Azam TV badilisheni Tamthilia zenye mlengo wa itikadi za kidini

Azam TV badilisheni Tamthilia zenye mlengo wa itikadi za kidini

movies and siries ni sialaha za kijasusi wa kiuchumi,mtindo na kiutawala... tv pia ni silaha kichwa kikishindwa kudadavua yanayoonekana kwa macho..balaa litakukuta kama hili..
 
Mkwawa punguza makasiriko angalia tv ya Mwamposya au Jehovah Jire mchana na usiku kucha nani anakuzuia wewe mshamba?👹
 
Ikifika saa nne weka Azam One huko kuna series za marekani hii itakusaidia kuepuka maudhui ya Azam Two, mwanzoni nilikuwa naangalia hizo tamthilia ila nilikuja kuacha baada ya kuona story zake zinafanana tu, nikahamia Azam one huko ni moto sasa hivi inaisha Godfather of Harlem then ianze Snowfall.
 
Sasa mkuu unafanya kazi saa zote? Mind relaxation jambo mhimu..au ishu ni tamthliya lakini kurelqx kivingine sawa?
Hawa watu Wana maisha magumu sana maana kila kitu kwao ni complicated hawajui hata hizi tamthilia ni mafunzo ya maisha halisi
 
movies and siries ni sialaha za kijasusi wa kiuchumi,mtindo na kiutawala... tv pia ni silaha kichwa kikishindwa kudadavua yanayoonekana kwa macho..balaa litakukuta kama hili..
Na ukiwa timamu ndo utaliona hili
Na watu hapa wanakuja na majibu mepesi eti " badilisha chanel" yaani kama kitu cha kawaida hawaoni chuki inayopandwa ndani ya jamii hapa waislamu watajiona superior kuliko wakristu

Hizi tamthilia na filamu zina impact ya hali ya juu ya kubadili mtazamo wa watu
 
Mkwawa punguza makasiriko angalia tv ya Mwamposya au Jehovah Jire mchana na usiku kucha nani anakuzuia wewe mshamba?👹
Mwamposa ile iko mahususi kwa ajili ya kazi zake na hiyo Jehovah jire ni taaisi ya kidini ila Azam two ni universal hivyo ninachokisema kina maana
 
Ikifika saa nne weka Azam One huko kuna series za marekani hii itakusaidia kuepuka maudhui ya Azam Two, mwanzoni nilikuwa naangalia hizo tamthilia ila nilikuja kuacha baada ya kuona story zake zinafanana tu, nikahamia Azam one huko ni moto sasa hivi inaisha Godfather of Harlem then ianze Snowfall.
Haijalishi ni Mimi au nani anayepaswa kuangalia ninachokiangazia hapa ni usawa katika jamii uwiano wa maudhui na kutoa hisia kandamizi dhidi ya kundi fulani
 
mkuu sasa si ndio filamu, ulisahau Rambo na arnod walipiga kambi nzima?mbona hulalamiki hilo
Sijawahi kuziona hizo tamthilia unazozisemea Mimi naongelea nilichokiona
 
Nina mwaka wa 5 nshakitupa hiki kijamaa sababu ya hizo tamthilia zao, nliona watoto wanachokijenga kichwan mwao sitoweza kuki control vichwani mwao siku za usoni
Jana nimerudi nimechoka nikafikia kujitupa tu kwenye kiti hakukuwa na mtu sebuleni ila TV ilikuwa inaonesha chaneli ya Azam 2

Macho yangu yakaona kipande kimoja kwenye tamthilia ya kituruki bila shaka inaitwa Alpasalani nadhani, Sasa Kuna Binti alikuwa Yuko kwenye mtego na viongozi wa utawala mwingine inaonesha huo utawala una Ukristu maana askari wake wana misalaba kwenye mavazi yao.

Sasa hawa askari aisee ni midebwedo vibaya mno yaani mwanamke moja anaua infidels (humo wanaita wadhalimu) zaidi ya 20 mbele ya kiongozi wao halafu Yuko pekeake na bado anaendelea kusurvive!? Duuuh ina maana hao ni wanyonge kiasi hiko? Halafu mule inaonesha waislamu ni watu wema sana na wakristu ni watu wenye Roho mbaya mno na hii chanel secular ila inabagua Imani moja na kuipendelea ingine.

Ututuki ni nchi ambayo raia wake wengi ni waislamu hivyo ni sawa kuwa na maudhui kama Yale, Sasa Tanzania hii ni multi religion county huwezi kuwa na maudhui hayo hayo tu kila siku ya kukandamiza Imani moja na kuipendelea ingine kulikuwa na;
  • Ertugrul
  • Ottoman
  • Barbarossa na Sasa ni hii
  • Alpasalani
Zote hizi maudhui ni yaleyale.

Azam tv badilikeni, hela tunalipa sisi lakini mnatutibua nyingi makusudi kabisa.

Na huu mwezi nitaacha kulipia hiki kisimbuzi kama ni ligi kuu nitaangalia bandani na kisimbuzi nitanunua cha startimes.

Azam tv mjifunze kwa wenzenu, mbona wao wanajua mipaka yao.

Mnakera bwana aah!
 
Back
Top Bottom