Azam TV jitokezeeni hadharani Muwaombe radhi viongozi wa Yanga Sc, mashabiki na wadau wa mpira kwa interview ya Fiston Mayele mliyoiyoifuta

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Kituo cha Habari cha Azam TV kimefuta mahojiano waliyofanya na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele katika kurasa zake zote za mitandao ya kijamii baada ya klabu ya Yanga kuripotiwa kuitaka Azam TV kufanya hivyo.

Mahojiano hayo yaliyonukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini yalijikita katika kuichafua klabu ya Yanga pamoja na mpira wa Tanzania kiujumla na kuzua mjadala mkubwa miongoni mwa wafuasi wa soka.

Azam Media wanapaswa kujitokeza hadharani na kuomba Radhi kwa upuuzi walioufanya kwani wamechafua taasisi na tasnia ya mpira wetu huu kwa ujumla.

Ukisikiliza interview ya Fiston kalala Mayele imejaa kashifa ya udhalilishaji wa viongozi pamoja na ligi yetu kwa jumla lakini Azam media bila kujali/kuchuja wameipost.

Maoni Yangu: Endapo Azam media wasipoomba Radhi mashabiki wa Yanga na viongozi pamoja na wadau wa mpira basi itafahamika kuwa Azam media watakua wametumika kuichafua Yanga Sc na mpira wetu kwa ujumla.
 
Kama mahojiano hayavunji sheria zozote za nchi hakuna sababu ya kuyafuta.
Azam ni chombo cha habari, kazi yake ni kuripoti tu. Maoni ya Mayele ni ya kwake, asipoyatoa kupitia Azam media anaweza kuyatoa kupitia chombo kingine chochote cha habari. Sio jukumu la Azam media kurusha habari zenye kuwafurahisha tu Yanga, hata za kuwakera zinapaswa kuruka hewani.
 
Kwahy na ww tena unaniuliza swali.?
Kwenye kufuta kuna mambo mengi ndani yake ila sio kwamba kilichoongelewa n uongo, na ht kama ni uongo bc huo uongo n kutoka kwa mayele na sio Azam. Yanga waache kuwafanyia unyama wachezaji wao.
Wachezaji gani waliofanyiwa UNYAMA !?
 
Kituo cha Habari cha Azam TV kimefuta mahojiano waliyofanya na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele katika kurasa zake zote za mitandao ya kijamii baada ya klabu ya Yanga kuripotiwa kuitaka Azam TV kufanya hivyo.

Mahojiano hayo yaliyonukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini yalijikita katika kuichafua klabu ya Yanga pamoja na mpira wa Tanzania kiujumla na kuzua mjadala mkubwa miongoni mwa wafuasi wa soka.

Azam Media wanapaswa kujitokeza hadharani na kuomba Radhi kwa upuuzi walioufanya kwani wamechafua taasisi na tasnia ya mpira wetu huu kwa ujumla.

Ukisikiliza interview ya Fiston kalala Mayele imejaa kashifa ya udhalilishaji wa viongozi pamoja na ligi yetu kwa jumla lakini Azam media bila kujali/kuchuja wameipost.

Maoni Yangu: Endapo Azam media wasipoomba Radhi mashabiki wa Yanga na viongozi pamoja na wadau wa mpira basi itafahamika kuwa Azam media watakua wametumika kuichafua Yanga Sc na mpira wetu kwa ujumla.
Wachuje ili iweje? Kama mnaona mayele anawachafua basi jisafisheni kutumia azam hiyohiyo, na clouds waliwachafua kwa kumuhoji feisal
 
Back
Top Bottom