hiyo.
Mpaka sasa AzamPesa wameshakubaliana na Tigo, Airtel na Zantel. Hivyo huduma hii inapatikana katika line za mitandao tajwa.
Vodacom, Halotel na mitandao mingine bado wapo kwenye mazungumzo. Watakapokubaliana basi huduma hii itawezeshwa katika line hizo.
Je, huduma hi inahusika
na nini?
Kama ilivyo huduma zingine, huduma hii inahusika na;
1.Kutuma Pesa
2.Kutoa Pesa
3.Kulipia bili
4.Kulipia bidhaa za Azam
Je, huduma hii imeanza kufanya kazi?
Ndiyo, huduma hii imeshaanza kufanya kazi kwa wateja wote waliosajiliwa.
Je, najiungaje na huduma hii?
Fika katika duka la wakala na uweze kusajiliwa. Kinachohitajika ni namba yako ya simu pamoja na namba yako ya NIDA. Ndani ya dakika mbili tayari utakuwa umeshasajiliwa kuwa mteja wa AzamPesa.
Je, huduma naweza kupata vifurushi 'bundles' maalum vya Azam?
Hapana. Kama ambavyo nilijwishaeleza hapo juu kwamba Azam bado hawajaanzisha mtandao wao hivyo swala la vifurushi linabakia kuwa maamuzi ya mtandao husika.
Je, huduma hii naipata wapi?
Huduma hii inapatikana katika mikoa yote Tanzania. Ijapokuwa bado haijatapakaa kila mahali lakini upatikanaji wake katika maeneo mengi ya miji ni uhakika.
Je, menu 'ussd' ya AzamPesa ni ngapi?
Baada ya kusajiliwa, utabadili namba ya siri. Hivyo utabonyeza *150*08# na kuweza kupata huduma ya AzamPesa.
Kama una swali lolote kuhusiana na huduma za AzamPesa, basi karibu.
Wasalaam.
Kwa sasa ambapo huduma ndiyo imeanza, uwezo wa kutuma pesa kwenda mitandao washindani bado.Pia unaweza kutuma pesa kwenda mtandao washindani????......mfano kutuma pesa kutoka azampesa kwenda Tigo pesa au airtel money
Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Huduma hiyo kwa sasa bado. Ila ni mategemeo yetu itawezeshwa siku za mbeleni bila riba yeyote.Je , huduma ya kusongesha mihamala inapatikana kwenye Azampesa maana wengine hiyo ndio mkombozi wetu
Ifike pahala serikali iwabane hawa matajiri wafanye biashara kubwa zina tija zaidi kuliko kuwaachia waue vibiashara vidogo vya wananchi wa hali ya chini.
Usipanick fikiria kwa taratibu utaelewa nilichomaanisha.Unataka kutuambia Airtel money, Zpesa, Tigo pesa, Halopesa na M-pesa ni watu wa hali ya chini?
Mcmpangie hela zake, hela anazo za kutosha, hata akianzisha biashara ya kuuza dagaa ni yeye mzee.
Usipanick fikiria kwa taratibu utaelewa nilichomaanisha.
Jicho la mwewe! Hii inalenga kwenye kulipia vifurushi katika ving'amuzi vyao;
1.kutakuwa na punguzo kwa wale watakaotumia Azampesa.
2 Kwa Wateja ambao hawatatumia Azampesa watakuwa wanachewa kupata Huduma baada ya kulipia hivyo itawalazimu kujiunga Azampesa. Muda ni hakumu wa kweli.
Noted.Elimu bado inahitajika tuijue kwanza hiyo azam pesa.
Na sijaona matangazo yake mkuu, imekaaje hiyo mnaitangaza vipi huenda ikaeleweka zaidi kupitia matangazo.