Azam Tv kutoonesha Ligi kuu Tz bara msimu ujao

Na uyaseme hayokwa wasabato na siku yao ya sabato pia usitolee mifano kwa waislam tu !
 
Huu utakuwa unafiki wa khali ya juu..kama World cup iliyomalizika Russia wadhamini wakuu walikuwa mabingwa wa kilevi Budweiser na bado nchi yenye asili ya dini ya kiislamu kama Saudi Arabia na nyinginezo na zimeshiriki ikiwa ni pamoja kuonyesha michezo yote ikiwa na udhamini wa pombe achilia mbali hata hao Azam kureport matokeo ya michezo yoote...iweje leo mtuletee habari hizi za "kipuuzi" napenda kuamini kuwa ni uhongo mtupu na sio kweli
 
Una uhakika bakhresa haendelei kwenye biashara zake?
 
Afunge asifunge atajua mwenyewe kwanza siangaliagi mpira wa kishamba mimi wa bongo hii.
 
Wapewe dstv,tuwasahau hawa azam
Naona Azam wanajisahau watz wengi walinunua king'amuzi kwa sababu ya mpira wa bongo aiseee acha nijiandae kuuza king'amuzi chao wasiletee habari zao za kijinga
 
Anazan yupo uarabuni acha atujaribu na sisi tumuoneshee . tena star times au ving'amuzi vingine wakipanga wataua Azam Tv kifo kibaya sana
 
Swali nje ya mada lakn...hivi kwahyo mashabiki watakaoenda World Cup 2022 Qatar hatagonga Budweiser kama ilvokua Russia!?
Watakunywa mzeee hiyo hizo gharama unazan watafidia vp
 
Anazan yupo uarabuni acha atujaribu na sisi tumuoneshee . tena star times au ving'amuzi vingine wakipanga wataua Azam Tv kifo kibaya sana
Tatizo star time yeye hana mashine za kurekodi na kurusha live zaidi ana studio ya kurusha hewani kilichorekodiwa na watu wengine kama ilivyokuwa kombe la dunia , hivyo akitaka kuchukua kandarasi hiyo inamlazimu anunue vifaa vya kisasa kabisa kwa ajili ya kuonyesha live maana sioni kampuni nyingine yenye kamera bora kama za huyu jamaa mwenye dini yake ambaye anataka kututesa.
 
Wanaona Pombe Ni Dhambi Wakati Nao Ni Wadhambi Tu. Lini Walikuwa Ni Watakatifu Kama Si Unafiki? Wanaogopa Tope Wakati Wanakanyaga Udongo
Kila watu wana taratibu na kanuni zao, ni kama vile tulivyojipangia kusimama wakati kitambaa
kinachoitwa bendera kinateremshwa kwenye Mlingoti, Ni utii wa kulazimishana hivyo usiwalaumu
waliojipangia kanuni zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…